Bodi ya ATCL yaivunja Menejimenti ya Shirika hilo

Bodi ya ATCL yaivunja Menejimenti ya Shirika hilo

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Habari zilizonifikia ni kuwa Menejimenti ya Shirika la Ndege ATCL imevunjwa ili kukidhi vigezo na haja za Shirika hilo na malengo yaliyowekwa kwa miezi 8.

Imeamuliwa Wakurugenzi Wote na baadhi ya Mameneja waondolewe mara moja (Isipokuwa Mtendaji Mkuu aliyeajiriwa hivi karibuni) hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo utendaji dhaifu, viwango hafifu vya elimu kinyume na matakwa ya nafasi hizo na uadilifu.

Aidha wakurugenzi na Mameneja waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali imeamriwa warudishwe kwenye ngazi zao za chini.

Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu atangaze nafasi za Wakurugenzi, Mameneja na nafasi nyingine atakazoona zinafaa kutafutiwa wafanyakazi wapya.


​

=======
UPDATE

Hata hivyo hatua zaidi zitachukuliwa kwa mawakala wa kukatisha tiketi kwakuwa utaratibu uliokuwepo hakuangalia maslahi ya shirika na ikithibitika hakuna ulazima wa kuwatumia mawakala basi kutakuwa na zoezi la kubatilisha mikataba ya mawakala na kuwatumia wafanyakazi wa Shirika.

​


Mwenyekiti wa bodi ATCL amedai shirika lilikuwa linakopa sana zamani na sasa wachofanya ni kulipa madeni ya zamani

​


Wamesema wamepunguza sana matumizi yasiyo ya lazima na wana mpango wa kuongeza safari za ndani za Kilimanjaro na Mtwara, pia wamefanikiwa kuongeza mapato ya ndani yatokanayo na mizigo iliyozidi
Pia wanadhibiti utolewaji wa tiketi za bure unaotolewa kwa wafanyakazi wa shirika ambao unaonekana kutumiwa vibaya na wafanyakazi


​

Pia amesema wamejitahidi kutatua changamoto mbalimbali kama ucheweshaji wa ndege na wanaendelea kutatua changamoto ya uhaba wa marubani ambapo hadi sasa marubani wanne wamemaliza mafunzo na wengine wanne wanatarajia kumaliza mafunzo mwishoni mwa mwezi huu mafunzo hayo yanacchukua muda kwa kuwa yanategemea ndege mpya mbili tu.

Awamu ya mwisho ya ukamilishaji wa mafunzo inatarajiwa kumalizika mwezi Disemaba ambapo itaifanya ATCL kuwa na marubani 13.

======
Baada ya kuanza safari zake Octoba 14 2016,Shirika la Ndege la ATCL limekili kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo ucheleweshaji wa ndege na kutoa huduma katika maeneo ambayo yalipaswa kuhudumiwa.

Akitoa changamoto hizo,Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo,Mhandisi Emmanuel Korosso amekili kuwepo kwa changamoto ya Marubani katika Shirika hilo ikizingatiwa mpaka sasa Shirika hilo linatarajiwa kumaliza mafunzo ya Marubani 13 katikati ya mwezi Desemba.

Amesema kuhusu Wafanyakazi Bodi yake imeagiza Menejimenti ya Shirika kusimamisha kwa muda mkataba wa hiari ambao unatoa mwanya kwa wafanyakazi kutumia vibaya ruhusa za matumizi ya tiketi za bure.

"Katokana na haja ya kuboresha Utendaji, ATCL iliamuliwa Wakurugenzi wote katika Menejimenti ya ATCL isipokuwa Mkurugenzi Mtendaji,na baadhi ya Menejimenti waondolewe katika nafasi zao Mara moja kutokana na Utendaji dhaifu na viwango vya Elimu visivyokidhi matakwa ya nafasi zao",amesema Mhandisi Korosso

"Tumeamua wakurugenzi wanaokaimu nafasi zao warudishwe katika nafasi zao za chini ambazo siyo za Menejimenti au wahamishiwe katika vituo vya mikoani",ameeleza Mhandisi Korosso

Aidha,Wakurugenzi na Menejimenti waliokuwa wamethibitishwa tumeagiza waondolewe ATCL ili wapangiwe majukumu mengine kulingana na sifa zao.

Aidha Bodi imemuagiza Mtendaji Mkuu kutangaza mara moja nafasi zote za Wakurugenzi na pia nafasi za Mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo wa muda uliopitishwa na Bodi (Interim Organization Structure).

Pia Mtendaji Mkuu ameagizwa kutangaza nafasi zozote ambazo anaona kuna umuhimu wa kuajiri watu wengine kutokana na utendaji usioridhisha wa wafanyakazi wanaoshikiria nafasi hizo kwa sasa.

Chanzo: Michuzi Jr
 
Sawa,nakumbaka kunamtu alikua anashauli hivyo kupitia humu,naona wamemsikia.
KUMBE ANASHAULIKA SASA,MSEME JINGINE.hahahahahahahaha
 
Hopefully they will accommodate the sock peacefully
 
ATCL Hoyeeeeeeee...ATCL Juuuuu...... haya ndio mambo tunayoyataka watanzania wa leo...hatutaki bla blah...tena wale watu wa marketing ndio wawe wa kwanza kufukuzwa....ivi inakuaje adi leo hawana page humu jf?? shutuma zao wanazijibia wapi>>?? mi stak
 
Safi sana kulikuwa hakuna elimu inayotakiwa kwa watendaji wa juu,wengi wameungaunga,ni vizuri kufukuza wote
 
Ngoja tu nibaki huku najilimia zangu mpunga ninaweza kutoka kimaisha kuliko kuajiriwa maana sijui kesho yangu itakuaje!!

Tangazo kama kuna mtu anahitaji shamba la kukodishwa tuonane pm.
 
Uamuzi huu wa kuifutilia mbali manegement mbovu ya ATCL umekuja kama wadau wengi walivyoomba ingawa wamechelewa sana, ile manegement ilishakuwa kama mtoto nunda CAG kasema, Rais kasema na waziri wao kasema lakini hakuna hatua iliyochukuliwa, yaani walikuwa wanaona kabisa wanachimbiwa kaburi lakini wao wamekaa kama ngamia asubiri achinjwe
 
Mimi nafikir sio elimu watu wamechoka serikali wali isusa shirika na tusifikirie shirika la ndege linataka madigrii hapana sita.iosa.icao ni elimu ambayo inajitegemea kwenye airlines sasa kwa tz itakuwa ngumu ndo maana airlines kama Qatar air. Emirates Na hao rwanda air kuna wageni wahindi wazungu Na kila mwenye ujuzi ili kuensesha shirika sisi watz tuna usiasa ndani so kufanikiwa ni kugumu sana bil qualified staff Na sisi tz hatuna watu hao waliokuwepo ni watu wazima mfano engineering mtu wa chini ana miaka 60 watu waliosoma airlines education wachache leo tz ukitaka manager airline quality uwezi kumpata nje ya hao wazee sasa wacheni siasa tafuteni watu wa maana tuanze biashara!!!!
 
Ngoja tu nibaki huku najilimia zangu mpunga ninaweza kutoka kimaisha kuliko kuajiriwa maana sijui kesho yangu itakuaje!!

Tangazo kama kuna mtu anahitaji shamba la kukodishwa tuonane pm.
Huko kwenu mvua imenyesha? Hapa nilipo jua kali sana! Nimefika Dar nikakuta watendaji wabovu kama hawa wa ATCL wameruhusu mafuriko ya kinyesi, wao wanaita ni mvua!
 
Back
Top Bottom