Baby Madaha: skendo ya Madawa ilivyomtesa

Rugaikamu

Member
Aug 8, 2017
37
20
maxresdefault.jpg


MWANADADA kutoka kiwanda cha filamu na muziki Bongo, Baby Madaha ameeleza kuwa katika maisha yake hakuna kitu kilichowahi kumtafuna na kumletea shida kwenye familia yake kama skendo ya kutumia unga.

Akichonga na Risasi Vibes, Baby alisema kuwa, skendo hiyo ilitokana na kushiriki kwenye filamu mbalimbali akiwa kama teja, jambo ambalo lilisababisha watu wazushe kwamba alikuwa akitumia unga.

“Kiukweli skendo ya unga ilinitesa sana kiasi kwamba familia yangu wakajua kweli ninatumia unga, unajua mama yangu na mdogo wangu ni madaktari, kwa hiyo suala hilo lilikuwa ni la aibu kiasi kwamba walinichukua na kunipeleka hospitalini kupima huko ndiko nikagundulika kwamba nilikuwa situmii unga, hiyo ndiyo ikawa nafuu yangu,” alisema Baby Madaha.
 
Aende zake Kwaio anawafanya wabongo hawajui tofauti ya maigizo na maisha halisi
 
Back
Top Bottom