Bado kuna malaika dunia hii

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Hamjambo?

Ninayoyaandika hapa ni ya kweli na wala maunihukumu jamani, jifunzeni tu maisha yaendelee.

Nakumbuka wakati nipo chuo, miaka kama mitatu iliyopita, niliipenda sana jf. Katika purukushani za kuingia na kutoka, nilikutana na mada moja iliyomuhusu kijana mwenye virusi vya UKIMWI ambaye alikuwa anatafuta mwenza.

Kwa jinsi alivyoelezea, kwa kweli nilimuonea huruma. Nikamtafuta na kumuahidi kumuunganisha na dada mmoja mwenye tatizo kama lake.

Kweli nilimuunganisha lakini mpaka leo sikuelewa waliishia wapi. Yule kaka akaanza kunizoea. Taratibu nikaanza kufall kwake.

Tulikaa katika mahusiano ya kutoonana kwa karibia mwaka wote tukiwa mikoa tofauti. The man was bright aiseee. Alikuwa mtu anayejua kuijenga hoja yake na kuitetea iwe kwenye siasa, uchumi au utamaduni.

Ukiuliza hoja za ugonjwa wapi amepata na vitu vingi juu ya hilo suala, alikuwa anajibu pasi na kujisikia vibaya.
Kama masihara siku akaniomba tuonane kama ni yeye kuja au mimi niende. Kwa kweli nilienda mimi mkoani.
Nakumbuka alinipokea vizuri sana nyumbani kwake na tulilala kitanda kimoja.

Jamaa alikuwa amenikumbatia usiku mzima akinibembeleza kama mtoto. Kila nilipojaribu "kujiongeza" alinikataza. Hata kiss tu aligoma kunipa.

Siku ya pili alinikatia tiketi nirudi masomoni. Hali ile ilinifanya nifikirie zaidi na nilizidi kumpenda kwa moyo wangu wote.
Niliporudi chuo, tukapotezana na jamaa baada ya muda fulani kupita. Kumbe tayari alianza kuumwa.

Nilikitahidi kumtafuta bila mafanikio. Nilimwandikia jumbe mbalimbali lakini hazikujibiwa si jf, facebook wala kwa simu.
Siku sina hili wala lile, napita jf naona jamaa aliniacha peke yangu, akafariki. Mtu pekee ambaye alikuwa na nafasi nzuri ya kunitumia apendavyo, lakini akanihurumia na kuendelea kunichunga kwa kunifariji kwa maneno na kumbatio lake.

I missed you so much dear, Rest in peace.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hamjambo?
Ninayoyaandika hapa ni ya kweli na wala maunihukumu jamani, jifunzeni tu maisha yaendelee.
Nakumbuka wakati nipo chuo, miaka kama mitatu iliyopita, niliipenda sana jf. Katika purukushani za kuingia na kutoka, nilikutana na mada moja iliyomuhusu kijana mwenye virusi vya UKIMWI ambaye alikuwa anatafuta mwenza.
Kwa jinsi alivyoelezea, kwa kweli nilimuonea huruma. Nikamtafuta na kumuahidi kumuunganisha na dada mmoja mwenye tatizo kama lake.
Kweli nilimuunganisha lakini mpaka leo sikuelewa waliishia wapi.
Yule kaka akaanza kunizoea. Taratibu nikaanza kufall kwake.
Tulikaa katika mahusiano ya kutoonana kwa karibia mwaka wote tukiwa mikoa tofauti. The man was bright aiseee. Alikuwa mtu anayejua kuijenga hoja yake na kuitetea iwe kwenye siasa, uchumi au utamaduni.
Ukiuliza hoja za ugonjwa wapi amepata na vitu vingi juu ya hilo suala, alikuwa anajibu pasi na kujisikia vibaya.
Kama masihara siku akaniomba tuonane kama ni yeye kuja au mimi niende. Kwa kweli nilienda mimi mkoani.
Nakumbuka alinipokea vizuri sana nyumbani kwake na tulilala kitanda kimoja.
Jamaa alikuwa amenikumbatia usiku mzima akinibembeleza kama mtoto. Kila nilipojaribu "kujiongeza" alinikataza. Hata kiss tu aligoma kunipa.
Siku ya pili alinikatia tiketi nirudi masomoni. Hali ile ilinifanya nifikirie zaidi na nilizidi kumpenda kwa moyo wangu wote.
Niliporudi chuo, tukapotezana na jamaa baada ya muda fulani kupita. Kumbe tayari alianza kuumwa.
Nilikitahidi kumtafuta bila mafanikio. Nilimwandikia jumbe mbalimbali lakini hazikujibiwa si jf, facebook wala kwa simu.
Siku sina hili wala lile, napita jf naona jamaa aliniacha peke yangu, akafariki. Mtu pekee ambaye alikuwa na nafasi nzuri ya kunitumia apendavyo, lakini akanihurumia na kuendelea kunichunga kwa kunifariji kwa maneno na kumbatio lake.
I missed you so much dear, Rest in peace.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa miaka ya sasa ,karne ya sasa naimani atakuwa amefariki kwa ugonjwa mwingine na si HIV

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulimuacha boyfriend wako wa nyumban baada ya kupata wa chuo ukamuacha wa chuo baada ya kumpata wa JF ukataka kuchukua ngoma af ukampe wa chuo na ukirud nyumban ukamzawadie wa nyumban na baada ya hapo ungekuwa mwepesi sana maana tayar ungejua unao hakika ungeua wengi sana we kadada badili tabia kuwa na huruma...
Apumzike kwa amani shujaa wetu alijua kukupa wewe ngoma ni kutupa sisi wanaume wenzake alituthamini sana
Mungu ampumzishe kwa amani...
 
Back
Top Bottom