Badili, Jiondoe au kubali matokeo… | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Badili, Jiondoe au kubali matokeo…

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by JamiiForums, May 17, 2012.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  May 17, 2012
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 4,899
  Likes Received: 1,647
  Trophy Points: 280
  Original poster - Mtambuzi | May 14, 2012

  BADILI: Unapojikuta kwenye hali usiyoipenda, unaweza kufanya jitihada za kuibadili au kubadili mtazamo wako kuhusu hali hiyo. Ikiwa uko katika uhusiano unaodhani haukusaidii kwa mfano, unaweza kwenda kwa washauri nasaha, unaweza kuzungumza na mwenzi wako na kujaribu kuufanya uhusiano huo uwe bora zaidi ama waweza kubadili mtazamo wako wa namna uhusiano wenye faida unavyotakiwa kuwa.

  Mara nyingi huu ni uchaguzi mgumu sana kuufanya kwa sababu inaweza ikalazimu kumkabili mtu mwingine kutoka katika tabia isiyo na faida kwako. Kubadilika kunatuondoa kwenye nafasi yetu tuliyoizoea na ambayo tunaiona inatufariji na kunahitaji ujasiri mkubwa kufanya hivyo.

  Kuamua kuacha kumtegemea mpenzi kukupa furaha na kutafuta furaha kutoka vyanzo vyenye kuaminika zaidi siyo jambo rahisi, lakini ni muhimu.

  JIONDOE: Kama umeshindwa kubadili hali kwa sababu yoyote ile umeshindwa kumfanya mtu abadili tabia yake kwa mfano, ni bora kujiondoa, ondoka kabisa. Kujiondoa kunakufanya uondokane na hali isiyofurahisha na kunasafisha njia kwako kwa ajili ya kuchagua jambo jingine mbadala. Ni wazi,watu wengi hukimbilia kuchagua njia hii, hukimbilia kujiondoa kwa sababu huogopa sana kujaribu njia ya kwanza ya kubadili hali ama kubadilika wao wenyewe.

  Lakini ingawa kukimbilia hatua hii bila kujaribu ya kwanza si busara, kuna wakati ambapo kujiondoa ni hatua pekee ifaayo kuchukua. Hata hii nayo inahitaji ujasiri mkubwa kwa sababu, mara nyingi akili zetu hutuweka katika nafasi ya kutumia methali ya ‘Zimwi likujualo’ kama utetezi wa kuendelea kuvumilia madhila yasiyo muhimu tunayokumbana nayo.

  KUBALI: hatua ya mwisho unayoweza kuchukua kukubali. Ziko hali ambazo huwezi kuzibadili na kukwepa ukweli wa jambo hilo, ni sawa na wendawazimu. Hebu mfikirie mfungwa wa kisiasa kama ilivyokuwa kwa mzee Nelson Mandela wa Afrika Kusini na wenzake. Wakati alipokuwa akishikiliwa jela, asingeweza kuibadili hali ile, wala asingeweza kuamua kuondoka. Hakuna jingine aliloweza kufanya ila kukubali hali halisi na kufanya kila analoweza kuishi katika hali hiyo. Kuna wakati kukubali linakuwa ni chaguo la kwanza tunalopaswa kuelekeza macho yetu, wakati tukiwa tunafikiria njia bora ya kubadili hali au kujiondoa.

  Nina hakika kila mtu anapotazama mambo yanayozunguka maisha yake, atakutana na moja ambalo haridhishwi nalo kwa asilimia 100. Utafanya nini kushughulikia hilo, utajaribu kubadili hali au mtazamo wako wa hali? Uko tayari kujiondoa ikiwa una hakika huwezi kubadili hali au uko tayari kubadili mtazamo wako kuhusu jambo hilo ili uweze kuendelea nalo? Uko tayari kukubali kile ambacho huna uwezo wa kukibadili na wala huwezi kujiondoa?


  Nafasi ni yako kutumia busara zako kuchagua.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,524
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  ushauri mzuri!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,030
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Well said..
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,194
  Likes Received: 1,590
  Trophy Points: 280
  Neno hilo Mtambuzi. Hapo kwenye kukubali nadhani inajumuisha na 'ku-adjust'. Mahusiano yanahusisha compromise. Ofcoz kuna vitu ambavyo hupaswi kamwe kukubaliana navyo kama physical and emotional abuse. Lakini ku-adjust ili ku-cope na mwenza ni muhimu sana. And ofcoz it takes two to tangle.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ... Mtambuzi na King'asti mwanadamu si KINYONGA.... ;) hata kinyonga hawezi iga sauti na umbile.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,194
  Likes Received: 1,590
  Trophy Points: 280
  Siku hizi umeanza siasa za mmu moskwito, shauri yako!
  Kitu muhimu sio kubadilika kila wakati, bali ku-adjust. Ntakupa mfano hafifu, kama mwenza anavuta sigara, ukimsihi aache ikashindikana. Maybe mtakubaliana no smoking inside the house? Avutie huko kibarazani. Kukupunguzia kero. Lakini kama unaona hutaki kabisa basi chukua ndogondogo kwani umemzaa weye? Huwezi kumbadili mtu unless anataka kubadilika, na sio kwa ajili yako bali kwa ajili yake mwenyewe. So hakuna ujanja baba, shauri, adjust or take a hike...
  Lol, ngoja nijistue na caffeine kwanza!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. cartura

  cartura JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 3,053
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mfano mzuri, but mtu anayevuta fegi anataka moyo kweli ku-cope naye cos s/he is always reeking...
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mimi hapo nitajiondoa mazima. Sitaki sigara, thats it. Hata akivutia nje, bdo atanuka moshi wake mdomoni, na nguoni.

  Mie siangalii short term pekee, huko mbele ya safari kuna higher risks akaja kunisumbua na gonjwa la saratani ya koo au mapafu.
   
 9. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Aksante Mtambuzi kwa somo zuri. Ubarikiwe.

  Nikiiangalia hii kiundani naanza kujiuliza ukweli wa zile methali za Penzi ni maua popote huchanua, sijui oh love doesnt ask why n.k ................. hakuna kitu kama hicho si ndio? Nikiangalia mfano wa King'ast na Mbu juu ya kumpenda mvuta sigara, I thought kwa kuwa penzi ni maua popote huchanua wala haliulizi kwa nini, basi hata hili la kumpenda mvuta sigara na kisha kufanya adjustment kama anavyosema Da King'asti linawezekana ...no?
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ....lol, MwanajamiiOne....ewe soulmate wangu. Nitakufafanulia.

  Katika yale nitayoya justify mapenzini (ukweli "maumivu ya mapenzi" yaanzapo) ni yale yasiyo na hasara kwetu, mfano; yaliyo nje ya uweza wako, kama umejitahidi lakini hujui kabisa mapishi, usahaulifu, nk...

  Haya mapungufu ya "kujitakia" mfano Ulevi, Utoro, Udanganyifu, dharau, nk kwangu mie I cant justify them aisee.... Ni mapungufu makubwa ambayo sidanganyiki "tena" na ahadi ati mtu akishaoa/kuolewa ataacha.

  Mtambuzi, King'asti, sijui nimeeleweka?...u-kinyonga siuwezi mie,....mbu majaaliwa yake kuuma na kupuliza tu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Okay My Soulmate kwa hiyo point ya kasoro za kujitakia nimekuelewa ingawa ninajiuliza Mbu wangu weye umeniona mie MwanajamiiOne, ukampenda kabla ya kugundua kuwa anavuta sigara! Au kupenda kwako kuna subira mwenzangu? Kuwa unabonyeza kibatabi cha Pause kwamba hebu kwanza mbona Mj1 mwenyewe anavuta sigara?! Hapana simwezi?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,712
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  ....dahh...

  I bet am in a wrong class. MwanajamiiOne, kwangu mie, mapenzi hayamaanishi ninapenda asb, mchana uchumba, jioni ndoa.

  Mfano; 'emotionally' naweza vutiwa na busara zako hata mwaka hapa jf (hatujuani)...then tukakubaliana kuonana, na hapo huenda kukawa na physical attraction...

  Baada ya hapo mapenzi yanajengwa sehemu ya tatu thru mazoea... Na kujikubalisha. If that wont work, sio lazima tuwe sote bana.

  Relationship ni mjumuisho wa phase mbalimbali kufikia uchumba, au hata ndoa. Huko kote kuna 'start, stop, pause, na re-boot' bana...au? Experience yangu tofauti myb, out of ( ...) girlfriends, ambao kwa sababu mbalimbali tulishindwana and I ended up Marrying my (ex) wife.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #13
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,747
  Likes Received: 1,093
  Trophy Points: 280
  Mbu, binadamu siyo Kinyonga lakini anaweza kubadilika-badilika kama Kinyonga..........................LOL
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...