Bachela kujipikia ni kupoteza muda na Pesa

Bachela kujipikia ni kupoteza muda na Pesa

Msosi wa buku?mkuu hapo Labda kande,anyway cooking is fun,unatoa dongo unavyotaka sio mama ntilie unapangiwa kula ugali laini au wali usio na Nazi.Tatizo langu nikipika lazima niungue,haijalishi Nina gloves au lah,ila at some point kabla sijala ntaunguza vidole,na pia kazi ya kuosha sufuria ya ugali,naweza loweka hata wiki.
 
Ilo jotroo la tumbua hata kusearch sasa utaweza?!! Humo nakusetia motroo wa kubake cake lazima uzimie babu wee 🤣🤣🤣🤣

Afu mzabzab mwenye uzi atatufukuza, Umesahau siku ile!!!!!!
Njoo basi chemba unioe tumbua hilo
 
Kuna vitu unafanya halafu siku ukakaa ukatafakari utaona ulichagua njia isiyo sahihi kabisa....

Unapokua unaishi mwenyewe, ukaamua kujipikia basi labda iwe kwa mtazamo huuu

1. Ni kitu unapenda kutoka moyoni,
2. Unapoishi hakuna mgahawa karibu
3. Uchafu wa migahawa inayokuzunguka
4. Huwezi kutunza pesa hivyo bora ununue chakula hata ukiishiwa unachakua n.k lakini sio sababu ya Saving.
5. Mgahawani hawapiki chakula kizuri.

Lakini kinyume na hapo kama unaamini una save chochote basi unajidanganya,

1. Kupoteza mda, hiki ndio kipengele kikubwa, kuanzia manunuzi/maandalizi, kupika kwenyewe, kuosha vyombo, kusafisha jikoni, kupanga na shughuli nyingne zote zinazofanyika jikoni...

2. Kero za takataka, hasa ndugu zangu wa mjini, umepika ushamaliza mambo yako tumbo limejaa, kipengele ukiangalia makololo ya mabaki ya vyakula, hapo ndio unafikiria pakuyapeleka, Nyumba nyingne hazina Waste disposal nzuri, ni timing ifike usiku ukatupe barabarani.

3. Kero ya kucheza na bajeti, mda wote wewe kuwaza, unga nusu shilling kadhaa,mafuta nusu bei ile, Sukari kilo sijui sh ngapi, kesho ukienda bei imebadirika unakua mkali..

4. Gharama, kujipikia ni gharama, usijidanganye kabisa eti kuna kitu una save, Leo hii unaweza ukaenda mgahawani ukala chakula cha Buku, niambie ni katika mazingira gani utajipikia chakula baadae ukijumlisha mboga, chakula, gas, viungo, Chumvi n.k utakua umetumia chini ya buku? Nipe hio bajeti hapa na kweli iwe applicable.

5. Hasara, katika upikaji sio mda wote unachopika unakila chote, kuna kubakia, kuharibika, kuharibu, kuunguza n.k zote hizo ni lost ambazo ukiziweka kwenye mahesabu unazidi kuongeza budget..

6. Ratiba, upo sehemu unafanya hili na lile, kichwani unawaza kwenda kugombana na masufuriaa, unalazimika kufunga hata ofisi sababu umekua mfungwa wa kujipikia

Faida za kula mgahawani..

1. Unaokoa mda, hili ndio kubwa, utatumia huu mda kufanya mambo mengine ya msingi
2. Unaokoa pesa
3. Unakua flexible na nini ule, Nyumbani mda mwingine unalazimika kula kitu ambacho kuhutaka sababu tuu ndio kimebaki hutaki kukiharibu au
4. Unakua huru na ratiba zako mda ukifika unaenda kula unaendelea na ratiba.
5. Usafi, mda mwingi ndani panakua pasafi, unapofanya usafi ni wakawaida, Kinyume na hapo unatembea njiani vidole vinanuka vitunguu..
6. Unaepuka kero za takataka na maji taka.

Katika hayo yote simaanishi ndio usijue kupika, simaanishi usiwe na chombo hata kimoja,

Jifunze kupika, mana hujui na mazingira gani utalazimima kupika..

Nunua vyombo vyote, siku kwa kujiachia ukaona leo na mimi nijipikie, hio pia iko poa

ILA SIO KUA MTUMWA WA MAPISHI..
Pia kwa kiasi kikubwa hapa nazungumzia wale tuliopanga,

Kwa watu wenye Familia au zaidi ya mmoja Hilo la kupika yaweza kua options nzuri, Pia katika hili Sijalenga wanawake.

Niko tayari kukosolewa na kurekebishwa kwa hoja itapendeza.

Najua ni maisha yako, Sijakupangia namna ya kusihi, ni mtazamo tuu.
hapo may be uzugumzie uvivu wa kuosha vyombo ndo huwa inakuwaga kipengele kwa baadhi ya 'wasela' baada ya kula.

Assume nimenunua mahitaji ya mwezi mzima natia kwenye friji...nikiwa na hamu,natoa kuku wa kienyeji,samaki,nyama,mboga za majani nk
Nikitaka kupika hapo sinunui chochote b'se kila kitu kipo ndani.Unakula msosi unaotaka,kwa kiwango unachotaka na kwa wakati unaotaka+usafi.

i.e msosi unatumia tembo(10k)kuendelea kwa msosi.ukiwa na kila kitu ndani unaokoa gharama!

msosi kidogo angalau samaki mkubwa na ugali buku 3..mpaka buku tano kulingana na eneo kwa kipato chetu cha chini.Japo kwa mama ntilie upo ugali wa buku jero(1500/2000) na mtoto wa samaki hauwi satisfied kwa watu walaji kama sisi.

ndo maana tunakula ugali angalau na kokoto 4000/5000.

sasa ukijipikia unaokoa gharama ila kitu uwe nacho sio uanze kununua kila unachotaka kupika mara kitungu,nyanya,hoho,karoti,mboga,unga,mchele lazima kupika hapa iwe gharama.

ukipika unaepuka uchafu wa mama ntilie wakupenga kamasi na kujifutia kwenye nguo,kuchokonoa pua huku anakamua tui la nazi,kuongeza maji ya kwenye ndoo ya kunawia kwenye maharage or mboga kutokana na uharaka nk.

kupika ni gharama kama kila unanua onspot ili upike.Ikiwa hivi option ni kula kwa mama ntilie 'Mungu atatulinda na magonjwa'.

Ukiwa unataka msosi healthly na usafi bora upike.
 
Sio uchafu mkuu tatzo muda.
Sio kweli,mfano sufuria ya ugali ukiiloweka nusu saa inatosha,bakuli Moja sahani Moja na mwiko na vikombw labda huwezi ukaosha lisaa!

Muda gani unausemea? tatizo ni kufikiri kupikia na kazi za usafi ghetto ni za mwanamke.wapo wanaume hata kufua ni shida achilia pasi,kutandika mpaka muda wa kuja kulala.

Ni uvivu tu.muda gani unahitaji ?
 
Sasa kumbe unaweza kuandika kuhusiana na mada uliandika upupu gani mda ule,
Rubish kabisa, unawaza ushirikina tuu kitoto kidogo.
Duuh utakua na matatizo ya afya ya akili.umetoa maelezo mareeeeeeefuu hoja kijiko cha chai "mwisho eti:huo ni mtazamo tu!!kumbe ni mtazamo?
 
Sio kweli,mfano sufuria ya ugali ukiiloweka nusu saa inatosha,bakuli Moja sahani Moja na mwiko na vikombw labda huwezi ukaosha lisaa!

Muda gani unausemea? tatizo ni kufikiri kupikia na kazi za usafi ghetto ni za mwanamke.wapo wanaume hata kufua ni shida achilia pasi,kutandika mpaka muda wa kuja kulala.

Ni uvivu tu.muda gani unahitaji ?
Ni uvivu na uchafu kweli.
 
Back
Top Bottom