Katika kujenga nchi ki uchumi na kijamii na hasa nidhamu katika utumishi wa umma, tulipokuwa tumefika, hakukuwa na namna nyingine ya kufanya mbali na kutanguliza buldoza. Na ndivyo inavyokuwa katika kujenga miundombinu kama barabara n.k. Buldoza kwanza, halafu mitambo mingine kama grader vinafuata nyuma.
Hatua tulipofika sasa, japo bado kuna mchwa unatafuna mbao zetu, lakini huwezi kulinganisha kazi ya ki utawala iliyokuwepo kati ya mwaka 2015 na sasa 2021. Kuna nafuu sana katika kupima workload. Sasa hivi walau imeishazoeleka kuwa kusimamisha kazi mtu aliyevurunda si jambo la kushangaza. Huko nyuma ilikuwa kuhamishwa kitengo tu basi. Nakumbuka tuliamishwa kuwa kuna vigogo wakikamatwa nchi itatikisika, lakini sasa baada ya kumkamata Manji, Rugemalira, Seth na MO kuhifadhiwa sehemu kwa muda hakuna tena untouchables, wote tuko level moja.
Hivi unadhani hayo yangeweza kufanywa na mtambo mwingine mbali na Buldoza? Hebu jiulize, toka kumepambazuka leo amekutana na teja wangapi? Umesikia lini jambazi kavamia benki au jambazi kateka basi au kavamia baa?
Mengi tutayasema kwa mihemuko, lakini mzee baba, kazi kubwa kaifanya.
Labda ni nikubaliane na Jaji Ibrahim Juma kuwa, hatuna shaka na uwezo wa Rais wetu, mama Samia Suluhu, lakini pia tukubaliane kuwa atafanya makubwa kwa kusimama katika mabega ya watangulizi wake. Atapita ambapo tayari tingatinga limepita. Kwakweli marehemu Magufuli amesawazisha nchi kama Buldoza linavyopasua barabara na sasa ni kazi ya grader kuondoa mizizi, vishindo na vimawe vidogovidogo, excavator zichimbe mitaro mpaka barabara itakapokuwa kama mkeka.
Tusisahau kuwa wakati Buldoza liko kazini vitu vingi huumia, na vingine kufa kabisa, kama vile miti, vichuguu n.k. Kwa vyovyote vile mchwa na kumbikumbi wa kwenye vichuguu watalalamika. Lakini ndege na nyani waliokuwa na makaazi katika miti wataona kuwa hilo buldoza halina undege au unyani na utumbili kama vile ambavyo binadamu hulaumiwa kwa kusema hana ubinadamu.
Asiyeona haya aliyoyafanya marehemu Magufuli namuomba tafakari upya mambo ya EPA, RICHMOND, CAPACITY CHARGES, ESCROW, TICS, HUJUI MIMI NANI?, NITAKUWEKA NDANI, WATU WAMEDHULUMIWA VIWANJA, MACHINGA WAMEPIGWA, MGAMBO WANAMWAGA BIDHAA ZA WAVUJA JASHO, TOZO ZA MAZAO, MIRADI KUKAMULIKA BAADA YA MIAKA NENDA RUDI, WATOTO SHULENI KUKAA SAKAFUNI n.k. Hiyo yote ilikuwa kero! na aibu kwa nchi.
Acha Mungu aitwe Mungu.
Namaliza kwa kusema Rahaa ya milele umpe ee bwana, na Mwanga wa milele umuangazie. Apumzike kwa amani Bwana John Joseph Pombe Magufuli. Amina.