Kufuatia babu wa loliondo kugundua dawa ya magonjwa sugu na ukimwi.. Makanisa mengi yamebaki njia panda na kutokujua la kufanya huku waumini wengi wakikiristo kukimbilia huko na makanisa kubaki tupu hasa kimapato. Kufuatia hilo makanisa kama kwa kakobe amediriki kuwa muwazi na kumponda mchungaji babu wa loliondo kuwa ni tiba za kishetani na kutoa aya zinazoonyesha uchafu wa dawa hizo. Hatua hiyo imeyafanya makanisa kugongana kwa kukosa muongozo juu ya dawa hizo na waumini wapo njia panda wasijue lipi ni lipi. Kwa upande wa waislam wameshatoa msimamo kuwa dawa hizo ni kinyume na taratibu na[haramu kutumia] waumini wameelewa.. Kwa maelezo hayo ni bora viongozi wa kikiristo kutoa msimamo mmoja kama BABU NI DECI nyingine au kibwetere wa tz. Ili waamini wasibaki njia panda wamuamini nani kakobe au babu ?