Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Mimi Nina imani na CHADEMA, mpaka pale chama kama EFF kitakapozaliwa Tanzania,I'm radical, extremist and conservative, kwa sasa Bado ntaendelea kuiamini CHADEMA na kumuamini mheshimiwa Freeman Mbowe,kwa Tanzania ni Mbowe tu anawaweza CCM,wengine siwaelewi.
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
Nyani Ngabu umeongelea matukio mawili ambayo yamenifanya nisiamini uongozi wa Chadema. Nafuatilia siasa sana hasa za hapa kwetu lakini bado sijashawishika kuchukua kadi ya chama chochote. Chadema niliwashangaa sana mwaka jana, lakini sikuwanyima kura kwasababu ya CCM aliyokuwa ameiacha Jakaya. Lakini bado mambo ya ngosha yameanza kutia kinyaa nikadhani kama kweli Chadema wako madhubuti watamkomalia ngosha hadi aelewe nini maana ya demokrasia na vyama vingi. Hiki cha leo nimekiita kinyaa. Best solution wangezuia watu wasiandamane then wangeendelea na mikakati yao mengine. Leo wameprove kuwa ni waoga sana, hata kukamatwa tu kulala sero imewatia uwoga usio kifani. Mbowe aachie uongozi tu waje wenye maoni mapya.
 
Chadema ni watoto wa mjin weka mbali na watoto hawafai hao
 
Nilijua tu kuwa lazima watafunga breki shimoni. Lakini pia siyo mara yao ya kwanza kufanya hivyo.
 
Well said Ngosha,kusema ukweli watakaoendela kuwaamini CHADEMA basi wana hitilafu kwenye
Frontal lobe yao.Watu wazima Adrenaline zao zimepanda kwa mwezi mzima,leo mwishoni kabisa wanaambiwa their workdone is equal to zero.Halafu wanapewa siku 31 zingine tena,bado wamo tu,itabidi wapimwe akili kwa kweli.
Huu sasa ni unaa na unafiki, we si kutwa nzima ulikuwa unakataza wasiandamane leo wasitisha umebadili gia unafiki mtupu
 
Hii ngoma ya ukuta bado mnacheza kweli nyie mtaendelea kuimba tu
 
Tatizo kubwa la CDM ni kwamba ukiwaambia walifanya makosa kumsimamisha Lowasa Kama mgombea Wao wanakuita CCM, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa like lilikuwa ni kosa kubwa, migogoro iliyopo CUF, NCCR na CDM yenyewe chanzo chake kikuu ni Hilo kosa.
Nyie watu wa ajabu kweli,mtu akifanya kosa si anachukuliwa hatua za kisheria?mmeshindwa nini kumshtaki kwa kosa kubwa kama hilo la ufisadi,wakati mnavyombo vyote vya kisheria?

Tumeangaliaweeee tukaona tunapiga kelele bure tuu,basi tukajiridhisha hana kosa.
 
Huu sasa ni unaa na unafiki, we si kutwa nzima ulikuwa unakataza wasiandamane leo wasitisha umebadili gia unafiki mtupu
Wewe ni lini nimewakataza wasiandamane?;hata kama ,inakuwaje intruder abadilishe uamuzi wao?
 
mimi binafsi bado nina imani,naamini viongozi wa chadema wametumia busara kusitisha UKUTA,wananchi wengi wameupinga UKUTA lakini hii ni maafa kwetu sote maana sio muda mrefu mambo yanaweza yakawa magumu kuliko yalivyo sasa hivi na watu watakumbuka kwamba UKUTA ulihitajika na watauhitaji wakati huo.Muda utasema.
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1105908/
 
Back
Top Bottom