Bado nafasi mbili wazi Katibu Mkuu CCM na Waziri wa Fedha, hivyo January, Dkt. Nchimbi na Dkt. Mwigulu vuteni subra

Kwanini mbili? Na anapaswa kuvunja baraza lote, aunde lake akihirikiana na pm atakaye mchagua.
 
Ilani ya chama na katiba ya nchi vinahusianaje? Au unajitoa ufahamu tu.
Ila ni aibu kwa chama kinachojitapa ni kikubwa kuliko vyote kukosa watu wenye weledi hadi kianze kuokoteza kutoka nje.
Kikwazo kipo - unatakiwa uikane ilani yako na utekeleze ya wenzako!! Kuikana ilani ni sawa na kukikana chama chako!! Usaliti ni dhambi kubwa!!
 

Kama ambavyo kuna Wapuuzi waliwajaza Upepo ( Waliwajambisha ) hawa Watajwa wako ya Kuula katika Teuzi za Mama ( Rais ) hasa nafasi hii ya Umakamu wa Rais na Wakawaamini ( japo haijawa na imekula Kwako kwa Kuikosa ) ndiyo hivyo hivyo ambavyo katika hizo nafasi tajwa zilizopo wazi.

Hakuna ambaye atachaguliwa na wasipeteze hata muda Wao kuzunguka kwa Waganga Kutwa kwani Mfumo ulishawatupa hivyo wabakie kama Wabunge au Mawaziri inatosha tu.
 
Ukisoma post nyingi na mawazo mengi utagundua kwamba kiko kikundi maalumu ambacho ndicho pekee kinastahili uteuzi na kupewa nafasi zote za juu,na watanzania wengine hawastahili.

Kila wakat utasikia January Makamba, Mwigulu, Nape, Nchimbi nk.

Yaani kuna watu spesho wameumbwa kwa ajili ya vyeo vya juu.
 
Kama anko hayati,magu alivyoondoa dhana ya kupewa nafasi ya juu Kwa kufata kujulikana ,Kama makamba na kundi lake,nape na wengine basi hivyo watanzania wenye sifa za kuongoza hizo nafasi ni wengi zaidi ya hao hivyo hatuki jina kongwe tunataka mchapakazi hodari,sio wa kujisifu kutwa kuchwa mitandaoni Kama January makamba
 
Na hii mentality lazima iondoke. Tanzania ni ya wote na siyo utawala wa kurithishana miongoni mwa familia teule. Eti 3-5 generations wote muwe na nafasi za juu....
 
Katiba ingeruhusu,ndio hoja aliyoileta...wewe unazungumza Nini?aisee "mshike Sana elimu usimuache aende zake"
 
Umenena vema,chagua mwigulu mawe YAMEKOMA...
 
January na Nchimbi msikate tamaa bado nafasi moja japo " mwenyewe " anaweza kurudi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…