Badili mtazamo wako kuwa hivi ili usipate shida kuhusu wanawake

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Tangu unaanza kumtongoza jiwekee akilini kuwa wewe ndo kiongozi. Inamaana utaongoza mazungumzo, mahusiano na ngono kiujumla. Hata kama upo kwenye mahusiano ya miaka 40, endelea hivyo. Hilo ni jukumu lako, hivyo kuanzia sasa badili mtazamo juu ya kuwa na mwanamke. Badili kutoka,

Nawezaje kumpata - Ngoja nione kama anafurahisha. Nawezaje kumpata - Ngoja nimpe nafasi nione kama ananifaa. Nawezaje kumshawishi - Ebu nione kama tabia zake tutaendana. Yeye ndo kila kitu kwangu - Acha aendelee kuitetea nafasi yake nliyompa. Sjui ntafanya nini nkiwa naye - Nauvaa uongozi na nitaendelea kumuongoza nitakavyo na nitajifunza zaidi. Inabidi nijitahidi kumfurahisha - Ninampa furaha kadri niwezavyo. Ngoja nifanye hivi na hivi ili anipende - Ngoja niwe mwanaume anayevutia mwanamke kirahisi.

Jiwekee kwamba yeye ndiye ajithibitishe kwako. Jiwekee kwamba yeye ndo afate misimamo yako.
Jiwekee hautaendeshwa na mwanamke yoyote. Mitazamo hiyo na zaidi itakusaidia kuwa sawa baada ya kuachwa, au ukikataliwa.

Lakini haimaanishi uache kuchukua hatua. Ila muongoze unakotaka ili iwe rahisi kwake kujithibitisha kwako.
Ili iwe rahisi kwake kujiachia kwako. Hapo mahusiano yanakua kirahisi.

Duniani hapa mtazamo ndo kila kitu. Ukiwa na mtazamo wa huwezi kuishi na mwanamke unayemtaka hautaweza. Lakini ukiwa na mtazamo wa unaweza, utaweza tu. Utakua na mtazamo unaomvutia mwanamke kirahisi na unaomfanya akugande vile utakavyo.

Kutokana na maombi ya wengi nimeandaa program ya akili yenye mvuto, utajifunza jinsi ya kuishi na huo mtazamo mpya na jinsi ya kuutumia ili umuongoze mwanamke kirahisi maishani.

Mtazamo wako ndio unakusukuma ufanye vitendo fulani. Ukibadili mtazamo na vitendo vyako vitabadilika.
Kutoka kwenye kumnyenyekea mwanamke, kumruhusu akuendeshe, utakua wewe ndo unanyenyekewa.

Lakini angalia usitumie mitazamo hiyo kumnyanyasa mwanamke.

Nikutakie Siku Njema Yenye Baraka.
 
Pole kwa unayoyapitia mkuu, naamini umejifunza mengi sana tangu kipindi kile
 
Back
Top Bottom