Mkuu nia ya serikali si kujua tu kama hizo dawa zinatibu, je zina usalama gani kwa mtumiaji? unaweza ukanywa leo ukapona ukimwi lakini kumbe baada ya miezi 6 unaanza kupata madhara makubwa yanayotokana na hiyo dawa, mara ngapi tumeletewa madawa yanayo tibu lakini kumbe yana madhara makubwa mbeleni.Kupima ufanisi wa kitu kuna njia nyngi: mfano, ufanisi wa mkandarasi unaweza kupimwa kwa kupima ubora wa jengo au barabara aliyojenga na si kukagua vyeti vyake au zana alizotumia. Nawashauri wapime wagonjwa kama wamepona au la.
Ondoa dhana ya kudhani dawa inapimwa ili kujua tu kama inaponyesha au la ili ipigwe marufuku, tambua wale wote wanao kunywa dawa hizi wakianza kupata madhara mbeleni tutakuwa wa kwanza kuhoji serikali ilikuwa wapi