Badala ya kodi za simu mngefanya haya kwanza...

Haki na maendeleo

Senior Member
Jun 15, 2021
123
262
Habari wakuu, kiukweli Serikali hii imetuumiza mno, kwenye makato haya ya simu, mm nafikiri kabla ya kuwaza kumkata mwananchi wa wa butobori!!! Wangeanza kufanya haya

1: Kupunguza posho na mishahara ya wabunge, na kuondoa viti maalumu havina kazi, sambamba na kuondoa wabunge Covid 19​
2: Misafara ya hovyo ya viongozi isiyo na tija, raisi anatembea na kijiji eti ni msafara!! , sijui mkuu wa wilaya Naye ana msafara , misafara hiyo haina tija, unakuta kwenye gari yupo kiongozi mmoja tu anaendeshwa​
3: Sioni faida ya mwenge wa uhuru, zaidi tu ni kueneza uzinzi na maradhi​
4: Safari ambazo sio rasm tuachane nazo, tumeshuhudia juzi katibu wa CCM Daniel Chongolo anatembelea ndege yetu, hapohapo Kikwete naye ana ndege alienda kumzika Rais wa Zambia, Makamu wa Rais naye ana ya kwake alienda Ufarasa kwenye ziara, hapohapo, mama yetu Rais naye ana ya kwake ya kwenda nayo Dodoma, kimsingi haya ni matumizi mabaya ya kodi zetu.​

Serikali ya awamu ya sita mjitafakari upya, hapa tulipo wananchi tumewachoka vya kutosha CCM tumewachoka mno

Katiba katiba katiba katiba katiba katiba, tunataka katiba
 

Attachments

  • VID-20210401-WA0018.mp4
    5.1 MB
Back
Top Bottom