Baba yetu naye atakufa lini? Somo!!

Zogoo da khama

JF-Expert Member
May 20, 2013
623
582
Hakuna siku niliyojisikia vibaya kama siku moja nipo nyumbani, kama kawaida yangu nilikua nimelewa chakari, nimejilaza kwenye kochi. Hapo ni baada ya kumtukana mke wangu na kuwaambia wote waende jikoni.

Ilikua ni usiku, lakini baada ya muda njaa ilinibana, nilinyanyuka kwa kuyumbayumba kwenda jikoni ili kudai chakula ambacho mke wangu amepika nikiwa hata sijui pesa katolea wapi kwani asubuhi sikuacha chochote.

Baada ya kufika mlangoni nikiwa kabla sijaupiga teke kama kawaida yangu nilisikia sauti ya mtoto wangu wa miaka minne akimuuliza Mama yake. “Mama eti na sisi Baba yetu anakufa lini?”

Nilistuka, nikasimama na kuanza kusikilzia walikua wanazungumza nini. “Wewe mtoto nyamaza usiseme hivyo ni vibaya, tema mate chini!” Mke wangu alimkemea lakini mtoto hakujali.

“Sasa Mama mbona Dadada amesema Baba yake Juma amekufa, ameenda kwa Mungu na hatarudi tena, kwanini na sisi Baba yetu asiende ili tubaki wenyewe…”

Mtoto aliendelea kuongea, mke wangu alijaribu kumkanya lakini hakusikia aliendelea. Mtoto mwingine mkubwa binti yangu wa miaka kumi yeye alimkatisha kumuelewesha.

“Baba Juma anaenda kwa Mungu kwasababu ni mtu mzuri, Baba yeye hataenda kwa Mungu anaenda kwa shetani, haendi mbinguni….” Alimaliza kumuelewesha mdogo wake, mke wangu alichanganyikiwa zaidi, alijaribu kuwakanya lakini yule mdogo aliendelea…

“Heri Baba hata afe, maana anakupiga wewe kila siku ana sisi kutupiga. Mimi ningekua Rambo ningemuua paaap! Paaa! Pigo moja tu anakufa! Nikiwa mkubwa namuulia mbali” Alionge akwa kujigamba.

Mtoto aliendelea kuongea sasa kwa msisimko. Nilijikuta nasimama wima, pombe zote ziliniishia njaa ilikoma, nilianza kutembea kurudi sebuleni, nilishindwa hata kukaa. Niliingia chumbani na kuanza kujiangalia kwenye kioo.

Nimeyafanya nini maisha yangu. niliwaza nikikumbuka zamani nilivyokua nikitamani kuwa na familia nzuri, kua na mke mzuri na watoto ambao wananipenda.

Lakini sasa mtoto wangu mwenywe, mtoto wa miaka minne alikua anatamani mimi Baba yake kufa! Nilitamani kulia lakini nilijua haitasiadia, niliingia bafuni na kuanza kujitapisha, nilitapika pombe yote, nikaingia kwenye friji nikachukua bia zote na wine.

Nikaenda kuzimwaga kisha nikarudi jikoni, nikafungua mlango kistaarabu nikaumbaia mke wangu sasa nimecha pombe, naomba mnisamehe lakini sasa nimemaua kubadiliaka.

Tangu siku hiyo sijawahi kunywa pombe, kumpiga wala kumtukana mke wangu, nina amani na furaha kuliko kipindi chote. Kumbe manaynyaso niliyokua nikimpa mke wangu yalikua yakiniumiza mimi zaidi kuliko mke wangu.

***MWISHO

Kamwe hakuna furaha ya peke yako, huwezi kufurahi ukiwa mwenyewe, starehe ya peke yako ni starehe ya upweke. Mwanaume unahitaji familia ili uweze kusema unafuraha.

Kama familia yako inalia, mkeo analia basi jua huna furaha. Pia haikufanyi mwanaume kamili, haikufanyi mwanaume zaidi kuwatesa wanao au mke wako, inakufanya mwanaume mpumbavu tu!

Kama wewe ni baba jiulize je kwa unayotenda ipo siku mwanao atayasema haya?
 
Duh imepita miaka mingapi tangu uambiwe hivyo hata Mimi niliwahi kusema hvy uenda ukawa babangu
 
Nimeipenda hadithi hii wewe ni mtuzi hodari nimekuelewa hasa hapa>>>

''Kamwe hakuna furaha ya peke yako, huwezi kufurahi ukiwa mwenyewe, starehe ya peke yako ni starehe ya upweke.''

Asante inabeba famili na baba akiwa muhusika mkuu lakin kuna sura nyingine imejificha ficha hivi. Wanaume furaha ya mkeo na watoto na familia kwa umumla ndiyo furaha yenye kishindo kikuu tuzijali familia zetu .
 
IMG-20170423-WA0057.jpg
 
Nilipokuwa nasoma wale yatima walikuwa wanagaramiwa kila kitu sijui niwafadhili au serikali kuanzia ada,sare,begi na madaftari kila kitu kuhusu shule kwa wale wenye mzazi mmoja walikuwa wanalipiwa ada na madaftari nlitamani angalau baba angekuwa amefariki angalau nipate na mimi kulipiwa ada

Kwa sababu ilikuwa ni tatizo kwangu kupata ada nilikuwa nafukuzwa shule mara nyingi
, baba hakuwa maskini alikuwa akifanya kazi nzuri tu kwenye shirika moja la wajapan alimuacha mama na kwenda kuoa tena
Sijui ugomvi wao coz nilikuwa bado sijajitambua wakati wanaachana lakini baba hakuwahi kutujali kwa namna yoyote Ile

Nilikuwa nikienda kwake kuomba angalau pesa kwa ajili labda ya shule au nyumbani niliishia kurudi nikiwa nalia kwa uchungu sana kutoka kwa majibu nnayopata
 
Nimeipenda hadithi hii wewe ni mtuzi hodari nimekuelewa hasa hapa>>>

''Kamwe hakuna furaha ya peke yako, huwezi kufurahi ukiwa mwenyewe, starehe ya peke yako ni starehe ya upweke.''

Asante inabeba famili na baba akiwa muhusika mkuu lakin kuna sura nyingine imejificha ficha hivi. Wanaume furaha ya mkeo na watoto na familia kwa umumla ndiyo furaha yenye kishindo kikuu tuzijali familia zetu .
Nimeileta hii baada ya kukutana na kisa cha dada mmoja namnukuu"Mwanangu toka nikutoe tumboni baba yako siijui hata senti yako, hajui kula yako, lala yako, vaa yako hata shule haijui kwa miaka mitano sasa, mimi ndo baba na ndo mama, ole wake alete tumbo lake ndo atantambua" mwisho wa kunukuu, hapo unapata picha gani?
 
Back
Top Bottom