Bado kuna malaika dunia hii

Bado kuna malaika dunia hii

Brother hawa ndugu zetu ni watu wa kujaribu. Ndo akimuona Alicia Keys amevaa jeans lillilochanika kwenye tako na yeye atapiga hivo hivo.

Hivyo, na yeye alitaka kujaribu namna ya kuishi na Virusi vya Ukimwi. Sema msela hakutaka kumpa hiyo experience!
Wanawake mna tatizo gani nyinyi?
Yaani unajua jamaa ameathirika lakini bado unamlazimisha akutafune seriously,?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamjambo?
Ninayoyaandika hapa ni ya kweli na wala maunihukumu jamani, jifunzeni tu maisha yaendelee.
Nakumbuka wakati nipo chuo, miaka kama mitatu iliyopita, niliipenda sana jf. Katika purukushani za kuingia na kutoka, nilikutana na mada moja iliyomuhusu kijana mwenye virusi vya UKIMWI ambaye alikuwa anatafuta mwenza.
Kwa jinsi alivyoelezea, kwa kweli nilimuonea huruma. Nikamtafuta na kumuahidi kumuunganisha na dada mmoja mwenye tatizo kama lake.
Kweli nilimuunganisha lakini mpaka leo sikuelewa waliishia wapi.
Yule kaka akaanza kunizoea. Taratibu nikaanza kufall kwake.
Tulikaa katika mahusiano ya kutoonana kwa karibia mwaka wote tukiwa mikoa tofauti. The man was bright aiseee. Alikuwa mtu anayejua kuijenga hoja yake na kuitetea iwe kwenye siasa, uchumi au utamaduni.
Ukiuliza hoja za ugonjwa wapi amepata na vitu vingi juu ya hilo suala, alikuwa anajibu pasi na kujisikia vibaya.
Kama masihara siku akaniomba tuonane kama ni yeye kuja au mimi niende. Kwa kweli nilienda mimi mkoani.
Nakumbuka alinipokea vizuri sana nyumbani kwake na tulilala kitanda kimoja.
Jamaa alikuwa amenikumbatia usiku mzima akinibembeleza kama mtoto. Kila nilipojaribu "kujiongeza" alinikataza. Hata kiss tu aligoma kunipa.
Siku ya pili alinikatia tiketi nirudi masomoni. Hali ile ilinifanya nifikirie zaidi na nilizidi kumpenda kwa moyo wangu wote.
Niliporudi chuo, tukapotezana na jamaa baada ya muda fulani kupita. Kumbe tayari alianza kuumwa.
Nilikitahidi kumtafuta bila mafanikio. Nilimwandikia jumbe mbalimbali lakini hazikujibiwa si jf, facebook wala kwa simu.
Siku sina hili wala lile, napita jf naona jamaa aliniacha peke yangu, akafariki. Mtu pekee ambaye alikuwa na nafasi nzuri ya kunitumia apendavyo, lakini akanihurumia na kuendelea kunichunga kwa kunifariji kwa maneno na kumbatio lake.
I missed you so much dear, Rest in peace.

Sent using Jamii Forums mobile app
asee...interesting
 
Dada umetisha, KWELI hukipendi hata kidogo. Unatakiwa ujipende kwanza wewe mwenyewe. Unajichoma Moto ilikumfurahisha jirani. Hatuishi hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si bora mgonjwa mwenye mapenzi ya dhati kuliko mzima kiruka njia, maishe yenyewe yako wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787], Eti Bora mgonjwa mwenye Mapenzi ya dhati? Inamaana hamna wazima wenye Mapenzi ya dhati? Mapenzi ya dhati Ni kunywa ARV pamoja au. Kumbe na wewe huwa una pumpa sometimes.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787], Eti Bora mgonjwa mwenye Mapenzi ya dhati? Inamaana hamna wazima wenye Mapenzi ya dhati? Mapenzi ya dhati Ni kunywa ARV pamoja au. Kumbe na wewe huwa una pumpa sometimes.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wapo wenye mapenzi, lakini hata huyo mgonjwa anastahili kupendwa. Miaka yenyewe ya kuishi duniani iko mingapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Wapo wenye mapenzi, lakini hata huyo mgonjwa anastahili kupendwa. Miaka yenyewe ya kuishi duniani iko mingapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Anastahili kupendwa lakini sio it kujitoa muhanga...Kuna watu wafamilia mmoja Hana mwingine anao...wanakunywa Dawa kikamilifu..
Sasa huyu alikua nataka wafanye Mapenzi bila hata kujifikiria yeye kwanza...Sasa huo Nini Kama sio ujinga wakiwango Cha Corona virus

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anastahili kupendwa lakini sio it kujitoa muhanga...Kuna watu wafamilia mmoja Hana mwingine anao...wanakunywa Dawa kikamilifu..
Sasa huyu alikua nataka wafanye Mapenzi bila hata kujifikiria yeye kwanza...Sasa huo Nini Kama sio ujinga wakiwango Cha Corona virus

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwisho wa siku kila mtu ana uhuru wa kuamua afanye nini na maisha yake. Haina haja ya kumkashfu wakati maisha ni yake yeye binafsi, k yake hashei na mtu mwache aitumie atakavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku nyingine usirudie kufanya upumbav kama uloufanya.in the name of mapenz.
Stupid imbecile.
 
Mbona malaika tupo sema tunatofautiana vyeo kuna wengine sie ni malaika wa shetani!! Nakuhakikishia usingetoka na uzima wako hiyo ni dhambi kwa shetani kumuacha mwanamke kitandani..

Halafu na wewe uache uongo hizi movie zilishaishaga toka miaka ya 19 huko.
 
Back
Top Bottom