Bado tunakukumbuka Regia Mtema....

Bado tunakukumbuka Regia Mtema....

Pumzika pema GS....
Maisha yanaenda.....na bado unaishi kati yetu..
 
RM2.jpg

Alikuwa mpambanaji na mbunifu sana katika siasa,
We miss you kamanda.
 
We miss you Regia.

Bahati mbaya ile chadema uliyoiacha kipindi kile, sio hii iliyopo sasa.
mambo yamebadilika mno.
viongozi wanatimuana, wanatukanana, wanapelekana mahakamani.
Matamko kila kukicha, wasemaji wa chama wamekuwa wengi.
Mwenyekii alikiri kuwa alipewa pesa na Nimrod Mkono yule mbunge tajiri wa CCM.

Chadema ile sio hii Regia. Rest in peace mpiganaji.

We ni kingwendu kweli acha kuchafua sledi za watu.
 
Hii ni siku ya kumkumbuka mzalemdo na mpiganaji wa Taifa hili aliyetutoka miaka miwili sasa imepita; ni siku ya kuweka naziri ya kuyatekeleza yote yale aliyosimamia wakati wa uhai wake na sio siku ya malumbano. Rest in peace GENDER SENSITIVE.
 
Chadema ni ile ile. Chadema ni moja. Chadema imeimarika zaidi. Regia amefariki hakuacha mgogoro wa madiwani Arusha ulioratibiwa kwa karibu kabisa na Zitto Zubeir Kabwe.
Regia amefariki hakumwacha Zitto Zubeir Kabwe akitumiwa na usalama wa taifa kukiharibu chama ambacho Regia alijitoa kukijenga.
Regia amefariki hakumwacha Zitto Zubeir Kabwe akitukana viongozi wakuu wa chama. Regia alifariki aliacha nidhamu kwa viongozi wake.
Sasa chadema inarudisha misingi yake. Inajenga timu inayowaza mamoja kuelekea kutwaa dola 2015. Inasafisha makapi,makandokando na mapandikizi yote ya CCM.
Chadema ni moja, mwenye kutaka ukombozi wa pili wa Mtanzania na aje!
Wewe ni f...a..ll.a
 
We miss you Regia.

Bahati mbaya ile chadema uliyoiacha kipindi kile, sio hii iliyopo sasa.
mambo yamebadilika mno.
viongozi wanatimuana, wanatukanana, wanapelekana mahakamani.
Matamko kila kukicha, wasemaji wa chama wamekuwa wengi.
Mwenyekii alikiri kuwa alipewa pesa na Nimrod Mkono yule mbunge tajiri wa CCM.

Chadema ile sio hii Regia. Rest in peace mpiganaji.
You nailed it
 
Kila nafsi italala mavumbini Regia umetangulia sote 2talala,,,! Tunakukumbuka dadaetu!
 
Lala salama REGIA. Toka uondoke viongozi wa CHADEMA wanaothubutu kuingiza pua za humu kwa ID zao halisi hawazidi wawili. Ulithubutu kuingia JF mara kwa mara kwa jina lako REGIA MTEMA, kwa hilo tu nakusifu.
 
Na hii ni mojawapo ya Thread aliyoileta Hayati Regia hapa Jamvini kuelezea kile alichokifanya(kwa wakati huo) tangu aapishwe kuwa Mbunge....

Disemba 31, 2011​
Wakuu habari!
Ni matumani yangu kuwa tumejiandaa kumaliza mwaka vizuri na ku-plan vizuri for next year.
Tukiwa tunafunga mwaka nimeona niandike kwa kifupi yale niliyoyafanya kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kuapishwa kuwa mbunge wa vitimaalumu Novemba 12, 2010.
Taarifa hii inaonyesha utekelezaji wa kazi za ubunge, kazi za chama wilayani Kilombero na kazi za chama kitaifa.
A. KAZI ZA KIBUNGE
Tangu nimeapishwa nimefanikiwa kufanya kazi mbalimbali za kibunge wilayani Kilombero, jimbo ambalo niligombea na kupata kura 38,550 sawa na asilimia 45 ya kura zote zilizopigwa. Utekelezaji wa awamu hii ulikuwa ni QUICK WINS. Quick zifuatazo zimefanyika;
  1. Nimepigania bei ya sukari ishuke - kuna maeneo bei imeshuka lakini maeneo mengine hali bado ni mbaya. Kilombero ni wilaya inayozalisha sukari, kiwanda cha Illovo, hivyo bei ya sukari inapaswa kuwa chini kuliko maeneo yasiyozalisha sukari.
  2. Nimepigania kituo cha polisi cha wilaya kiboreshwe – kimeboreshwa
  3. Nimepigania kituo cha afya cha Mlimba kipatiwe maji na ambulance irudishwe hivi vyote vimefanyika. Ambulance ilikuwa gereji zaidi ya miezi sita mwaka 2010.
  4. Nimepigania utekelezaji wa huduma bure kwa wajawazito, watoto chini ya miaka mitano, wazee na wenye ulemavu - kuna maeneo nimefanikiwa lakini maeneo mengi bado.
  5. Nimetetea haki za wafanyakazi wa kiwanda cha sukari na KPL - baadhi ya kero zimetekelezwa lakini nyingine bado - suala la maslahi bado ni tete, suala la usalama kazini bado ni tete.
  6. Nimetetea na kusimamia kero ya wakulima na wafanyabiashara ya kuongezeka kwa ushuru bila kushirikishwa katika hatua zote muhimu.
  7. Nimepigania haki ya umeme kwa wananchi wa Kilombero kwani tuna vyanzo viwili vya umeme, Kihansi na Kidatu.REA imeenda kule ila inasuasua sana lakini wizara imetuhakikishia kuwa inatekeleza azma yake ya kupeleka umeme maeneo yote ya karibu na vyanzo vya umeme.
  8. Nimepigania barabara ya Kidatu-Ifakara kwa kiwango cha lami-imeshindikana kwa mwaka wa fedha 2011-2012.
  9. Nimesomesha wanafunzi 86 sekondari, 13 vyuo vikuu hawa wa vyuo vikuu walihitaji kutoa advance ili waweze kusajiliwa then wapate mkopo.
  10. Nimeezeka madarasa mawili ya shule ya Msingi Mkula.
  11. Nimegharamia visima viwili vya maji.
  12. Nimemuhudumia baba aliyekuwa kipofu kwa miaka nane akaweza kuona tena kupitia Hospitali ya CCBRT.
  13. Nimesaidia wagonjwa wengine zaidi ya 42 wakapata huduma za afya na kupona.
  14. Nimesaidia jezi kwa vijana katika kata 12 kati ya 23 za Wilaya ya Kilombero
  15. Nimefanikisha ligi mbili katika kata mbili –Ligiza, mpira wa miguu na netiboli
  16. Nimeshiriki kwenye fundraising katika misikiti mitatu na makanisa manne.
  17. Nimekuwa sehemu ya kufanikisha uzinduzi wa Chuo Kikuu Kishirki Cha Mt. Fransisco.
  18. Nimeshiriki kuwasaidia wahanga (neno sahihi waathirika) wa mafuriko wilayani Kilombero.
  19. Nimefanikisha wanafunzi wa shule ya msingi kushiriki Umitashumta ngazi ya wilaya, mkoa na taifa.
  20. Nimefanikisha vikundi viwili vya kina mama wajane kuweza kujiajiri na kuendesha maisha yao wenyewe.
  21. Nimefanikisha vikundi vitano vya kina mama kuweza kujiajiri.
  22. Nimefanikisha vikundi vitatu vya wenye ulemavu kujiajiri wenyewe.
  23. Nimefanya mikutano ya hadhara ya elimu ya uraia pamoja na shukrani, zaidi ya 20. Na mengine madogo madogo mengi.

B. KAZI ZA CHAMA WILAYANI KILOMBERO
Katika kukuza chama wilayani Kilombero nimefanikiwa kufanya yafuatayo;

  1. Nimelipia na kufungua ofisi za CHADEMA katika kata tano.
  2. Nimefungua na kuzindua matawi 13 yaliyojengwa, na yenye uongozi wa kudumu.
  3. Nimeingiza wanachama zaidi ya 8,000.

C. KAZI ZA CHAMA ZA KITAIFA

  1. Nimeshiriki maandamano ya CHADEMA kanda ya ziwa katika mikoa yote ya kanda hiyo katika kupigania haki za Watanzania.
  2. Nimeshiriki maandamano ya CHADEMA Nyanda za Juu Kusini kasoro (mikoa ya Iringa na Ruvuma) katika kupigania haki za Watanzania.
  3. Nimeshiriki kwenye kazi za siasa Arusha - sakata la kuvuliwa uanachama madiwani, kusaka muafaka.
  4. Nimeshiriki kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga.
  5. Nimeshiriki kutoa mafunzo ya upungufu wa sheria ya mabadiliko ya Katiba 2011 katika Mkoa wa Ruvuma.
  6. Nimeshiriki kwenye siasa za vyuo vikuu, makongamano, mikutano ya hadhara na uzinduzi wa matawi
  7. Nimeshiriki kwenye siasa za Dodoma, Singida na Morogoro.
Natambua nilipaswa kuyafanya zaidi ya haya lakini kutokana na sababu mbalimbali hayo ndio niliyofanikiwa kuyafanya.
Angalau nimefanikiwa kufanya karibu asilimia 70 ya niliyopanga kuyafanya kwa mwaka huu 2011 kama mbunge wa vitimaalumu wilayani Kilombero.
Naomba nichukue fursa hii pia kuwashukuru wana-JF wote kwa support yenu kwangu kwa hakika ninawashukuru sana.
JF imekuwa ni nyumbani, JF imekuwa nidarasa, vile vile JF imekuwa ni Tanuru la Moto maana wakati mwingine huwa ninaingizwa kwenye moto hasa.
Na mwisho nichukue fursa hii kuwaomba radhi wale wote niliowakwaza kwa namna moja ama nyingine, tuanze upya mwaka ujao.
With Love
Regia
 
Regia Mtema katuachia mfano wa kuwajibika kwa wapiga kura

Lula wa Ndali Mwananzela

Toleo la 222
18 Jan 2012

KIFO cha Mbunge wa Viti Maalumu, Regia Mtema (CHADEMA) kilichotokea Jumamosi iliyopita kimeacha pengo kubwa katika maisha na fikra za watu wengi ambao walikuwa wanamfuatilia na kumfahamu.
Kwa hakika kimeacha pigo kubwa kwa familia yake na kuacha ombwe lisiloweza kuzibwa.
Wakati wazazi wake, ndugu, jamaa na marafiki wanamsindikiza katika makao yake ya milele itoshe kwetu kuyaweka maneno yake kama kumbukumbu katika mioyo yetu.
Mwishoni mwa mwaka jana Regia aliandika kwa kirefu mambo ambayo alishiriki katika kuyafanya kama mbunge katika mwaka wa 2011.
Baadhi ya watu waliona labda alikuwa anajionesha au anajipa ujiko (anajipendekeza) akijitengenezea njia ya kuelekea 2015. Wachache waliomuelewa walielewa kuwa alikuwa anawapa taarifa watu mbalimbali kuhusu mambo yale aliyokuwa ameyafanya mwaka uliopita.
Ilikuwa baada ya kusoma yale maelezo yake ndipo nilielewa kitu kimoja ambacho ni viongozi wachache sana wanacho.
Kujali watu ambao unawajibika kwao. Regia alijua kuwa anafuatiliwa kama kiongozi kijana na anafuatiliwa kama kiongozi ambaye anatokea Jimbo la Kilombero.
Regia alitambua jinsi ambavyo kile ambacho aliamini (na baadhi yetu kukubaliana naye) kuwa bila kutumika kwa mbinu kubwa angeweza kutangazwa mshindi wa ubunge kule Kilombero.
Moyoni alitambua na wananchi wengi wa Kilombero walitambua kuwa alikuwa ni chaguo lao. Hawakujali kuwa ni mwanamke, hawakujali kuwa alikuwa mlemavu na kwa hakika hawakujali kuwa anatokea chama cha upinzani.
Maelfu ya wananchi ambao leo wanamsindikiza kule Kilombero wanamtambua kuwa alikuwa ni "mbunge" wao kwa maana ya kuwa alikuwa ndiye mwakilishi wao.
Regia alikuwa anajua anawajibika kwa hawa watu.
Hili lazima litufikirishe kidogo. Kama mbunge ambaye hakuchaguliwa na mtu hata mmoja na akapitishwa kuwa mbunge wa "kuchaguliwa" anajiona kuwa ni halali, vipi kuhusu mbunge ambaye alichaguliwa kwa maelfu ya kura japo hakupewa ushindi?
Hivi kweli tunaweza kusema mbunge aliyebebwa bila kuchaguliwa na mtu hata mmoja ni halali "kuwawakilisha" wananchi kuliko mbunge ambaye alichaguliwa hata na watu kumi?
Regia alikuwa ni mwakilishi wa wananchi na hilo alilitambua na wale ambao walikuwa pamoja naye walitambua hivyo.
Hivyo, maneno yafuatayo ni ripoti ambayo wengi wetu hatujawahi kusikia kutoka kwa kiongozi hata mmoja kueleza mafanikio yake.
Wapo wengine wamejaribu na wachache wamewahi kuandika kwa kina na kusema "mimi nilishiriki kufanya hivi" au "mimi nilifanya hivi". Regia ametuonesha kuwa kujitangaza kwamba umefanikiwa kufanya jambo hili siyo kujipendekeza bali ni kutangaza kwa kujiamini kuwa ulifanikiwa kufanya unavyosema.
Tunaposema kauli hizi za Regia tumshukuru Mungu kwa maisha ya Regia kwa nafasi aliyotupa kufahamu mambo ambayo hata hatukuwa tunayafahamu.
Tunawashukuru wazazi wake kwa maisha na malezi waliyompa; tunamshukuru kwa namna ya pekee pacha wake Remija ambaye maisha yake yalikuwa yamefungana kutoka tumboni.
Na tunawashukuru wale wote ambao walimsaidia Regia kuwa Regia na kuwa kiongozi kati yetu. Nina uhakika inshallah sisi kama wananchi tunaweza kumuenzi.
Lakini hili tutalizungumza baadaye. Kwa wakati huu naomba niweke maneno yake mwenyewe karibu wiki mbili tu zilizopita akielezea mafanikio yake na jinsi maneno hayo yalivyotoka kwenye mtandao wa JamiiForums.com ambako Regia alikuwa ni miongoni mwa wanachama maarufu zaidi!

- See more at: Raia Mwema - Regia Mtema katuachia mfano wa kuwajibika kwa wapiga kura
 
Naamini umepumzika kwa amani Regia
 
Hakika kila nafsi itaionja mauti ,


R.I.P______REGIA MTEMA.
 
Rest In Peace dada yangu. Nimeshiriki misa yako leo. Mwanga wa milele ukuangaze
 
Endelea kukaa kwa amani na heri huko uliko peponi Regia
 
Back
Top Bottom