Bado Pweza Mtu asisitiza Hakuna Uchaguzi Hapo Jumapili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bado Pweza Mtu asisitiza Hakuna Uchaguzi Hapo Jumapili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mlachake, Oct 25, 2010.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Na Issa Mnally
  Hali ya Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Ali Omar Juma ikielezwa inarejea vizuri, kiwewe kinatawala kuhusu anayetajwa kufariki dunia kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, 2010.

  Ingawa wagombea wenyewe hawaoneshi kutetereka kwa namna yoyote kutokana na tishio la mmoja wao kufariki dunia, lakini uchunguzi unaonesha kuwa swali la ‘nani atakufa’ linasumbua ubongo.
  [​IMG]
  Dk. Slaa (CHADEMA)
  Tayari imekwisharipotiwa kwamba baadhi ya Watanzania walikata tamaa mapema, tangu waliposikia utabiri kuwa mwaka huu hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu kwa sababu mmoja wa Wagombea Urais mwenye nguvu atafariki.

  Mnajimu alwatan barani Afrika, Sheikh Yahya Hussein ndiye sababu ya sakata hilo kupitia utabiri wake na katika mazungumzo na gazeti hili Ijumaa iliyopita alisisitiza kwamba siku zimebaki chache lakini mgombea mmoja ataaga dunia.

  Sheikh Yahya aliliambia Ijumaa Wikienda ‘The Biggest IQ Paper’ kuwa ni lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ijiandae kuhairisha uchaguzi kwa sababu macho yake yameona na yana uthibitisho wa kifo cha mmoja wa wagombea.
  [​IMG]
  Hashim Rungwe (NCCR-MAGEUZI)
  Alisema, anachokifanya yeye ni kutabiri kwa kufasiri nyota lakini siyo uchawi kama ambavyo wengi wamekuwa wakiamini.

  “Huu ni utabiri siyo uchawi, siku bado zipo, kwahiyo tungoje siku kati ya hizi chache zilizobaki, yatatimia tu niliyoyasema,” alisema Sheikh Yahya.

  Katika hatua nyingine, wananchi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa utabiri wa Sheikh Yahya ni mtihani kwa taifa kwa sababu ngoja ngoja inatia kiwewe.

  “Sisi wananchi tunawaza sana, labda nisiwasemee watu nijiseme mimi mwenyewe, nina mawazo mengi kusema kweli,” alisema Faustine Kimadao wa Boko, Dar es Salaam katika mahojiano yaliyofanyika Kituo cha Daladala, Mwenge.

  Kimadao alisema: “Watu ambao tunaamini katika siasa, hii inatugusa sana, tunaweza kudharau ya Sheikh Yahya lakini tukumbuke kwamba mwaka 2005 alitabiri na ikatokea.
  [​IMG]
  Jakaya Kikwete (CCM)
  “Alisema Rais Mkapa (Benjamin) ataongezewa muda wa kutawala kwa sababu uchaguzi utaahirishwa na kweli ikatokea. Tuyatazame haya katika pande mbili, binafsi nina hofu.”

  Mtanzania mwingine, Bora Steven katika mahojiano hayo alisema kuwa mwanzoni alikuwa anapuuzia lakini siku zinavyokaribia anaanza kupata mchecheto kwa sababu kuna alama za huzuni.

  “Kwa vyovyote vile, mgombea yoyote wa Urais akifariki ni maumivu kwa taifa, kwa kuanzia kuangalia chama chake, wafuasi na gharama ambazo nchi itaingia baada ya uchaguzi kuhairishwa,” alisema Bora.

  Aliongeza: “Tunamuomba Mungu atuepushie kwa sababu Sheikh Yahya ametabiri tu lakini mwisho wa siku, Mungu ana nafasi kubwa ya kuamua kinyume chake.”
  [​IMG]
  Ibrahim Lipumba (CUF)
  Maoni zaidi
  Khatib Mitea, muuza mafuta, alisema: “Mimi kwa mtazamo wangu Sheikh Yahya katabiri lakini akumbuke kuwa yeye sio Mungu, sidhani kama itatokea kwa mtazamo.”

  Salum Nassor, dereva taksi alisema: “Sheikh ni haki yake kutabiri lakini atambue kuwa Dini ya Kiislamu inasema utabiri ni dhambi, mimi nawafuatilia sana hawa wagombea wa Urais mpaka sasa sidhani kama kuna mgombea atakufa.”

  Majaliwa Robert, muuza vocha Bamaga, Mwenge: “Mimi kwa upande wangu namwamini sana Sheikh Yahya, nawataka Watanzania wakae chonjo. Unakumbuka mwaka 2005 alitabiri uchaguzi utahairishwa na ukahairishwa kweli.”

  Khatibu Idd, alisema: “Siwezi kuamini kama mmoja wa Wagombea wa Urais atapoteza maisha, kwa mtazamo wangu yule mtabiri alikuwa anawatisha tu Watanzania wasijitokeze kuchukua fomu.”
  [​IMG]
  Mugahywa Muttamwega (TLP)
  Thomas Maganga: “Mimi sipendi sana kuamini mambo hayo ya utabiri, lakini yule Sheikh ni mtabiri wa Kimataifa nawataka Watanzania wenzagu tusubiri tuone kile kitakacho tokea.”

  Upande mwingine, baadhi ya wananchi wameeleza hofu yao kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Freemasons kuichagulia Tanzania Rais.

  “Tunasikia Freemasons wakimtaka mtu fulani ndiye ashinde Urais basi atashinda na yule wasiyemtaka hatapata kitu, kwahiyo tunaogopa hilo,” alisema Halima Jaffar wa Ubungo, Dar.

  Mkazi wa Kinondoni, Jadu Kitani alisema kuwa tishio kwamba nchi nyingi marais ni Freemasons ndiyo linafanya ahisi wanaweza wakasimika mtu wao Tanzania.
  [​IMG]
  Peter Kuga Mziray (APPT-MAENDELEO)
  “Mimi sijui kama kuna mgombea yoyote wa Urais ni Fraemason lakini najua wanataka kuitawala dunia, kwahiyo inawezekana kabisa wameandaa mtu wao. Mungu asaidie washindwe,” alisema Jadu.
   
 2. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee ndio maana hata washabiki wa Simba walitaka kumchapa siku aliposema Simba hawapati ubingwa 2009/2010, na nafikiri anahitaji kichapo toka kwa wafuasi wa rais atakaefariki, mi simmind kabisaaaa huyu.
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Nasikia ameunganisha nguvu na Mzee Kulola kumtetea JK
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Hivi hadi leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia kuna watu wanasikiliza utabiri wa nyota wa huyu mtu? Jamani tubadilike. Unajimu ushapitwa na wakati
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280
  Mzee Kulola ndiyo nani?? Au unamsema yule kulola taperi wa sadaka makanisani??
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Hivi ulijuaje? Ndiye huyo!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,830
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Huyu mwanga ashindwe katika jina LA YESU aliyehai jina lipitalo majina yote
   
 8. R

  Realist Member

  #8
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 11, 2006
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kulola ni mtumishi wa Mungu, kama ni tapeli au la Mungu atamhukumu mtumishi wake na sio sisi...
   
 9. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Huyu anahatarisha amani ya Nchi.
  Ninaomba kama ikitokea mgombea yeyote akapata madhara Investigation ya kwanza tuanze naye!!!
  Kama m2 anatia msimamo namna hii, Si lazima atafanya kila awezalo ndio tabiri yake itimie.
  Liktokea lolote awe ameshahama Tanzania. Lazima tumchome moto akiwa hai.
   
 10. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2010
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  huyo ndo shekhe yahya ambae pia alitabili simba ingefugwa katika mechi fulani-sikumbuki timu iliyocheza na simba. lakini simba ikashinda wapenzi wa simba wakaenda kwake kumfanyia fujo kwa kuwatabiria uongo wa kufungwa, ilibidi polisi waende kufanya kazi yao nyumbani kwa shekhe yahya ndo ikawa salama yake
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  ALITABIRI KUWA REGINAL MENGI ATAGOMBEA URAIS MWAKA HUU, mbona tunaelekea mwisho wa kampain hajatangaza nia?
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,255
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  itakula kwake
   
 13. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Mungu yupi, maana ipo miungu mingi.Kumbuka alisema kuwa JK ni chaguo la Mungu, hapo hapo JK huyo analindwa na jeshi la majini ya Sheikh Yahya.Hebu tuambie ni mungu gani mweye shirika na majini.
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  yahaya anachokifanya sasa ni kulazimisha jahazi kusail kwa kutegemea pepo za kusi badala ya tekinolojia iliyopo.
  Poleni sana watanzania mnaoogopeshwa ha hili jini mtu
   
 15. e

  emalau JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,177
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 180
  Inawezekana anaandaa mipango ya kumuua mmoja wa wagombea ili utabiri wake utimie, kwa hiyo investigation ya kwanza itaanzia kwake atueleze.

  WAO WANA PESA NA SHETANI, SISI TUNA MUNGU

  Go Dr. Slaa
   
 16. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  huyu jamaa si mchawi mchawi...kwani anashindwa kumroga akafa...kwa nini anajiamini???akifa mgombea yoyote akamatwe..ni mchawi huyu
   
 17. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Five days to go!!!
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  huyu mzee yahya sura yake inatisha sio mchezo! Kwa upande wa utabiri mtaona atageuza kibao kuwa kilikuwa ni "kifo cha kiroho!"
   
 19. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,549
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Kwa maana ya Mzee Kulola kujiunga kwenye chama la majini? HILI NALO NENO
   
 20. P

  Pagi Ong'wakabu Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chonde chonde WanaJF taarifa hizi zisije tumiwa as propaganda na ssem maana hawana aibu na wanahitaji kushinda kwa gharama yeyote ikiwa ni pamoja na kupotosha jamii hasa maeneo ya vijijini kueneza uvumi kuwa mgombea wa chama fulani KAFA ili wapiga kura wakate tamaa. Mtakumbuka mtindo unaofanana na huu ulitumiwa hivi karibuni na makada wa chama fulani huko Arusha walitoa taarifa za uongo, mgombea wa chama fulani amejitoa na kujiunga na chama fulani HATUDANGANYIKI 31/10/2010 Dr W. P. SLAA MAGOGONIIIII PIPOOOZ POOOOOWER
   
Loading...