Babu yangu kashindwa hudhuria kikao cha Ukoo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,206
4,698
Asili yetu ni Kijiji cha Nyamwaga, Tarime Mkoani Mara na ni desturi ya ukoo wetu kufanya vikao kujadili masuala yanayotuhusu

WanaUkoo hupewa taarifa mapema kwani wanaishi maeneo tofauti na baadhi ya maeneo kuna shida ya miundombinu ya usafiri

Hata hivyo kwenye kikao cha karibuni Babu yangu hakuhudhuria na nilipojaribu kudodosa niliambiwa hakupewa taarifa kwa wakati!

Nimeshangazwa na sijui kwanini Babu yangu ambaye ni MwanaUkoo Mwandamizi tena aliyewahi ongoza Vikao vingi vya Ukoo siku za nyuma eti ameshindwa hudhuria kikao kwa kukosa taarifa!

Babu yangu ni Mstaafu wa aliyerejea Kijijini akisimamia miradi yake ya kilimo na ufugaji aliyoianzisha kutokana na pesheni yake.

Pamoja na changamoto hiyo kikao kiliendeshwa vizuri na Mwenyekiti wa Ukoo Mzee Chacha na kufikia maazimio/ maamuzi kadhaa sambamba na kuhimiza upendo na mshikamano

Pamoja na kukosekana kwa Babu yangu nitaheshimu maamuzi au maazimio ya Kikao cha Ukoo

Siku moja nitamtafuta tukae chini anipe mrejesho wa kilichojiri!

Wasalaam
 
Family matters! Then unategemea tu comment kitu gani mkuu?

Anyway siyo kila jambo ni la kulileta JF
 
Tatizo babu yenu kastaafu hivyo wana ukoo mmepunguza heshima kwake,mnaona wa nini hana hela na pensheni ndogo

anyway kama ni lugha ya mafumbo bado babu anatakiwa aheshimiwe
 
Wapi Dodoma huko? Mzee Butiku hajahuzulia? Au Warioba? Nazani nimekuhelewa kiasi japo sijajua kati ya hao wawili ni yupi mumojawapo
 
Si nimeona mahali babu yenu kasafiri kaenda huko amerika kumzungumzia yule mjomba yenu aliyekuwa mweka hazina mkuu wa ukoo wenu kwani alisharudi?
 
Back
Top Bottom