Bajeti Kuu, 2023-2024: Wanafunzi wa kidato cha Nne wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye Vyuo vya Ualimu, Afya, Sayansi, Ufundi wapewe mikopo

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,240
4,326
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kuanzishwa kwa programu ya mikopo kwa Wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye Vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu”

“Kufuatia mabadiliko ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014, toleo la Mwaka 2023 na mabadiliko ya mitaala yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sira chini ya uongozi shupavu wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri wa Tanzania, ambapo Serikali inalenga kutoa elimu ya amali kwa ngazi zote kuanzia Shule za awali, elimu ambayo itamuwezesha Kojana wa kitanzania kujiajiri au kuajiriwa na hivyo kutoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa”

“Hivyo, napendekeza kuanzisha programu ya mikopo kwa Wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye Vyuo vinavyotoa elimu katika fani za kipaumbele ambazo ni sayansi, afya, ufundi na ualimu, hatua hii itaanza na Wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa masomo wa 2023/24, MAMA yuko Kazini”

“kwa upendo wa MAMA yetu hakuishia kwenye mikopo ya Wanafunzi tu, pia aliamua kuongeza kiwango cha posho ya kujikimu maarufu kama Boom kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu kutoka shilingi 8,500 hadi shilingi 10,000 kwa siku”

“Mafanikio mengine ni pamoja na kujengwa kwa vyumba vipya 27,235 vya madarasa ya msingi na sekondari ikijumuisha madarasa 15,000 ya UVIKO-19, madarasa hayo pia yanajumuisha madarasa 8,000 ya Sekondari yaliyojengwa kwa shilingi bilioni 160 iliyotolewa kupitia Pochi la MAMA ili kukabiliana na ongezeko la Wanafunzi wa kidato cha kwanza”
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba leo June 15,2023 amewasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Bungeni Jijini Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyapendekeza kwenye hotuba yake ni kuanzishwa kwa programu ya mikopo kwa Wanafunzi wanaochaguliwa na Serikali kusoma kwenye Vyuo vinavyotoa elimu katika fani
Wazo zuri sana wabunge tunaomba muipitishe hiyo bajeti Ili tupeleke maendeleo kwa watanzania
 
Bilioni 160 ilitoka kwenye POCHI LA MAMA!! Mmeiona hiyo? Na kwenye bajeti ya leo mmesikia bajeti ya pochi hilo? Au kwa vile siangaliagi tbc?
 
Mnataka kuwapatia zigo zito la madeni pindi wamalizapo masomo na kupata kazi, si nzuri kabisa hii.
 
Ni lini Serikali itaanza kutoa Mikopo hiyo kwa wanachuo wanaotarajia kujiunga na vyuo vya kati Mwenzi wa 10?
 
Back
Top Bottom