Bachela kujipikia ni kupoteza muda na Pesa

Mnalishwa hamira kwa wingi hamjui tu! Mgahawani mnauziwa chakula kilichobaki jana!
 
Ningali kijana hata mimi niliamini hivyo 100%; migahawa mikubwa yote ya Sinza wakati huo walinijuwa sana hasa kwa vile nilikuwa na gari la kipekee sana enzi hizo, hivyo ukishafika na kupaki wanajua umefia. Lakini baadaye nilikuja gundua kuwa ulikuwa ni ujinga sana
 
Mimi naomba niwakumbushe wale wanaooamini Kupika baadhi ya vyakula/mboga zinazotumia mda mrefu mfano maharage eti kutumia mkaa unasave gharama tofauti na Gas,

Hahaa ndugu yangu kaa vizuri tafakari piga hesabu.
Gas ni cheap zaidi ya mkaa,
Kinachokutesa ni hofu ya technology na ule mlio ges ikiwa inanguruma mda mrefu tuu..

Halaf kwa mimi ninayetumia umeme wa 4 tariff, yaani elf 2 napata unit zaidi ya 16, mimi umeme kwangu ni cheap kupikia kuliko hio GasWapishi Wengi ni waoga wa Technology.
 
Kula mgahawani ni gharama kuliko kupika

Kaa chini upige tena hesabu zako
Mimi ninapoishi
Ugali/Wali + Mboga za majani, Dagaa/maharage = 1000

Ugali/Wali + Mboga za majani, Nyama(3) = 1500

Twende kazi hapa... ukijipikia.
Mboga za majani, Nyanya, Vitunguu, chumvi, karoti, hoho(hivyo vyote unavipata ndani ya buku) weka sasa hizo Dagaa na unga au mchele ni katika mazingira gani utavipata chini ya buku?

Ukiweza kujikongoja, njoo kwenye Gas, mafuta,

Suala la GHARAMA naungana na mtoa mada, hakuna mazingira unaweza kupika chakula cha kawaida tuu chini ya Buku. HAKUNA, Come again.
 
Ukweli mtupu. Chakula cha mtu mmoja ni ghali sana. Yaani mboga tu gharama yake unaongelea zàidi ya 4000 mpaka ikamilike kulika.

Wakati hiyo pesa nikienda mgahawani nakula safi kabisa na mtindi naagiza.😂
 
Icho chakula cha 1000/2000 kwa mwanaume hakitoshi labda km unafanya kazi ya kuuza duka
 
Nikijipikia mboga itabaki nitaila wakati Mwingine.

Nikijipikia nitakula kile kitu roho inapenda.

Nikijipikia Nina uhakika na chakula ninachokula

Nikijipikia napunguza gharama za matumizi
Point.
 
Bachelor's nyie ni sawa ila hata baadhi ya wanawake hawawez pika sababu wapo wenyew Kwa mm siwez aisee napika mwanzo mwisho japo nipo mwenyewe napika Milo yote pia naenjoy sababu Nakul kitu ninachotaka
Duh kumne hapa nitakuwa naulizwa unataka kula kwanza au kulaaaa kwanza🤣🤣🤣🤣

By the usiku wote huo wafanya nini jf wakati unatakiwa kuwa unapumzika na hubby bibie
 
Labda kama wachimba mtaro na kusukuma mkokoteni
Ni kweli, tukija katika picha hio, tutoe suala la gharama ila tusema tuu chakula cha mgahawani kwa ujumla tuu ni kichache, mana kuna sehemu unakula chakua cha elf nne bado unaweza usishibe.
 
Kwa mjini sawa.
Mfano unafanya kazi posta unaishi Bunju au Tegeta mda mwingi upo barabarani kuwahi usafir
 
Ndio mkuu mwanaume kula chakula cha 2000 hata afya yako haiwezi kuwa sawa
Ni kweli, tukija katika picha hio, tutoe suala la gharama ila tusema tuu chakula cha mgahawani kwa ujumla tuu ni kichache, mana kuna sehemu unakula chakua cha elf nne bado unaweza usishibe.
 
Ukiwa na friji na microwave wewe ni kupika vitu vya week mzima kama maharage nyama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…