sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,408
- 19,033
Kama kweli unampenda mtoto wako / unaemlea ni muhimu sana kumuandalia mazingira ya kuweza kujitegemea kikamilifu kwa majukumu ya kimsingi,
pindi mtoto afikapo miaka 13 awe anaweza kuji handle mwenyewe na shughuli za nyumbani kwa ujumla, kinyume na hapo basi ujijue wewe kama mzazi umefeli malezi ya kawaida kabisa.
Ma house girl na house boy waweza kuwaajiri lakini ni kosa kubwa sana kuwahamishia kazi za watoto wako, bill gates na utajiri wake watoto walifanya kazi za nyumbani.
Kuna wazazi ambao utotoni walifanyishwa kazi nyingi sana kiasi ziliwachosha sana na kuwafanya wazichukie kazi za nyumbani kwa ujumla, kundi hili limeathirika kisaikolojia na wakiwa watu wazima wakipata pesa za kuajiri house girl wanaona kila kazi kwa mtoto ni mateso, baadhi utawasikia "sitaki mtoto wangu apitie shida kama nilizopotia acha apumzike"
Hii sio sawa hata kidogo, kinachopaswa kuzingatiwa ni kumpa kazi mtoto kulingana na umri wake ila sio vinginevyo.
Tabia ya kurudia rudia hujenga mazoea, Mtoto inabidi azoee hizi kazi kwa faida yake na jamii kiujumla.
Kila baada ya mwaka au miaka miwili unamzoesha majukumu mapya huku akiendelea na ya zamani.
MIAKA 3
Majukumu binafsi
- Kuoga mwenyewe chini ya uangalizi
- kupiga mswaki kila akiamka na kabla ya kulala
- Kuweka nguo chafu kwenye tenga
- Akimaliza kula apeleke chombo sehemu ya kuoshea
- akimaliza kutumia kitu ajue pa kukirudisha na kukipanga (toys, midoli, vitabu, rimoti. n.k)
MIAKA 4 - 5
Majukumu Binafsi
- Kuchota maji yakuogea na kujiogesha bila kufunga mlango
- kufua nguo nyepesi za ndani, leso na soksi.
- kufuta meza baada ya kula.
- kuosha sahani yake aliyolia.
- kukunja nguo zake
- kubrush viatu vyake
Majukumu ya kifamilia
- kufuta vyombo vilivyooshwa kasoro vyenye ncha kali
MIAKA 6 - 7
Majukumu binafsi
- kuoga mwenyewe
- kutandika kitanda
- kujiamsha na kujiandaa kwenda shule
- kufua nguo zake kila siku
- Kujiandalia chai
- kufagia chumba chake na kupiga deki
Majukumu ya kifamilia
- Kufagia uwanja wa ndani ya nyumba
- kumwagilia maua / bustani ya nyumbani
- kuosha vyombo
- kukunja nguo za wazazi / walezi
MIAKA 8-9
Majukumu binafsi
- kupiga pasi nguo zake
- kujipikia chakula kwa uangalizi wa karibu
Majukumu ya nyumba
- Kufagia uwanja wa nje
- kupalilia bustani / kupanda mboga za bustan
MIAKA 10 - 11
Majukumu Binafsi
- kuweza kujipikia
- kama kazoea schoolbus/lift ajifunze kwenda mwenyewe
- Kusafisha choo
- kukata / kufyeka nyasi
Kwa umri huu tayari i inabidi awe anaweza kujifanyia majukumu binafsi mengi, umri huu ni kuweka efforts kwenye majukumu ya familia na mazingira ya byumbani.
- Kupika chakula cha familia
- kuosha gari / pikipiki
- msimu wa kulima mkalime wote
- kwenda kumwaga taka za nyumba kwenye dampo
- kusafisha banda la kuku, mbwa, ngombe, n.k.
- kuchinja kuku
- n.k
ANGALIZO
usizoee kumpa mtoto pesa kufanya kazi za nyumbani, inabidi aelewe kuwa mambo anayofanya ni kwajili ya usafi wake, mazingira yake, kujifunza namna ya kuishi kwenye jamii za watu, n.k. mlipe pale unapoona kafanya kazi iliyovuka anayotakiwa kuifanya na awe karidhia kuifanya.
Ni njia ipi nzuri ya kuwasimamia wafanye majikimu yao ? wahakikishe wanafanya kazi zao kabla ya kucheza games, kuangalia tv, kucheza na wenzao, n.k. kiburi kikizidi kuwapandishia sauti inaweza kusaidia, inapobidi tumia kiboko (usitumie ngumi, gogo, mtwangio, mateke, n.k.)