Kuhusu kamusi mistakes nyingi sana zinatokea
Na ndio maana huwa zinakuwa updated kwa kutoa matoleo mapya kila mwaka au kila baada ya muda fulani.
wakati fulani neno 'ukwasi' lilikuwa linatumika sehemu ya kutumia 'ukata'
hadi wazee wa BAKITA walikemea na kupinga kamusi zilizo andika hivyo
now utaona kuna mabadiliko
Ngoja kwanza, kuna kamusi ambayo ilikuwa inafasili hilo neno kwa hiyo maana? Au kilichokuwa kinatokea ni watu tu kulitumia vibaya hilo neno katika mazungumzo yao?
Manake hilo la kutumia neno au maneno vibaya au visivyo hutokea sana na sababu yake kuu huwa ni ujinga tu.
Mimi nimeanza kusoma kamusi zamani sana na ninazo kamusi za zamani [hata ile ya TUKI ya mwanzo kabisa ninayo] na hilo neno wala lilikuwa halifasiliwi kihivyo hata hiyo zamani. Na hata kwenye kamusi za sasa wala halifasiliwi hivyo.
mfano wazee wa kiswahili walisema tena on the record kabisa kuwa
neno 'maboresho' ni makosa na sio kiswahili ingawa bado linatumika
na si ajabu likawepo kwenye kamusi
Unajua lugha ni 'dynamic'. Wakati mwingine misamiati huongezeka na wakati mwingine maana za misamiati iliyopo nazo huongezeka.
Sasa hao wazee inavyoelekea wao ndo wamekuwa 'stuck' na dynamism ya lugha imewashinda.
Kama wewe ni mpenzi sana wa lugha na ukuaji wake basi utakuwa unajua kuwa kila mwaka kamusi za Merriam-Webster na Oxford, kwa mfano, huwa zinaongeza misamiati mipya ya lugha ya Kiingereza kwenye kamusi[mfano Selfie, Staycation, Twerk n.k.] na pia huongeza maana za maneno kwenye misamiati ya zamani pale inapobidi.
wenyewe walisema hilo neno 'bora' liko hivyo hivyo
makosa mfano kusema 'taifa stars itafanyiwa maboresho'
inatakiwa uweke neno lingine kama 'marekebisho'
labda iwe 'taifa stars itafanyiwa marekebisho iwe bora zaidi....
Hahahaa ndo maana kuna watu huwa wanaona kuwa lugha ya Kiswahili haikui wala kupanuka kwa sababu ya fikra za hao waitwao "wazee wa Kiswahili".
Kiingereza kila siku kinaongeza misamiati mipya na hiyo huwa inakuwa influenced na mambo mengi tu yakiwemo teknolojia [selfie], hip-hop [twerk], na kadhalika.
Sasa kwa nini kwenye Kiswahili iwe kufuru kuongeza misamiati au maana za maneno yaliyopo?
Ni kitu au jambo gani ambalo ndo huamua kuwa sasa neno fulani ni neno rasmi katika lugha ya Kiswahili?
Lugha ni kitu ambacho hukua, hupanuka, na kubadilika.