Bahlul amshauri harun

KABAVAKO

JF-Expert Member
Apr 5, 2011
229
32
siku moja Bahrul alimtembelea Khalifa Harun Rashid, akaombwa kutoa nasaha;

Hapo Bahlul alianza:

"Ewe Harun! Iwapo wewe utakuwapo porini ukashikwa na kiu ya maji ambayo hayapatikani, huku ukikaribia kufa. Je utalipa kiasi gani kwa kiasi cha kikombe kimoja cha maji?"



"Sarafu za dhahabu (Dinar)!" alijibu Harun.



"Iwapo mwenye maji asiporidhia sarafu hizo, je utampa nini badala yake?" aliendelea kusema Bahlul.



"Nitampatia nusu ya dola yangu" alikatiza Harun kwa haraka.



"Naam, baada ya kumalizia kiu chako, ukashindwa kupata mkojo (ukaziba) nawe usiweze kujitibu, je utampa nini yule atakaye kutibu huo ugonjwa?" Alisema Bahlul.



"Nitampatia sehemu ya nusu ya dola yangu iliyobakia"Harun akanena katika hali ya bumbuwazi.



Basi hapo kwa kupumua, Bahlul alisema: "Ewe Harun! Usijivunie Ukhalifa wako ambao unajua uthamini wake ni sawa na kikombe cha maji na uponyaji wa ugonjwa wako. Hivyo, ni kheri yako iwapo utawatendea watu wako kwa upole na haki!"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom