Wametishwa na wametishika, maandamano ya leo yalikuwa yanasubiriwa na watu wote wapenda democrasiaHawa CHADEMA ndo basi tena.
Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.
Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.
Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.
Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.
Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.
Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?
Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.
Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.
Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?
Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.
Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.
Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
Mkuu Nyani Ngabu ulikuwa na maslahi gani na maandamano ya leo, na umeathirika kiasi gani baada ya kukuta yameahirishwa?
CDM ni jeshi kubwa sanaMtampiga vita NN
Lakini kawapa ushauri huu upinzani wa sasa umekatisha tamaa wengi
Hakuna agenda za kitaifa na nyeti za kuukuza upinzani na mkichelewa , JPM akianza kutekeleza ahadi zake moja baada ya nyingine mtapotea kabisa
Mnachotakiwa cdm , badilikeni
Zama zimebadilika
ukuta umeporomoka haukuvunjwa bhana [emoji23][emoji23][emoji23]
Kikao kimehairishwa indifinitelyHuu mtego waliowekewa Chadema wangeingia mkenge ndio ungekuwa mwisho wao.
Watanzania tunaongoza kwa unafki, Nyani Ngabu yupo Marekani anataka wenzake wauwawe yeye abaki tu kwenye keyboard.
Nina imani kikao cha msajili kitapata ufumbuzi na mikutano itaruhusiwa kwa vyama vyote.
Malengo ya Chadema kisiasa yamefikiwa hakuna haja ya kutowa sadaka maisha ya watu na kusababishia ulemavu.
Wapo wenye imani na cdm ni wale wenyeakili za kushikiliwaSwali ni bado wapo wenye imani na chadema?
Utaona uvccm wakitumwa kufanya maandamano yao mwishoni mwa mwezi WA Tisa.CHADEMA Walitaka Publicity,na Wameipata!na Hata Kusema Kuwa Watumishi wa Mungu Kuwaomba Watulie Bado ni Kick Nzuri!
Na Mpaka Oktoba Mosi CHADEMA Haita Kauka Vinywani Mwenu!
Hivi Usafi Kesho Unaendelea,ahahaha!
CHADEMA Wametanguliza,wao Wamepiga Kona Fasta!
Sasa Komredi kwa nini usingeandamana? Virungu na washawasha wa Magu?
Damu vipi lakini, ungechangia?