Baba yangu alichanganyikiwa au?

kazuri kakid

Member
Oct 6, 2021
15
118
Nawasalim kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mimi nimezaliwa familia ya kawaida tu, baba yangu alikuwa mwalimu ila aliacha kazi bila sababu za msingi.

Nina dada zangu ila wote hawajafanikiwa kimaisha. Huyu baba tukimuulizaga kwanini hakujiwekeza ujanani na wakati alikuwa na uwezo huo anajibu kuwa eti hakutaka utajiri. KamalizaKamaliza form four 1972.

Hivi huku ni kurogwa? Alikataa Uhakimu, alitakiwa kusoma urubani pia baba yake akakataa, na ualimu wenyewe aliacha, yaani simuelewi, sasa kwanini aangaike uzeeni?

Alitusomesha, na alitimiza wajibu wake kama baba, ila kwanini hakutaka utajiri wakati alikuwa na uezo huo? Marafiki zake wengi ni wakurugenzi na watu wenye hadhi zao.

Huwa anasema hataki utajiri, hata nyumba ya cement alikuwa hataki tumemlazimisha sisi watoto tukamjengea, hivi huyu baba anafikria nini? Mbona anatudhalilisha watoto hasa si wa kike?

Na anasema kabisa kuwa eti angetaka utajiri basi angekuwa trilionea ila hakutaka. Na anaridhika kabisa na maisha aliyopitia, hajutii kupoteza nafasi ujanani.

Watu wa saikoloji nishaurini kabla sijaanza kutafuta ukweli kama ni baba yangu mzazi. Naumia mno
 
Wala hana tatizo la kiakili. Kuna wazee wengi walikua na uwezo wa kupata maisha mazuri zaidi kipindi chao cha ujanani na hata baada ya kustaafu ila walimezwa na uzalendo waliokua nao na viapo vya wakati ule ilikua na ufuatiliaji wa kibabe toka kwa viongozi wa juu enzi hizo hivyo kujikuta wanafanya kazi huku wakifurahia status zao na marupurupu ya makazi na huduma nyinginezo. Hayo yote nimeacha kumuuliza mzee baada ya kua mkubwa na kuendelea na maisha yangu kwa nafasi zangu'
 
Zaman watu weng walkuwa wanaacha kazi na sjui n kwann,sio baba ako tu

Wengi wao sasa wamezeeka na wanamaisha magumu

Kuna ndugu yetu mmoja yeye ndo niliona alifanikiwa aliacha ualimu na akawa na gereji yake yupo na maisha mazuri tu mpaka sasa
 
kwa kuwa baba yako sio tajiri na hakufanya juhudi zozozte za kuwa tariji anangali yupo kijana, basi hiyo ndio inakupa mashaka kuwa anaweza asiwe baba yako mzazi? serious ?

baba yako alichagua maisha yake, na wewe ni zamu yako chagua maisha yako. kama unataka pesa zitafute uwe tajiri baadae watoto wako wasije kukukataa wewe sio mzazi wao kwasababu haukuusaka utajiri ujanani.
 
Hii nchi hii….Yaan sikuhizi kuna Vijana hopeless kweli kweli….
Mleta mada wewe una umri gan na mpaka sasa hivi una pesa kiasi gani?
Hebu tufafanulie hapo before hatujasema chochote juu ya mzee wako
 
Enzi za ujamaa hatukutakiwa kuwa matajiri hata mimi ningetaka leo ningekuwa billionea
 
Kama ni kweli huo ni mwenendo wa baba yako na wewe hii tabia uliyoonyesha ya kuja kutuuliza sisi Mambo yako ya familia yako basi familia yako yote mtakua mnavichaa
 
Hekima aliyotumia ni kuwa akipata mali na uweso mkubwa angepata stress sana za wanadamu ukiwa tajiri kibongobongo jamii itakusakama kwa kila baya, utaitwa mtoa kafara, utasukumiwa kila aina ya shida uitatue hata kama wengine wana uwezo huo kwa utakaposhindwa kininadamu tu utasakamwa balaa, na mwisho kuna wale wenye roho zao mbaya tu watakutafutia sababu mpaka wakuloge ufe uache watoto wakiteseka.
 
Back
Top Bottom