Babu wa loliondo ayachanganya makanisa.

Kivia

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
278
32
Kufuatia babu wa loliondo kugundua dawa ya magonjwa sugu na ukimwi.. Makanisa mengi yamebaki njia panda na kutokujua la kufanya huku waumini wengi wakikiristo kukimbilia huko na makanisa kubaki tupu hasa kimapato. Kufuatia hilo makanisa kama kwa kakobe amediriki kuwa muwazi na kumponda mchungaji babu wa loliondo kuwa ni tiba za kishetani na kutoa aya zinazoonyesha uchafu wa dawa hizo. Hatua hiyo imeyafanya makanisa kugongana kwa kukosa muongozo juu ya dawa hizo na waumini wapo njia panda wasijue lipi ni lipi. Kwa upande wa waislam wameshatoa msimamo kuwa dawa hizo ni kinyume na taratibu na[haramu kutumia] waumini wameelewa.. Kwa maelezo hayo ni bora viongozi wa kikiristo kutoa msimamo mmoja kama BABU NI DECI nyingine au kibwetere wa tz. Ili waamini wasibaki njia panda wamuamini nani kakobe au babu ?
 
Babu alisema eti katumwa na Mungu. Ivi kuna dini ambayo haijui mtu aliyetumwa na Mungu anaitwaje? kwa mabuda wanaweza wasijue ni kwamba Waliotumwa na Mungu huitwa "Manabii(wingi) Nabii(umoja), sasa tujiulize babu ni nabii? na kama siyo nini msimamo wa KANISA juu ya babu kusema yeye katumwa na Mungu?. Pia nini msimamo wa kanisa juu ya ndoto? na napenda kujua msimamo wa kanisa juu ya dawa ya Mungu kuwa na masherti.
 
kakobe sio mungu ,na kakobe ni mkristo ila hawawikilishi wa kristo wote kimtazamo, kuhusu waisram nazani wangeanza na shkeh yahaya anaye onyesha watu mlango wa kuzimu kabla hawajamfwata babu wa watu, pia hakuna aliye walazimisha waislam kwenda kwa babu ila magonjwa yao ndio yana wapeleka hivyo nibora wasiende ili wawapunguzie foleni wale wanao amini
 
huna point ya maana!!
 
Hili la Babu kutoa dawa au tiba lingeachwa kama suala la kitabibu au uganga. Wapo waganga wa kienyeji wengi katika jamii yetu na haijawahi kuwa tatizo la kiimani au kuhusishwa na dini.

Tukishindwa kuacha kushupalia hii tiba ya babu na kufanya kuwa ni uthibitisho wa dini basi kweli tutawachanganya waumini, wagonjwa na kila mtu katika jamii.

Hivi Babu amesema kuwa makanisa mengine si ya kweli?

Au madhehebu ambayo siyo ya imani ya Babu kuwa ni batili?

Au Babu amesema imani nyengine za dini ni imani za uongo?

Imeshaonekana kuwa Babu hachagui wala habagui nani? au mgonjwa yupi atumie dawa "yake" sasa sisi kama wanajamii kwa nini tunataka kulazimisha mtafaruku ambao haupo?

Anayeona anahitaji tiba kwa Babu aachwe akapate tiba na yule ambaye haihitaji aende kupata tiba kule ambako anahisi atapata tiba.

Serikali na vyombo kama red cross na/au red crescent wasaidie kuweka mazingira ambayo yatafanya kuwa ni mazingira salama kwa mkusanyiko unaofika huko.

Unapoondoa "hope" ya kupona au kupata tiba kwa mgonjwa yeyote ni sawa na kuwa umemhukumu adhabu ya kifo au unamuua mapema. "Hope" ya tiba ni nguvu inayowafanya wagonjwa to hang on to life. Si vyema kuijengea vizuizi au kufisha.
 
Babu alisema eti katumwa na Mungu. Ivi kuna dini ambayo haijui mtu aliyetumwa na Mungu anaitwaje? kwa mabuda wanaweza wasijue ni kwamba Waliotumwa na Mungu huitwa "Manabii(wingi) Nabii(umoja), sasa tujiulize babu ni nabii? na kama siyo nini msimamo wa KANISA juu ya babu kusema yeye katumwa na Mungu?. Pia nini msimamo wa kanisa juu ya ndoto? na napenda kujua msimamo wa kanisa juu ya dawa ya Mungu kuwa na masherti.

Mkuu.
Sijasikia kuwa Babu amesema yeye ni nabii...Alichosema ameoteshwa dawa hiyo na Mungu.

Wale wanaojitambulisha kama manabii huwa na kazi kuu ya kueneza dini na kusimamia dini na imani ya dini. Kwa mahojiano niliyoyasikia mpaka sasa sijaona sehemu ambayo Babu amesema kuwa yeye ni nabii.

Kutumwa na Mungu au kumtumikia Mungu ni wajibu wa kila binadamu. Kila binadamu ni "mtumwa " wa Mungu.
Kama unaamini katika uumbaji basi kila kilichoumbwa ni mali ya Muumbaji.

Kama unaamini katika evolution, it is a different story!
 
kakobe sio mungu ,na kakobe ni mkristo ila hawawikilishi wa kristo wote kimtazamo, kuhusu waisram nazani wangeanza na shkeh yahaya anaye onyesha watu mlango wa kuzimu kabla hawajamfwata babu wa watu, pia hakuna aliye walazimisha waislam kwenda kwa babu ila magonjwa yao ndio yana wapeleka hivyo nibora wasiende ili wawapunguzie foleni wale wanao amini
Yahaya Hussein wateja wake wengi ni Wakristo... Kwa sababu Waislam wanajuwa kabisa kuwa jamaa ni mushriki...!
 
woga wa mashehe na wahuni kama kakobe unafahamika. Babu peoposss pawa
 
Jamani waambieni hawa wanadini na viongozi wao wasiojisikia kwenda wasiende wasitake kutuchanganya tunaotaka kwenda kwa babu kuchukua tiba.hawalazimishwi wagonjwa kwenda kule we nenda hospitalini na kwenye makanisa yao huko. Tuachieni babu yetu
 
hizi taarifa umezitoa wapi? Umetunga ? Siamini hizi statistics zako

Siku zote uongo hujitenga na ukweli! Hii haina haja kuuliza maana ni uongo mweupe usiojificha! Ajaribu kuchunguza kabla ya kugive out!
 
Babu alisema eti katumwa na Mungu. Ivi kuna dini ambayo haijui mtu aliyetumwa na Mungu anaitwaje? kwa mabuda wanaweza wasijue ni kwamba Waliotumwa na Mungu huitwa "Manabii(wingi) Nabii(umoja), sasa tujiulize babu ni nabii? na kama siyo nini msimamo wa KANISA juu ya babu kusema yeye katumwa na Mungu?. Pia nini msimamo wa kanisa juu ya ndoto? na napenda kujua msimamo wa kanisa juu ya dawa ya Mungu kuwa na masherti.

Kaka eh? Hamani, jemedari wa jeshi la Ashuru aliponywa ukoma ila kwa sharti la KUJICHOVYA MARA SABA kwenye mto Yordani. Je, hayo sio masharti? Je, tiba ile haikutoka kwa Mungu?
 
kakobe sio mungu ,na kakobe ni mkristo ila hawawikilishi wa kristo wote kimtazamo, kuhusu waisram nazani wangeanza na shkeh yahaya anaye onyesha watu mlango wa kuzimu kabla hawajamfwata babu wa watu, pia hakuna aliye walazimisha waislam kwenda kwa babu ila magonjwa yao ndio yana wapeleka hivyo nibora wasiende ili wawapunguzie foleni wale wanao amini
Waislam tunafahamu kama Yahya Hussein is nothing but Mshirikina hilo neno Shekh lisikutishe jamaa msanii tu kama wasanii wengine na wafuasi wao ni mbumbumbu wasiojielewa na wasioelewa DINI pamoja na waliopoteza dira za maisha.
 
kakobe sio mungu ,na kakobe ni mkristo ila hawawikilishi wa kristo wote kimtazamo, kuhusu waisram nazani wangeanza na shkeh yahaya anaye onyesha watu mlango wa kuzimu kabla hawajamfwata babu wa watu, pia hakuna aliye walazimisha waislam kwenda kwa babu ila magonjwa yao ndio yana wapeleka hivyo nibora wasiende ili wawapunguzie foleni wale wanao amini

kaka umeniibia avatar......
 
me nashauri kwa ndugu zangu wakristo kwa kuwa kila muumini ana dhehebu nenda kwa kiongozi wako akufafanulia ucje ukaingia dhambini. Na kwa waislam ninachokijua tiba ya mitishamba imeruhusiwa kisichotakiwa ni kwena kwa mganga apige ramli, kukupa hirizi na mambo mengne ya ushrkna yamekatazwa aliewakataza kwenda kwa babu labda sababu yake kubwa iwe ni kwa kuwa anatoa mkristo ktk micng ya ukristo. Na huyo shehe yahaya anachofanya kwenye dini mbona kinajulikana ni dhambi? Acha niwape angalizo wanajf, usichukuliwe udhaifu wa m2 ndo mkasema ndo dini isemavyo hata km huyo m2 atakuwa kiongozi wa dini.
 
Yahaya Hussein wateja wake wengi ni Wakristo... Kwa sababu Waislam wanajuwa kabisa kuwa jamaa ni mushriki...!

Una uhakika na hili? mbona kwenye Kitimoto tunawaona akina "Juma" wengi tu ilhali wanafahamu wazi kuwa Kitimoto na haramu?
 
kakobe sio mungu ,na kakobe ni mkristo ila hawawikilishi wa kristo wote kimtazamo, kuhusu waisram nazani wangeanza na shkeh yahaya anaye onyesha watu mlango wa kuzimu kabla hawajamfwata babu wa watu, pia hakuna aliye walazimisha waislam kwenda kwa babu ila magonjwa yao ndio yana wapeleka hivyo nibora wasiende ili wawapunguzie foleni wale wanao amini
me nashauri kwa ndugu zangu wakristo kwa kuwa kila muumini ana dhehebu nenda kwa kiongozi wako akufafanulia ucje ukaingia dhambini. Na kwa waislam ninachokijua tiba ya mitishamba imeruhusiwa kisichotakiwa ni kwena kwa mganga apige ramli, kukupa hirizi na mambo mengne ya ushrkna yamekatazwa aliewakataza kwenda kwa babu labda sababu yake kubwa iwe ni kwa kuwa anatoa mkristo ktk micng ya ukristo. Na huyo shehe yahaya anachofanya kwenye dini mbona kinajulikana ni dhambi? Acha niwape angalizo wanajf, usichukuliwe udhaifu wa m2 ndo mkasema ndo dini isemavyo hata km huyo m2 atakuwa kiongozi wa dini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom