tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,195
- 27,810
CHOZI LA BABU SEYA BADO LAITESA SERIKALI YA CCM; BABU SEYA AMWAGIZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KWENDA KUMUOMBEA MSAMAHA KWA JK.
Kwa mujibu wa KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977, SURA YA PILI, SEHEMU YA KWANZA, IBARA YA 45, inampa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, ama bila ya masharti au kwa masharti, au kumwachilia kabisa mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote.
Nguza na mwanaye Papii walitoa ombi la kusamehewa na kuachiwa huru kupitia wimbo wakati wakitumbuiza katika maadhimisho ya Siku ya Magereza yaliyofanyika Chuo cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam tar 20/06/2014.
Ombi hilo waliliwasilisha kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe aliyekuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo ambapo Babu Seya na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha), walitumbuiza wakiwa na Bendi ya Wafungwa. Walimwomba Waziri Chikawe kufikisha ombi lao kwa Rais Kikwete. Chikawe akijibu ombi hilo alisema Mtu akishatumikia kifungo kwa miaka saba au 10 gerezani nina hakika kama ana moyo na nafasi ya kuacha, atakuwa amebadilika hivyo anaweza kupewa msamaha.
Maswali ya kujiuliza ni:
1.Je, kwa nini jambo hili linamlenga sana JK badala ya mahakama iliyotoa hukumu hiyo??
2.Je, kwani Babu Seya ndiye mfungwa pekee wa maisha katika magereza ya Tanzania? Kama wapo wengine, je, wao wameridhika na adhabu hiyo au hawana pa kusemea?
3.Je, rais ataweza kweli kutumia mamlaka aliyopewa na katiba kuwaachia huru watu hawa? Sheria nyinginezo na historia ya Tanzania zinasemaje kuhusu mfungwa wa maisha kuachiwa huru kwa msamaha wa rais?
4.Ikumbukwe katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2005 JK aliahidi kuwa kama atashinda kiti cha urais basi suala hili la Babu Seya atalipa kipaumbele zaidi, je, alifanya ivyo? Na kwa nini Babu Seya pekee ndio apewe kipaumbele na sio wafungwa wengine?
Mimi binafsi nimekosa majibu ya maswali hayo, naomba mwenye majibu ya uhakika tushirikishane.
:yield: