Bado Watanzania hatuna elimu ya uzalendo

Bado Watanzania hatuna elimu ya uzalendo

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2013
Posts
9,116
Reaction score
8,662
Ni mara ya tatu sasa nikiwa narudi nyumbani hupenda kulala Mwanza hotel flani mitaa ya Iloganzala. Wakati nikiwa hapo kwa mara ya kwanza nilishangaa muhudumu akiniongelesha kwa kiingereza pamoja na kwamba nimejiandikisha pale mapokezi kama Mtanzania na jina lenyewe halihitaji utafiti kufahamu kuwa mimi natokea wapi.

Nilipotoka matembezi mida ya saa mbili usiku nilikuta hata miziki inayopigwa hapo ni ile ya kimagharibi (kiingereza) hadi naenda kulala hakuna mziki wowote wa asili ya Tanzania uliopigwa. Hivyo hivyo safari ya pili kulala hapo nilishuhudia hayohayo japo niliona tofauti ya kuongeleshwa kiingereza kama safari ile ya kwanza japo hakuna mziki wenye mahadhi ya Kitanzania (Kiafrika) ulipigwa.

Awamu hii yamejirudia yaleyale hadi nikatamani nimuombe meneja aweke angalau hata kibao cha OTTU lakni sikuona Mtanzania mwezangu yoyote aliyeonyesha kukerwa na tabia hii. Nilijiuliza kwa nini Wasouth Afrika ambao wamechanganyikana na wazungu wanapenda sana miziki ya asili yao?

Hongereni kwa uongozi wa kivuko cha Busisi kwa kutupigia nyimbo zilipendwa za Bimale Orchestra na abiria kujisikia tuko nyumbani
 
Tuna safari ndefu sana kama taifa kutoka hapa tulipo!
 
Wewe pia huna elimu ya uzalendo, ndio maana ukakaa kimya tu huku unaona mambo hayako sawa,
 
Miziki yakibongo inafungiwa nabaraza, bongo movie bongo lala serikali inachangia kuwanyong'onyeza wasanii wabongo kwa sababu nyepesi MTU kaitangaza nyegezi katangaziwa tabu!
 
Ukiona hvyo jua hivyo havikuhusu wewe vinawahusu wageni,,hiyo ni biashara ndugu tunaangalia matakwa ya mteja,,sasa wewe kalumanzira umekuja only twice tena umekaa less than 24HRS Unataka tucheze had ngoma za kabila lako?. . Na kuhusu south Africa Dunia inajua yaliyotokea ,,,ubaguzi uliokithiri ndo umesababisha Yale yote yaliyotokea mfanoo tu kulikua na maaneo maalumu ha wazawa na maeneo maalumu ya makaburu,,,,, HOME WORK 1.Nini maana ya mzalendo 2. Taja Nguzo za uzalendo
 
uzalendo hauzuii kuiga, unamaanisha uvipende vya kwenu , na uige vya yule vile vizuri,
hii haina maana kuwa vya kwetu ni vizuri vyote et hata kama cha kwenu kinakera basi ukipende tu kwa mategemeo ya ishara ya uzalendo si kweli.
 
Ni mara ya tatu sasa nikiwa narudi nyumbani hupenda kulala Mwanza hotel flani mitaa ya Iloganzala. Wakati nikiwa hapo kwa mara ya kwanza nilishangaa muhudumu akiniongelesha kwa kiingereza pamoja na kwamba nimejiandikisha pale mapokezi kama Mtanzania na jina lenyewe halihitaji utafiti kufahamu kuwa mimi natokea wapi. Nilipotoka matembezi mida ya saa mbili usiku nilikuta hata miziki inayopigwa hapo ni ile ya kimagharibi (kiingereza) hadi naenda kulala hakuna mziki wowote wa asili ya Tanzania uliopigwa!!!. Hivyo hivyo safari ya pili kulala hapo nilishuhudia hayohayo japo niliona tofauti ya kuongeleshwa kiingereza kama safari ile ya kwanza japo hakuna mziki wenye mahadhi ya Kitanzania (Kiafrika) ulipigwa.
Awamu hii yamejirudia yaleyale hadi nikatamani nimuombe meneja aweke angalau hata kibao cha OTTU lakni sikuona Mtanzania mwezangu yoyote aliyeonyesha kukerwa na tabia hii. Nilijiuliza kwa nini Wasouth Afrika ambao wamechanganyikana na wazungu wanapenda sana miziki ya asili yao!!?

Hongereni kwa uongozi wa kivuko cha Busisi kwa kutupigia nyimbo zilipendwa za Bimale Orchestra na abiria kujisikia tuko nyumbani

Uzalendo mwingine wote ninao kasoro uzalendo wa kutetea serikali!

Thats the most stupid thing to do!

Serikali ijizalendo yenyewe!

I will never ever support any f.ucken government on anything whatsoever!

Any Government is a group of lunatics!

Every governments on the surface of the earth are illegal- Bob Marley
 
Ukiona hvyo jua hivyo havikuhusu wewe vinawahusu wageni,,hiyo ni biashara ndugu tunaangalia matakwa ya mteja,,sasa wewe kalumanzira umekuja only twice tena umekaa less than 24HRS Unataka tucheze had ngoma za kabila lako?. . Na kuhusu south Africa Dunia inajua yaliyotokea ,,,ubaguzi uliokithiri ndo umesababisha Yale yote yaliyotokea mfanoo tu kulikua na maaneo maalumu ha wazawa na maeneo maalumu ya makaburu,,,,, HOME WORK 1.Nini maana ya mzalendo 2. Taja Nguzo za uzalendo
Nimekuelewa mkuu
 
Sijaona uhusiano wa ulichokiandika na uzalendo.
Jamaa angefurahi kama wangemuwekea ngoma za kiduo,mangala,maswezi,msusumio,ngoma ya mpapa au kibao kata.Halafu kila mambo yana nyakati na mahali.Akitokea mlokole atataka na yeye apigiwe nyimbo za aina atakayo.Vilevile wahudumu hawawezi kujua kila mmoja anapendelea nini.
 
Hongereni kwa uongozi wa kivuko cha Busisi kwa kutupigia nyimbo zilipendwa za Bimale Orchestra na abiria kujisikia tuko nyumbani
Hahahaa, Bima Lee ipi mkuu ile ya kina Roy Bashekanako na nyimbo kama Peleleza na Sophi au Bima Lee Magnet Tingisha, Magnet 84 ya kina Marehemu Shaaban Dede na Jerry Nashon "Dudumizi" na nyimbo kama Neema na Shangwe ya Harusi?

Na mimi nijiunge na wewe kumpongeza huyo DJ wa kivuko cha Busisi kwa kuenzi miziki ya nyumbani
 
Uzalendo ni ule wa wale John wawili .........ntarudi baadae
 
Uzalendo ni ule wa wale John wawili .........ntarudi baadae
Ukweli ni kwamba huwezi kudai watu wawe wazalendo kwa maneno mengi bila kuwepo kwa mazingira na vishawishi vya kuvutia watu kuwa wazalendo.

Ukitengeneza mazingira vutia utashangaa watu hawa walikaa wapi kuamua wewe wazalendo hivi.
Ushahidi ni huo wengine kuamua kuwa wazalendo wa tamaduni za kigeni.
 
Kupitia uzi pia ni uzalendo kama mtoto wa john alivyosema kwa john ngoja tuwajengee barabara mpite
 
Jamaa angefurahi kama wangemuwekea ngoma za kiduo,mangala,maswezi,msusumio,ngoma ya mpapa au kibao kata.Halafu kila mambo yana nyakati na mahali.Akitokea mlokole atataka na yeye apigiwe nyimbo za aina atakayo.Vilevile wahudumu hawawezi kujua kila mmoja anapendelea nini.

Mwagito alitaka akute zinapigwa za kina Sumasesu Tololelage Ikhilunga ndio angewaona Wazalendo.
 
Hapawezi kuwapo uzalendo kwa wananchi ikiwa viongozi sio wazalendo. Hao ndo icon tunafanya wanayofanya
 
Jamaa angefurahi kama wangemuwekea ngoma za kiduo,mangala,maswezi,msusumio,ngoma ya mpapa au kibao kata.Halafu kila mambo yana nyakati na mahali.Akitokea mlokole atataka na yeye apigiwe nyimbo za aina atakayo.Vilevile wahudumu hawawezi kujua kila mmoja anapendelea nini.
Kkkkkkkkkkkk!!! Lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom