Baba wa taifa kutangazwa mwenye heri, wakatoliki hili limekaaje?

Kumbe tupo pamoja mkuu,hawa jamaa hawajui kuna watakatifu walikua wanajeshi na wameua sana vitani

Hao mpaka Ellen White awafundishe ndio waamini jambo lolote. Kwa hiyo, kwa kuwa Mwl. Nyerere mchakato wake kutangazwa Mwenye heri na mtakatifu umeanza wakati Ellen White akiwa hayupo duniani, basi itakuwa ngumu kwao kuamini kwamba Nyerere anaweza kutangazwa mtakatifu.
 
Mshamba Wa ukristu. Kaja Jana katika Ukristu achana naye. Mkaushie bado anajifunza kutambaa katika imani.
Ungetumia lugha ya ukristu ingependeza ili watu wote wasadiki yakuwa wewe u mfuasi wa Kristi miaka mingi hujaongoka sasa.
 
Wapo.wengi wameua hujui.maandiko, Mungu mwenyewe anaua kupitia gharika na safina sembuse Nyerere mtakatifu,

Japo hakuna ushahidi wa Moja kwa Moja wa kuua lakin sidhani kama kuna rais anaingia madarakani na kutoka bila kuua,

Inaitwa poteza wachache ili waliowengi watawalike vema
Sidhani kama nina cha kukujibi kwenye hoja ya Mungu kuua maana hiyo ni kufuru kwangu kuizungumzia.
Naongelea mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke akaishi kama mwanadamu duniani na akisha kufa akatangazwa kuwa mtakatifu. Ndio hoja yangu kuhusu baba yetu huyu je anastahili au hastahili?
 
Paulo ni mtume sio mtakatifu
Mkuu fanya mpango utafute kitabu chenye orodha ya watakatifu wa kanisa katoliki.
Huku parokiani kwetu kanisa linaitwa la Mtakatifu Paulo, labda huyu ni tofauti na Sauli.
 
Mtume Paulo aliua sana leo hii barua zake zinaunda Bibilia.

Mtakatifu ni mwenye dhambi aliyeweza kutubu na kumaliza maisha yake katika hali ya uwepo wa Mung (hali ya neema)
 
Kwahiyo ni sahihi kumtangaza utakatifu asiye na rekodi ya matendo matakatifu maishani mwake?
Hatuongelei Mitume wateule wa Mungu mwenyewe tuongelee watakatifu wateuliwa/watangazwao na sisi wenyewe.
Kwani mitume walivyoitwa na Yesu waliacha dhambi aroo? Na unaielewaje tafsiri ya neno Mtakatifu?

Mtakatifu ni yule ambaye yupo katika uwepo wa Mungu (kauona uso wa Mungu) baada ya maisha ya duniani kwani Mungu mwenyewe ni Mtakatifu na ametuambia kwenye Bibilia tuwe watakatifu kama yeye alivyo mtakatifu. Hii haijalishi wewe ni Mkristu ama wa madhehebu mengine. Mungu anajua anavyodeal na watu wake.

Sanctity is not a preveledge of few people but a call of GOD to humanity.
 
Inaelekea huelewi maana ya Yesu kushuka duniani! Kama wewe ni Mkristu basi bila shaka utakuwa ni wale Wa Vikundi vinavyojifunza ukristu.

Yesu alikuja kuwafanya wadhambi wawe marafiki zake na kisha waingie Mbinguni kula "Bata". Kama ndivyo, wewe unashangaa nini? Kama mwenye mbingu yake,Yesu Kristu, anawakubali wadhambi na kuwapokea wewe ni nani hata uhoji mchakato Wa kutangazwa Mwl.Nyerere, Mwenye Heri? Hebu jifunze hivi:

1, Mtume Petro ni Mtakatifu. Yeye alimkana Yesu wakati Wa mateso yake.
2. Paulo ni Mtakatifu. Alikaba na kuchinja wakristu wengi sana. Mbona hujahoji utakatifu wake?
Asipoelewa hili basi tumuachie Mungu.
 
Dini is for Stupids....

Yaani grupu la watu wazinzi ,waasherati na wazandiki kama mimi wanakaa kwenye meza wanapiga kura eti fulani awe "mtakatifu"..

Mbwa kasoro mikia kabisa...
Acha kufuatilia habari zao sasa. Na uzi kama huu usiwe unajiingiza kama huusiki. Watu kama nyie mnaojiita atheists huwa hamuachi kutaja jina la Mungu hata kama hamuamini.
 
Wapo.wengi wameua hujui.maandiko, Mungu mwenyewe anaua kupitia gharika na safina sembuse Nyerere mtakatifu,

Japo hakuna ushahidi wa Moja kwa Moja wa kuua lakin sidhani kama kuna rais anaingia madarakani na kutoka bila kuua,

Inaitwa poteza wachache ili waliowengi watawalike vema
Kina mfalme Daudi walivyokuwa wanapigana vita mpaka Mungu kamwambia huwezi nijengea hekalu maana mikono yako imejaa damu lakini sio kama Mungu alimuacha no alikuwa naye na akaandaa mazingira ya mwanaye ndiye amjengee Mungu hekalu, watakatifu wengi kabla ya kuongoka wanakuwa watenda dhambi sana, asiyejua kitu muache
 
Mkuu fanya mpango utafute kitabu chenye orodha ya watakatifu wa kanisa katoliki.
Huku parokiani kwetu kanisa linaitwa la Mtakatifu Paulo, labda huyu ni tofauti na Sauli.
Mtume Paulo alikuwa akiitwa Saul kabla hajatokewa na Yesu mwenyewe kumuongoa, hayo yako juu ya uweza wa mwanadamu kwakuwa si yeye aliyemfanya kuwa mtume Bali yeye Mungu.

Lakini haimaanishi kuwa Paulo mwingine asiwepo nje ya Paulo mtume.
 
Mtume Paulo aliua sana leo hii barua zake zinaunda Bibilia.

Mtakatifu ni mwenye dhambi aliyeweza kutubu na kumaliza maisha yake katika hali ya uwepo wa Mung (hali ya neema)
Kwa wakatoliki anayepewa mpako wa wagonjwa na mpako wa mwisho anakuwa amekufa kifo chema, lakini hatangazwi mtakatifu kwa sababu hi I.
 
Kina mfalme Daudi walivyokuwa wanapigana vita mpaka Mungu kamwambia huwezi nijengea hekalu maana mikono yako imejaa damu lakini sio kama Mungu alimuacha no alikuwa naye na akaandaa mazingira ya mwanaye ndiye amjengee Mungu hekalu, watakatifu wengi kabla ya kuongoka wanakuwa watenda dhambi sana, asiyejua kitu muache
Katika kitabu cha watakatifu wote wa Mungu Daudi hajatajwa.
 
Back
Top Bottom