Best home tutor
Senior Member
- May 8, 2026
- 194
- 268
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, ameishambulia serikali na wabunge wa chama tawala kwa kuwakamua tozo na kodi za dharau wananchi wa kipato cha chini, huku viongozi wakitengewa mabilioni ya fedha kwa ajili ya anasa na safari za angani.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Jumamosi, Juni 20, 2026, mjini Songea mkoani Ruvuma, Heche amemshambulia vikali Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge, kufuatia ushauri wake bungeni kuwa madereva wa bodaboda, bajaji na machinga watozwa shilingi 1,000 kila siku kwa ajili ya ujenzi wa barabara.
Heche ameeleza kuwa sekta isiyo rasmi tayari inalipa kodi kubwa kupitia manunzi ya vipuri, matairi na kodi 17 zilizorundikwa kwenye lita moja ya petroli, lakini fedha hizo zinaishia kutafunwa kwenye misafara ya anasa ya mawaziri na viongozi wakuu.
Amewataka wananchi kuungana na CHADEMA kudai Katiba Mpya itakayoruhusu siasa safi, na kuweka viongozi madarakani watakaobadili uchumi wa nchi ndani ya miaka mitano na kuruhusu kila Mtanzania kuishi kwa raha na mustarehe
Kauli ya Heche imejiri kufuatia mchango wa hivi karibuni wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Patrick Mwalunenge (CCM), bungeni Dodoma wakati wa kujadili Bajeti Kuu ya Serikali ya 2026/2027. Mwalunenge alidai kuwa sekta isiyo rasmi inayojumuisha bodaboda, bajaji na machinga si maskini na ina uwezo mkubwa wa kiuchumi.
Alishauri serikali iweke mifumo rasmi ambapo kila mwanachama wa makundi haya atakuwa anachangia shilingi 1,000 kila siku, hatua itakayokusanya mabilioni ya fedha kwa ajili ya kugharamia miradi mikubwa ya miundombinu na ujenzi wa barabara nchini bila kutegemea halmashauri pekee.