Bachela kujipikia ni kupoteza muda na Pesa

Bachela kujipikia ni kupoteza muda na Pesa

Kila nipatapo nafasi ya kuwa nyumbani Huwa napenda kujipikia michemsho sana sana siku ya ijumaa au jumamosi, huwa na enjoy sana, ila nikiamka na hangover inabidi nikimbilie chimbo la mama jane nikatwange mtori au supu nzito sana.

NB: Sijawahi kuridhika na ugali wa bar haswaa pale ninapoagiza kitimoto, kama nina hamu ya kitimoto ni bora niifunge tu ili nikapike ugali wangu nyumbani hata iwe saa 8 usiku. Mbinde ni kwenye kuosha vyombo, sufuria inaweza kaa hata siku 3 bila kuoshwa
Bora tu usipike km sufuria inakaa siku 3😂
 
Jamaa mtoa post ujapiga hesabu vizuri. kaa chini tafakari.
Kwanza tambua hakuna chakula cha buku sasa hivi kwa mama ntilie.otherwise ulishwe uchafu na kujitafutia maradhi.

ASUBUH-utajibana utakula maandazi matano na chai.jumla yake ni 700.
MCHANA-Utajibana pia maaba sehemu nyingi ugali wa kawaida ni 1500-2000.
USIKU-wali wa kawaida sehemu nyingi siku hzi ni 2000-2500.
NOTE.chakula cha mama ntilie mara nyingi huwaga ni kidogo sana.hivo unaweza usisihibe kabisa.ukaishia kubaki na njaa na kutamani uongezee na tuandazi tutatu pembeni.
SO KWA SIKU UNAMUACHIA MAMA NTILIE ELFU 6. 6000TSH.

TUJE KWENYE KUPIKA KAWAIDA.
ASUBUHI chai utatumia mia 700.hapa.kama.una kiporo unaweza tumia kiporo ulichobakisha usiku.hvo 700 yako ikapona.
MCHANA.hapa inategemea kama utataka kupika wali au ugali.wali kilo elfu 2000.nusu kilo elfu 1000.
Naamin nusu kilo unawezs kula mara mbili.
NIMECHOKA KUANDIKA.......
 
Umenifurahisha kuchaka kuandika,
Ila kuandika nako ni kipaji aisee...

Hata mimi natamani nikuelekeze kitu hapa kwa hio bajeti yako ila kuandika ni mtihanii.
 
Uko Tanzania hii hii mkuu??

Nipo Mwanza hapa mkuu
ngoja nikupe bajeti ya sh 10,000 kwa mahitaji yangu
unga sado 1 sh 4,300
mkaa 1,000 (n.b huwa unanitosha maana jiko langu latumia mkaa kidogo sana ukipelea ntaongeza wa 500)
vitunguu sh 500
chumvi sh 200
nyanya na vikolokolo vngne sh 1,000
dagaa sh 1,000
mafuta ya kula nusu chupa sh 800
JUMLA SH 8,800
hiyo sh 1,200 imebaki kwa dharura na kubadili mboga
Hapo mimi nimemaliza chai sio muhimu kwangu nakunywa hata uji ikibidi
 
Katika umri wangu huu wa miaka 37 kitu pekee ninachojua kupika ni kuchemsha chai tu, mke wangu akisafiri ninakula migahawani mpaka atakaporudi. Sifurahii kutojua kupika lkn ndo nimeshakua hivyo, nikibanwa sana natafuta mpishi anakuja home kupika na kuondoka
 
Ukiwa pekeako kupika ni ngumu na ni hasara, labda sehemu hiyo hakuna mgahawa pamoja nakuwa umri wangu umeenda na familia ninayo bado na penda vya kula vya mtaani, mfano nikijitaji supu ya utumbo Kuna Pahala Huwa naenda na nainjoi Sana pia nikijitaji nyama choma au kuku wa kuchoma lazima niende huko. So Kwa mtu single kupika naona Kuna hasara zaidi ila kifamilia una save bajeti ya Chakula maji umeme au gas
 
Kuna vitu unafanya halafu siku ukakaa ukatafakari utaona ulichagua njia isiyo sahihi kabisa....

Unapokua unaishi mwenyewe, ukaamua kujipikia basi labda iwe kwa mtazamo huuu

1. Ni kitu unapenda kutoka moyoni,
2. Unapoishi hakuna mgahawa karibu
3. Uchafu wa migahawa inayokuzunguka
4. Huwezi kutunza pesa hivyo bora ununue chakula hata ukiishiwa unachakua n.k lakini sio sababu ya Saving.
5. Mgahawani hawapiki chakula kizuri.

Lakini kinyume na hapo kama unaamini una save chochote basi unajidanganya,

1. Kupoteza mda, hiki ndio kipengele kikubwa, kuanzia manunuzi/maandalizi, kupika kwenyewe, kuosha vyombo, kusafisha jikoni, kupanga na shughuli nyingne zote zinazofanyika jikoni...

2. Kero za takataka, hasa ndugu zangu wa mjini, umepika ushamaliza mambo yako tumbo limejaa, kipengele ukiangalia makololo ya mabaki ya vyakula, hapo ndio unafikiria pakuyapeleka, Nyumba nyingne hazina Waste disposal nzuri, ni timing ifike usiku ukatupe barabarani.

3. Kero ya kucheza na bajeti, mda wote wewe kuwaza, unga nusu shilling kadhaa,mafuta nusu bei ile, Sukari kilo sijui sh ngapi, kesho ukienda bei imebadirika unakua mkali..

4. Gharama, kujipikia ni gharama, usijidanganye kabisa eti kuna kitu una save, Leo hii unaweza ukaenda mgahawani ukala chakula cha Buku, niambie ni katika mazingira gani utajipikia chakula baadae ukijumlisha mboga, chakula, gas, viungo, Chumvi n.k utakua umetumia chini ya buku? Nipe hio bajeti hapa na kweli iwe applicable.

5. Hasara, katika upikaji sio mda wote unachopika unakila chote, kuna kubakia, kuharibika, kuharibu, kuunguza n.k zote hizo ni lost ambazo ukiziweka kwenye mahesabu unazidi kuongeza budget..

6. Ratiba, upo sehemu unafanya hili na lile, kichwani unawaza kwenda kugombana na masufuriaa, unalazimika kufunga hata ofisi sababu umekua mfungwa wa kujipikia

Faida za kula mgahawani..

1. Unaokoa mda, hili ndio kubwa, utatumia huu mda kufanya mambo mengine ya msingi
2. Unaokoa pesa
3. Unakua flexible na nini ule, Nyumbani mda mwingine unalazimika kula kitu ambacho kuhutaka sababu tuu ndio kimebaki hutaki kukiharibu au
4. Unakua huru na ratiba zako mda ukifika unaenda kula unaendelea na ratiba.
5. Usafi, mda mwingi ndani panakua pasafi, unapofanya usafi ni wakawaida, Kinyume na hapo unatembea njiani vidole vinanuka vitunguu..
6. Unaepuka kero za takataka na maji taka.

Katika hayo yote simaanishi ndio usijue kupika, simaanishi usiwe na chombo hata kimoja,

Jifunze kupika, mana hujui na mazingira gani utalazimima kupika..

Nunua vyombo vyote, siku kwa kujiachia ukaona leo na mimi nijipikie, hio pia iko poa

ILA SIO KUA MTUMWA WA MAPISHI..
Pia kwa kiasi kikubwa hapa nazungumzia wale tuliopanga,

Kwa watu wenye Familia au zaidi ya mmoja Hilo la kupika yaweza kua options nzuri, Pia katika hili Sijalenga wanawake.

Niko tayari kukosolewa na kurekebishwa kwa hoja itapendeza.

Najua ni maisha yako, Sijakupangia namna ya kusihi, ni mtazamo tuu.
Kila mtu ashinde zake tutakutana fainali tutajua nani alisave na nani hakusave
 
Kuna mazishi special na taste special lazima upike mwenyewe Nyumbani.

Mama lishe hana muda wa kukuwekea masala wala babeq taste ili uenjoy marostrost Yale, ukitaka taste ya chakula cha kweli upike mwenyewe au uende restaurant za kueleweka.
 
Mtoa post anakuambia unakula chakula Cha buku!!unaahina unasepa huoshi suguria Wala kijiko!
 
Back
Top Bottom