Babu Seya kuachiwa huru na Kikwete?

Babu Seya kuachiwa huru na Kikwete?

Hamna cha kuonewa kama ulifuatilia ile kesi au tafuta hata nakala ya hukumu utaona kuwa walikuwa wakifanya hayo mambo
 
Siyo kweli kabisa.
1.mwalimu wa shule ya Msingi ya Mashujaa, Sigirinda Ligomboka, aliachhiwaje ikiwa watoto walithibitisha kuwaruhusu kwenda kwa Babu Seya kubakwa?
1. Nguza Mbangu, na Francis Nguza waliachiwaje ikiwa walithibitika?
 
Juzi juzi rais mh JK kawapa msamaha wafungwa zaidi ya 700 je hawa wabakaji wa watoto wameachiwa????

1. Nadhani kuna makosa maalum tu rais anaruhusiwa kusamehe la ubakaji haolipo
x
CHOZI LA BABU SEYA BADO LAITESA SERIKALI YA CCM; BABU SEYA AMWAGIZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KWENDA KUMUOMBEA MSAMAHA KWA JK.

Kwa mujibu wa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977, SURA YA PILI, SEHEMU YA KWANZA, IBARA YA 45, inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, ama bila ya masharti au kwa masharti, au kumwachilia kabisa mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote.

Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi la kusamehewa na kuachiwa huru kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam tar 20/06/2014.

Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete. Chikawe akijibu ombi hilo alisema “Mtu akishatumikia kifungo kwa miaka saba au 10 gerezani nina hakika kama ana moyo na nafasi ya kuacha, atakuwa amebadilika hivyo anaweza kupewa msamaha.”

Maswali ya kujiuliza ni:
1.Je, kwa nini jambo hili linamlenga sana JK badala ya mahakama iliyotoa hukumu hiyo??
2.Je, kwani Babu Seya ndiye mfungwa pekee wa maisha katika magereza ya Tanzania? Kama wapo wengine, je, wao wameridhika na adhabu hiyo au hawana pa kusemea?
3.Je, rais ataweza kweli kutumia mamlaka aliyopewa na katiba kuwaachia huru watu hawa? Sheria nyinginezo na historia ya Tanzania zinasemaje kuhusu mfungwa wa maisha kuachiwa huru kwa msamaha wa rais?
4.Ikumbukwe katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2005 JK aliahidi kuwa kama atashinda kiti cha urais basi suala hili la Babu Seya atalipa kipaumbele zaidi, je, alifanya ivyo? Na kwa nini Babu Seya pekee ndio apewe kipaumbele na sio wafungwa wengine?

Mimi binafsi nimekosa majibu ya maswali hayo, naomba mwenye majibu ya uhakika tushirikishane.
:yield:
 
Rais ana mamlaka ya kumsamehe mtu yoyote aliekwisha tiwa hatiani kwa kosa lolote haijalishi kabaka au kaua sheria imempa mamlaka kwa kosa lolote haijatoa excemption
 
Matumaini ya Babu Seya yatarejea tena endapo UKAWA tutachukua dola. Nina imani na Lowasa kwamba atawasamehe mapema familia hii. Mungu awatie nguvu na ujasiri na wazidi kuiombea njaa CCM ili ife rasmi trh 25 wakati wao wakifufuka kutoka gerezani.
 
Hakuna kitu kibaya kama kumfanyia mtu ubaya uliopitiliza wa namna hii. Hakika mungu hulipa endapo chozi la mtu aliyeonewa humtoka akimlilia mungu wake.
 
Afu inaonekana Bubu Msemaovyo kuna mambo mengine unaongea bila hata ushahidi ili mradi tu nawewe uonekane umechangia,,au unataka tukuonyeshe mwenendo wa kesi mpaka hukumu ya babu sea?kama jambo hulijui usipotoshe watu.
 
1. Nadhani kuna makosa maalum tu rais anaruhusiwa kusamehe la ubakaji haolipo
x

mkuu, kwa CCM kila kitu kinawezekana. imagine wameweza kumkunja twiga na urefu wake ule akaingia kwenye ndege....watashindwa kumtoa babu seya? sidhani.
 
Last edited by a moderator:
CHOZI LA BABU SEYA BADO LAITESA SERIKALI YA CCM; BABU SEYA AMWAGIZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KWENDA KUMUOMBEA MSAMAHA KWA JK.

Kwa mujibu wa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977, SURA YA PILI, SEHEMU YA KWANZA, IBARA YA 45, inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, ama bila ya masharti au kwa masharti, au kumwachilia kabisa mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote.

Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi la kusamehewa na kuachiwa huru kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam tar 20/06/2014.

Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete. Chikawe akijibu ombi hilo alisema “Mtu akishatumikia kifungo kwa miaka saba au 10 gerezani nina hakika kama ana moyo na nafasi ya kuacha, atakuwa amebadilika hivyo anaweza kupewa msamaha.”

Maswali ya kujiuliza ni:
1.Je, kwa nini jambo hili linamlenga sana JK badala ya mahakama iliyotoa hukumu hiyo??
2.Je, kwani Babu Seya ndiye mfungwa pekee wa maisha katika magereza ya Tanzania? Kama wapo wengine, je, wao wameridhika na adhabu hiyo au hawana pa kusemea?
3.Je, rais ataweza kweli kutumia mamlaka aliyopewa na katiba kuwaachia huru watu hawa? Sheria nyinginezo na historia ya Tanzania zinasemaje kuhusu mfungwa wa maisha kuachiwa huru kwa msamaha wa rais?
4.Ikumbukwe katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2005 JK aliahidi kuwa kama atashinda kiti cha urais basi suala hili la Babu Seya atalipa kipaumbele zaidi, je, alifanya ivyo? Na kwa nini Babu Seya pekee ndio apewe kipaumbele na sio wafungwa wengine?

Mimi binafsi nimekosa majibu ya maswali hayo, naomba mwenye majibu ya uhakika tushirikishane.
:yield:
Kuna makosa hayana msamaha ikiwemo ya madawa,ujambazi,ubakaji,ulawiti!
Kamwe hawato achiwa kabisa mpaka kifo kitakapo wakuta! Wanacho weza kufanya na kikawasaidia ni kuendelea kukata rufaa wajaribu!

Hayo maneno mengine ya kumhusisha Rais ni ya vijiweni tuu hawa watu walibaka na kudhalilisha watoto na uzuri hata humu zilishaletwa hukumu na rufani za jambo tajwa na ushahidi tukaujadili sana tuu!

Hawato achiwa kamwe!
 
Back
Top Bottom