Baba yangu mshirikina

Najua kuwa kwenye familia yetu kuna watu wachache wenye majibu mazuri ifikapo Oct, 2010. Basi sasa twendeni kwa ndugu zetu wengine na tuwaambie kuwa baba yetu hamfai mama. Tuna sababu nyingi, si ushirikina tu bali hata tabia yake ya kumtelekeza mama na kwenda kuponda raha kwenye familia nyingine zilizo bora kuliko ya kwetu.

Nasikia mwewe wake amegoma kuruka huko mbali baada ya kuona vumbi jingi angani!!!! Sijui tatizo ni vumbi ama hicho ni kigezo cha kula bata ugenini???
 
- Na wasi wasi na mama yenu maanake yeye ndo anakaa nae naanajua siri zake zote:rolleyez:
 
- Na wasi wasi na mama yenu maanake yeye ndo anakaa nae naanajua siri zake zote:rolleyez:

Lakini kuna mtu amenidokezea kuwa wewe ni mmoja wa familia yetu. Je, wewe unalionaje hilo? Tumwache akae na mama mpaka mkataba wake utakapoisha ama tumfurumushe kwa makaratasi ya kisomo hapo October 2010??

Toa jawabu ili wanafamilia wakurudishe kundini.
 
Kazi ipo mapwa zangu, tumuombeni mungu atuepushe na dhahma zake, mabaya yamueendee mwenyewe mazuri yaje kwa wana.
Sasa hao washkaji zake itakuwaje si ndio kule kule tu watatumaliza hawa tukiwachekea lol,
mi hiyo oct sikubali kupoteza haki yangu kwa mtu asiye rasmi.
 
Kazi ipo mapwa zangu, tumuombeni mungu atuepushe na dhahma zake, mabaya yamueendee mwenyewe mazuri yaje kwa wana.
Sasa hao washkaji zake itakuwaje si ndio kule kule tu watatumaliza hawa tukiwachekea lol,
mi hiyo oct sikubali kupoteza haki yangu kwa mtu asiye rasmi.

Kwa heshima mkuu, tuko pamoja!!!!
Mimi na wewe pamoj na yule hawavuki mwaka huu pamoja na kujipamba kwa mapambio ya maisha bora kwa familia. Hatudanganyiki mwaka huu.
 
mhh Ndugu wenyewe walivyokuwa wa roho na warafi kwa vitu vidogo, maana Baba na nduguze washawagundua kuwa ni wapenda vitu vidogo tena kwa muda tu, sijui kama ndugu wataweza kumuondoa Baba!!!! maana wakipewa Khanga na fulana tu wanasema huyu ndio anatufaa kukaa na Mama
 
- Na wasi wasi na mama yenu maanake yeye ndo anakaa nae naanajua siri zake zote:rolleyez:

Kwa nini unasema mama yenu na usiseme mama yetu? Ina maana wewe si mmoja wa wanafamilia?

Nimegundua kuwa watu wanampenda mama yetu kutokana na uzuri na rasilimali alizokuwa nazo. Na kitendo chake cha kutokuwa na sauti kinamfanya asiamue bali awaache vijana wachague. Mimi nakuunga mikono ndugu yetu Kingwipa1 kwa kutufumbua macho juu ya baba yetu.

Fasihi imetulia sana. JF mahala ninapopa-miss sana.
 
Baba tafadhali badili mwenendo...mimi sioni mwingine wa kukurithi kusema la ukweli kwani wote wanaotaka kumrithi mama wana yao mambo ama hawana competence. So, kama vipi gangamala baba, uachane na wale marafiki zako uliokuwa nao kipindi ukiwa mambo ya nje! temana nao kabisa baba, sepa na uwaache kwenye mataa..
Bado nina imani unaweza...na Mungu akusaidie!
 
Huyu baba aibu tupu yupo tayari kuacha watoto walale njaa yeye akauze sura mhh!!
 
:drum:uyu baba sjui tumkate chakukojolea..............haaaaaaa mie nshachoka bwan........oktoba tumrejeshe kunako jando akamaliziwe baadhi ya viungo ili tupate kuwa huru..............mie nxhachoka...........mama tabakia tu mjane kwa muda mbona ata mamushika naishi pekeyake........?ntampleka kwa rwakatale apate kupata semina za wajane ..she wi catch up da situation bt to live with dead faza iz mercy z gud to .....:painkiller:him before he could that to us ......coz what i c z ......n not a faza as it should b...............!!!!!!!!!!!!
 
Pamoja na tabia zake hizo lakini wanafamilia wengi bado wanampenda sana baba, wanasema matatizo yaliyopo nyumbani yanasababishwa na uchoyo wa akina kaka na kuwa tuvute subira kwani baba atawadhibiti hivi punde.
 
pamoja na tabia zake hizo lakini wanafamilia wengi bado wanampenda sana baba, wanasema matatizo yaliyopo nyumbani yanasababishwa na uchoyo wa akina kaka na kuwa tuvute subira kwani baba atawadhibiti hivi punde.

hatudanganyiki ng'ooo
 
Leo nimepita kwenye hii thread nimecheka sana na nikiangalia post yangu niliyochangia hapa!!!! Dah kweli ushirikina huu sasa umekuwa wa chuma ulete maana hata hela mifukoni hazikai na rasilimali zetu wanachuma tu hadi wanyama hai wanasafirishwa nje ya nchi. Kweli ni lazima ushirikina ulitumika hapa.
 
Back
Top Bottom