Bakari Mwapachu anyemelea uenyekiti bodi ya ATCL | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakari Mwapachu anyemelea uenyekiti bodi ya ATCL

Discussion in 'Great Thinkers' started by Bulesi, Aug 15, 2011.

 1. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Habari zilizozagaa mtaani ni kuwa Bakari mwapachu, yule mzee aliyeshindwa ubunge na Omar Nundu kule Tanga analobby Kikwete amteue kama mwenyekiti wa shirika la ndege la ATCL. Ukweli ni kwamba kama kweli hawa jamaa wanalitakia kheri shirika hili hawatathubutu kuchagua mwenyekiti wa bodi mchovu kama alivyo Mwapachu.

  Makosa yalishafanywa huko nyuma kwa kumpa uenyekiti Mistapha Nyang'anyi sidhani kama Kikwete atakuwa na ujasiri wa kufanya makosa mara mbili baada ya vioja alivyofanya huyo bwana kuhusu kuwapeleka mahujaji Mecca!! Bakari hostoria ya utendaji wake haioneshi kuwa anaweza kuimarisha shirika la ndege; huyu bwana ni mtumiaji sio mzalishaji.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Aug 16, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nilidhani kishastaafu kumbe bado?
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Aug 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,376
  Trophy Points: 280
  Kwanini wasimpe kaka yake?
   
 4. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #4
  Aug 16, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mkuu,hii tabia ya kupeana peana ndio ilirudisha na inarudisha mashirika mengi ya umma nyuma kimaendeleao/kiustawi, tufike mahali tuanze kuona sura mpya zenye mawazo mapya na uwezo mkubwa( wapo wengi) katika uongozi wa hizi taasisi na sio huu mtindo wa sasa...
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwkjj,
  Bakari ndiye mkubwa. Mdogo wake, Juma, kishapewa ulaji mwingine baada ya kipindi chake kumalizika EAC.
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jasusi, nadhani Mwanakijiji alikuwa na maana ya kuwa huyu waziri Nundu kwavile anatoka Tanga basi anampa kaka yake wanaetoka nae Tanga ulaji; sidhani kama alikuwa ana maana ya Juma mdogo wa Bakari!! Kwani Juma amepata ulaji gani tena zaidi ya kupewa ukugenzi wa Barrick na Exim ambao uteuzi ambao hauhusiani na serikali?
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa alikuwa Mkurugenzi wa ATC enzi hizo alisaidia sana kulinyanyua shirika wakati ule hadi kufikia likaweza kuwa na hadi ya kimataifa. Kipindi alichokuwepo Bakari Mwapachu kulikuwa na mengineer mahiri kama kina Tingitana, Mrima na mwengine sijui nani yule aliyekufa kwa ajali jina limenitoka.

  Pia kulikuwa na makapteni wa kimataifa akina Captain Maruma, Ngandile, na wengineo wote hawa walikuwa wazalendo walioweza kulinyanyua shirika na kuwa la kimataifa kwani shirika lilikuwa likiendeshwa kwa usomi zaidi na ufanisi na sio ufisadi. Alipoondoka huyu jamaa ndio shirika likaanza kufa hasa alipokuja yule Sanare. Jamaa hawa walitimka mpaka shirika likabaki halina watu makini.

  Sasa hivi wamemteua mtu wao wa system Chizi sijui itakuwaje yangu macho.

  Wakati mwengine tuwe wakweli kama jamaa anafikiria kumteua nadhani jamaa ana nia safi ya kulifufua shirika hilo ila akiwa chini ya Chizi sijui kama atafanikiwa but huwezi pengine huyo CEO amebadilika sio yule nayemjua mimi enzi zile. Ni afadhali JK angeliwatafuta wale wazalendo waliokuwa ATC zamani kabla hajaondoka mwapachu ndio wakaliendesha shirika kama bado wako wazima.
   
 8. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Shirika la ATCL lilifanya vizuri sana enzi za marehemu Sanare na sio enzi za Bakari Mwapachu; wakati wa Bakari yeye aliweka kipaumbele cha kuajili wanawake mashombe tu kama kawaida ya wapenda mabibi!!
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sanare aliua shirika la ATC . Jamaa alikuwa akiajiri ndugu zake kutoka kule kaskazini na kuongoza shirika kwa majungu na vimwana. Ndio maana KLM walikuwa na ushirikiano na ATC wakakimbia hali ya kwamba walikwishajenga bohari ya kufanyia repairs ndege zao pale Terminal one. Isitoshe kuna wale Scandinavian walikuwa na ushirikiano na ATC wakakimbia.

  Bakari Mwapachu alilichukua shirika likiwa hoi from East African Airways likiwa na ndege moja kama sikosei na alipoondoka shirika lilikuwa na ndege zaidi ya 15 Kubwa na ndogo. Sanare ndio alikuwa mpenda mabibi!!!!

  Aliingia akikuta shirika liko hai na ndege nyingi kaondoka shirika lina ndege za kuhesabika na magofu kwani KLM waliamua kuwaachia ATC bohari yao pale Terminal one, baadhi ya wazungu waliokuwa wakisaidia ukuaji wa shirika walitimka baada ya kuona mizengwe imezidi ATC, Wazalendo nao wakasepa.

  Sanare alianza kuua shirika, Mataka akamalizia kabisa msumari wa kaburi lake. Sio Mwapachu huyu mzee ni British (mzungu) na anapenda wasomi na sio vizee vya majungu kama waliofuata nyuma yake.
   
 10. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu unaemtetea kwanza amezeeka na amechoka sana na kumpa majukumu kama ya kufufua maiti ya ATCL itakuwa kumuua na yeye; rekodi yake ya utendaji sehemu zote alizopitia ni matanuzi tu tokea alivyokuwa BIT, halafi NIC na baadae Kampuni ya ndege kote aliacha rekodi mbaya. Kama ni nduguyo it is too bad, jamaa hawezi kuhimili mikiki ya management style ya leo na ndio maana hata ubunge alishindwa.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie nazungumza na facts kwani nafahamu performance ya Sanare alipokuwa ameingia ATC na Pia performance ya Mwapachu ATC alipoichukua from East African Airways. Huwezi kuwalinganisha kwani Sanare aliua shirika yeye na vimwana wake. Uzee sio hoja kwani Warren Buffet mbona mzee wa miaka 81 na he is still the second richest guy in the world and the leading and most sucessful investor.

  Hili shirika linahitaji watu makini kulifufua na sio matapeli kama Sanare na Mataka who took the company into its knees. Mwapachu na team yake ya Tingitana, Ngalesoni, Mrima, Maruma, Ngandile ilikuwa imekamilika na shirika lilikuwa vizuri sana na kutengeneza portfolio mpaka ikawa na recognition internationally (IATA status). Waliposhika akina Sanare ndio ufisadi ukaanza kwenda mbele.

  Mwapachu hanijui wala hanifahamu ila naifahamu rekodi yake ATC vizuri sana. Huko kwengine sio mada husika tunachojadili ni ATC uliza mtu yeyote aliyekuwemo East Africa Airways na ATC under Mwapachu utasikia rekodi yake. The last time I check under Mwapachu ATC ilikuwa inashindana na Kenya Airways kwenda Nchi za Ulaya. ATC imeporomoka mpaka kuwa shirika halifai hata kurusha ndege kwenda Zanzibar bure kabisa!!

  Hili shirika linawahitaji hawa wazalendo waje kulifufua hili shirika hata kwa kuwakodi kama bado wapo hai kwani ndio waliolinyanyua shirika likaja kuliwa na wenye meno. Maana walikuwa wazalendo kweli na ndio maana yalipoanza mambo ya kifisadi wengi wao walikimbia. Wewe kama una undugu na Sanare I am sorry but the guy aliboronga sana ATC ndio maana hakukaa muda mrefu ATC.
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ningekushauri uisome zaidi historia ya Warren Buffet ili uwe na uelewa wa kuweza kujua watu wa kuweza kumfananisha nae. Warren Baffet ni mtu mtafutaji na akishapata anazitumia rasilimali zake kwa umakini mkubwa sana; sasa hawa wabongo unataka kuwafananisha nae life style yao sio ya kutafuta bali kutumia kile kilichopo , hiyo mindset ya matumizi bila mpangilio ndio waliyoizowea toka wakiongoza mashirika ya umma waliyoyafilisi.

  Warren Baffet ni mtu aliyekulia kwenye private sector kwahiyo he is wary of the bottom line ya kampuni zake unlike hawa jamaa waliofilisi mashirika ya umma ambao mindset zao ziko kwenye matumizi tu in the hope kuwa watasaidiwa na serikali.

  Tunahitaji viongozi kwenye kampuni yetu ya ndege ambao ni energetic na wenye mindset ya kulitoa shirika toka utegemezi wa ruzuku toka serikalini mpaka kuwa shirika ambalo litajitegemea na kutengeneza faida a' la Warren Buffet companies.

  Sidhani huyo unayemtetea ana attributes hizo na ndio maana cotribution yake kwa maendeleo ya Tanga urban for the ten years he was their member of parliament ni insignificant hence kushindwa kwake kutetea kiti cha ubunge.
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndinani,

  Sihitaji kuisoma historia ya Warren Buffet kwani nishaisoma tayari. Nafahamu tangia alivyoanza kuuza magazeti akiwa kijana Mdogo sana mpaka kuja kupewa jina la the oracle of Omaha. Lakini wewe hoja yako kubwa ni uzee na ukaihusisha na ufanisi ktk Shirika la ATCL. Ndio nikakuambia uzee sio kigezo bali competence is what matters ndugu. An average age ya director ya makampuni makubwa USA na UK ni 50-60 years si umri mdogo huo. Lakini jamaa hao wanawachagua katika boards wanasababu wanafahamu kwanini wamewachagua na sababu mojawapo ni including performance ya mtu kipindi alipokuwa mwajiriwa wa kampuni.

  Bakari Mwapachu hakuna CEO Wa ATCL anaweza kumfikia in terms of his performance ndugu usimchafue Mzee Wa watu bure. Si sanare aliyekuja kuuza zile nyumba za masaki. Ole Kambaine (huyu ndie the worst kabisa alifilisi kila kitu pale ATCL) au Mataka. Na Mwapachu alifanikiwa kwa sababu alikuwa na vijana wake waliokuwa wazalendo na dedicated na kazi zao na taaluma zao. Vijana hao aliwaomba kwa kushirikiana na rais wahame kutoka Nairobi (yalipokuwa makao makuu ya East African Airways) kwenda Tanzania kuanzisha Shirika la Ndege la Tanzania. Nao walikuwa Maruma, Tingitana, Mrima, Ngalesoni, Ngandile, na Wengineo.

  Alivyoondoka Mwapachu Shirika likaanza kupoteza mwelekeo na kuelekea kufa kabisa. Sasa hivi Chizi ni kama analisuka upya Shirika unafikiri ni anafaa kuwa mwenyekiti wake kama sio Mwapachu? Mtu aliyekuwa na ufanisi mzuri ATC? Ushauri wasiishie tu kwa hao bali wawatafute hawa jamaa kwani ndio walikuwa moyo wa shirika. Kuna mdachi mmoja siku anaondoka baada ya kumaliza muda wake wa kazi alimwambia Mwapachu ukipoteza vijana wako Shirika litakufa. Kuangalia aliona mbali kwani walipoondoka hawa shirika lilikufa kifo cha mende. Wawatafute kuwasaidia kulisuka tena shirika angalau liwe na ndege mbili tatu au 15 kama ilivyokuwa wakati wa Mzee Mwapachu.

  Mwapachu msimchafue bure waliomuharibu ni washauri wake waliomuingiza mkenge aingie ktk siasa but the guy alipokuwa ATC aliperform vizuri sana na anajua kiini cha kufa kwa ATC. Waulizeni waliokuwa ATC zamani watakuambieni msizungumze msioyajua wakuu.
   
 14. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Nafurahi kuwa unakubali kuwa competence ni muhimu ili kulifufufa shirika ; swali langu kuhusu Bakari Mwapachu ni kwamba hiyo competence aliyonayo inaonekana akiwa kwenye kampuni ya ndege tu na sio mahala popote pengine ikiwa ni pamoja na Ubunge?

  Shirika hili limekuwa na mwenyekiti wa bodi Mustapha Ny'ang'anyi ambaye nae alijigamba kuwa ALIPOKUWA WAZIRI WA MAWASILIANO ENZI YA MWALIMU NDIYE ALIYENUNUA NDEGE ZOTE ZA ATC WAKATI HUO; akapewa kuwa mwenyekiti wa board ya ATCL.

  Je unayajua madhara shirika iliyoyapata chini ya uongozi wake juu ya kujigamba kote huko? Wote hawa wawili walikwenda kuomba ubunge sehemu wanazotoka na wote wawili wakakataliwa na wananchi!! Kule wanakotoka wananchi wanawaelewa uwezo wao kuliko mimi na wewe. Hawa jamaa waache waende wakawalee wajukuu zao na kunywa whisky zao, huu sio wakati wa kuchezea maisha ya WaTanzania.

  Kama hawakutengeneza maisha yao ya kustaafu wakati ule basi imekula kwao wabakie kuswali tu mwenyezi atawaonea huruma mbele ya haki. Mikutano siku hizi inafanywa kwa kutumia lap-top sijui hata kama huyo mzee wako anajua kudonyoa key board!
   
 15. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndinani,

  Mustafa ni opportunist na mwanasiasa. Hivi wewe unajua Bakari Mwapachu alikuwa akinunua ndege za Shirika from its own pocket??? (Yaani walikuwa hawapewi pesa na serikali kununua ndege?)

  Alilichukua shirika from East Africa Airways nadhani likiwa na ndege hazizidi 2 au 3 ameondoka shirika likiwa na ndege zaidi ya 12-15 kama sikosei zikisafiri locally and Internationally. This guy is exactly what we need right now ukiondoa siasa zinalozizunguka hilo shirika. Huyo waziri anasema alinunua ndege pengine angelizitaja hizo ndege alizozinunua na pesa zimetoka wapi?? Huyu jamaa Mwapachu ni competent na anafaa .

  Hata hivyo mafanikio ya Mwapachu haikuwa yeye peke yake bali na wale vijana aliotoka nao East African Airways kama nilivyosema mwanzo. Hawa jamaa nafikiri walipelekwa kusomeshwa urusi na nchi za mashariki walirudi na maadili ya uzalendo, ufanisi na utendaji kazi wa hali ya juu. Ndio chachu kuu hata ATC ikawa inakubalika kimataifa na hata KLM iliamua kujenga hangar ya ndege zake pale Dar kwani walikuwa wanasema hakuna waatalamu wazuri wa masuala ya ndege Africa kama walioko ATC.

  Tanzania inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno hakuna zaidi ya hapo. But time has changed nowadays vijana makini wako pale ila nafikiri wangeliwatafuta hawa jamaa kwakuwa walishirikiana na Mwapachu kulisuka shirika bila shaka wanaexperience ya kutosha kusaidia kulisuka tena hilo shirika kama kweli wana malengo ya kulifufua tena hilo shirika.

  Ila mkuu Mwapachu na Team yake aliyotoka nayo East African Airways was the best cream they have had. I just wish wangelipatikana wote ile dream team ikasaidia kulisuka tena lile shirika I used to feel proud kusafiri na shirika la ndege la nchi yangu but she is not there anymore. Siku hizi unapanda mashirika ya wenzetu ukinyanyasika na huduma mbovu, dharau na kejeli kibao wakati shirika la kwetu lilipokuwapo enzi zile hawa jirani zetu walikuwa wakituheshimu.

  Mustafa labda alinunua dege lile la mtumba lilokuja masaa 48 na kushindwa kufanya kazi na kugeuza kipindi cha Rais Ali Hassan Mwinyi. Nakumbuka ilikuwa Boeing kama sikosei 707 au 7 series gani ila lilikuwa used na halikuwa na uwezo wa kufanya kazi kabisa. Mwapachu na team yake walikuwa wananunua ndege brand new. Niliwahi kihudhuria ufunguzi wa Ndege moja aina ya Fokker Freindship ndege ilikuja brand news na makaratasi yake ya plastic (yaani viti vyake). Ndani ya ndege ulikuwa unasikia harufu ya upya na walikuja na wataalamu wao kutoka Amsterdam kuja kuhakikisha ndege inafika salama. Acheni jamani msizungumze msiyoyajua narudi ATC imejengwa na Mwapachu na ile timu yake from East African Airways. Alipoondoka ikawa sio ATC tena bali shamba la bibi ambalo akina captain Aziz na Sanare, Kambaine , Mataka na wengineo wakijitafunia tu mpaka lilipokufa.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Jasusi ana kila sababu ya kushangaa kuwa huyu bwana kumbe bado hajastaafu!! Bakari Mwapachu ni mmoja kati ya watedaji wa Mashirika ya Umma ambae alianza kufanya kazi enzi za Mwalimu Nyerere na ametumikia nyadhifa mbalimbali serikalini katika awamu zote za serikali ya muungano toka nchi hii ipate uhuru!! Mimi ningetegemea huyu wakati huu angekuwa anapumzika baada ya kulihudumia Taifa kwa miongo yote hiyo huku akifurahia pension yake. Sio jambo jema watu wenye umri mkubwa kutaka kufanya kazi za kutumwa tumwa maisha yao yote kwani hiyo inaweza kuleta athari kwa afya za wahusika na wakashindwa kufaidi matunda ya kazi zao. Nasema hivyo nikiwa na mfano hai wa mzee mmoja aliyelitumikia Taifa la Tanzania kwa muda mrefu na kwa umakini sana hata muda wake wa kustaafu ulipofika aliendelea kufanya kazi za mikataba na mwishowe stress za kazi zikamzidi akapata STROKE na hivi sasa ni mahututi hajiwezi. Wazee wetu ni vyema wakajifunza utamaduni wa kukubali kuwa wakati wao umepita vijiti wawape vijana walisukume gurudumu la maendeleo la Taifa kwani kutofanya hivyo ni hatari kubwa kwa afya zao na matatizo kwa familia zao. Kama huyo Bakari Mwapachu bado ana nguvu aanzishe kampuni yake [ Kama anavyofananishwa na Warren Buffet} na atumie uzoefu wake kuindesha na kuajili vijana wetu wengi wanaohitimu vyuo vikuu lakini hawana kazi; badala ya kulobby apewe kazi wakati alishaomba apumzishwe uwaziri sababu ya uzee wakati baraza la mawaziri lilipobadilishwa [Hii sababu ilitolewa na Rais kwanini aliwatema] Mimi nadhani ni sahihi kumtanbua Bakari Mwapachu kama mwanasiasa kama alivyo Mustapha Nyang'anyi na ndio maana alikuwa mbunge wa Tanga mjini kwa miaka kumi.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Question utendaji usiquestion umri wako hayo ni majungu tu na vijiba vya roho na husda. Kama angelikuwa mwapachu mzee na hakuwa kiongozi mzuri mwenye mawazo yatakayoleta mabadiliko yeyote ningelikubaliana na wewe. Ila kama huna cha kuqestion performance yake na ufanisi wake kazini basi hayo ni majungu.

  Bakari Mwapachu is the best CEO by performance ATC tangu kuundwa kwake. Mafisadi ndio waliomtoa pale kwani alikuwa akiwabania wao na wasaidizi wao waliokuja na kampuni zao kihindi za uchwara kuja ati kusaidia kuboresha ufanisi kumbe ni mirija ya ufisadi. Kama huna points za kuuliza utendaji wake tafadhali kaa kimya kwani hamuifahamu ATC ilivyokuwa na inaelekea labda umetumwa kuanzisha thread ya kumchafua mzee wa watu. Ukitaka kumfahamu huyu mzee kaulize wazee waliokuwa wamefanya naye kazi kuanzia subordinates wake ofisini pale ATC mpaka dereva wake watakuambia alikuwa mtu wa aina gani. Nimewauliza ni CEO gani wa ATC aliyewahi kununua ndege mpya kwa fedha za kampuni, kujenga nyumba za kwa ajili ya staff wake kule Masaki, Oysterbay, Mwenge, Mikocheni , Msasani, Mwananyamala. Nyumba hizi wamejenga kwa fedha za shirika pasina mkono wa serikali hata senti tano.

  Would you rather select a bogus Chairman au a chairman who had a good track record during the time he was as an employee of the corporation? Acheni majungu nyie hamuijui ATC Bakari Mwapachu was a best CEO ATC by performance kuliko hao wengine waliomfuatia.
   
 18. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hapa hakuna majungu ni ukweli tu kuwa jamaa kachoka na ndio maana utendaji wake kama mbunge ulikuwa hafifu kama inavyodhilishwa na rekodi za Hansard kwa miaka kumi ya ubunge wake; kama anaona hana kitu cha kufanya maana amechoka kuangalia luninga nyumbani tungemshauri afanye wenzie wanayofanya kama kujishuhulisha na charities za kuwasaidia wenye matatizo kwenye jamii. Wazo jingine ni kama anaipenda sana ATCL he should take up the challenge given by the minister of transport to harness local capital and buy a subtantial stake into ATCL!! Sasa Bakari Mwapachu kama ana business acumen awakusanye wastaafu wenzie watafute huo mtaji [ hata ikiwezekana kutokana na hizo walizolimbikiza toka mashirika ya umma] na wawekeze kwenye kampuni ya ndege [ As long as hawawi kama NICO]. Yeye akiwa na stake kubwa atakuwa ndio Warren Buffet wao na kama itafanikiwa kuifufua ATCL then kampuni yao ndio itakuwa BERKSHIRE HATHAWAY ya Tanzania na yeye kuwa THE ORACLE FROM TANGA na Mwenyekiti wa kampuni bila kulamba lamba miguu ya wadogo zake ; ni aibu mtu mzima kuwaangukia wadogo zako ki umri. The best CEO wa ATC by perfomance alikuwa Sanare na ndio maana alipelekwa kwenda kuanzisha TRA!!
   
 19. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sanare alipoenda TRA ilikuwaje? Bora hata Kitilya alileta mabadiliko kipindi cha Sanare TRA ndio ilikuwa watu wanakufanya shamba la bibi hata kodi hawalipi. Sanare alikuwa bogus CEO pale ATC ndio maana aliisababishia ATC hasara mpakaa wakaanza kuuza asset zao. Alikuwa akikumbatia majungu na mambo mengine yasiyo na msingi matokeo shirika likaanza kumfia yeye mkononi. Halafu unachekesha kweli unasema Sanare alikuwa besti CEO tuambie alipolichukua shirika alilikuta wapi na alipoondoka aliliachaje kama hujachekwa? Sanare alikuta ndege 15 kaondoka shirika linachechema na vindege vinne tu vyengine kauza kwa jamaa zake na rafiki zake. Bakari Mwapachu is the best CEO of ATC by performance ndugu alikuta shirika changa na akaligeuza na kuwa shirika kubwa na la kimataifa likiweza kushindana na mashirika kama Ethiopian Airlines, Kenya Airways na mengineyo Africa. Leo hii ATC mnashindwa hata na Precision Air you make me sick!!!!!

  Umesema mwapachu akaanzishe shirika lake na wastaafu wenzie. Warren Buffett ilimchukua almost a decade if not two decade to build a sucessful company. Na hata kama mwapachu akianzisha shirika lake litakuwa lake hili ni shirika la umma la kwetu sote hivyo mimi, yeye na wewe tuna haki na the last time I check serikali imesema litaendelea kuwa shirika la umma. Wangelifanya la busara serikali ingeliamua kuruhusu ATC iuze shares zake to the public ungeliona kiama cha mafisadi. Wairuhusu ATCL iwe listed watatokea wazalendo watalinyanyua shirika ila sasa hivi litaendelea kuwa shamba la bibi.
   
 20. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  <br />
  <br />
  Habari za ulaji na upenda mabibi inamhusu Bakari waulize waliofanya kazi RTC kiwa BIT mkuu
   
Loading...