Ng'wanapagi
JF-Expert Member
- Sep 18, 2013
- 9,116
- 8,662
Ni mara ya tatu sasa nikiwa narudi nyumbani hupenda kulala Mwanza hotel flani mitaa ya Iloganzala. Wakati nikiwa hapo kwa mara ya kwanza nilishangaa muhudumu akiniongelesha kwa kiingereza pamoja na kwamba nimejiandikisha pale mapokezi kama Mtanzania na jina lenyewe halihitaji utafiti kufahamu kuwa mimi natokea wapi.
Nilipotoka matembezi mida ya saa mbili usiku nilikuta hata miziki inayopigwa hapo ni ile ya kimagharibi (kiingereza) hadi naenda kulala hakuna mziki wowote wa asili ya Tanzania uliopigwa. Hivyo hivyo safari ya pili kulala hapo nilishuhudia hayohayo japo niliona tofauti ya kuongeleshwa kiingereza kama safari ile ya kwanza japo hakuna mziki wenye mahadhi ya Kitanzania (Kiafrika) ulipigwa.
Awamu hii yamejirudia yaleyale hadi nikatamani nimuombe meneja aweke angalau hata kibao cha OTTU lakni sikuona Mtanzania mwezangu yoyote aliyeonyesha kukerwa na tabia hii. Nilijiuliza kwa nini Wasouth Afrika ambao wamechanganyikana na wazungu wanapenda sana miziki ya asili yao?
Hongereni kwa uongozi wa kivuko cha Busisi kwa kutupigia nyimbo zilipendwa za Bimale Orchestra na abiria kujisikia tuko nyumbani