Huo sio waraka wa kwanza nawa mwisho kutoka kwa mababa wetu wa kiroho

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Ni Jumapili yenye baraka nyingi sana kwa watu wote wenye mapenzi mema na nchi hii ila itakua Jumapili chungu sana kwa watu wote walioamua/wanaotaka kuuza nchi hii kwa vipande 30 vya fedha kwa tamaa zao binafsi.

Hakika Mwl Nyerere(Rip) laiti siku ya leo angejaliwa baraka za kufufuka tena la kwanza angemshukuru Mungu wake kwa kumpa neema hiyo kwa kufufuka mara ya pili kwani aliyepata neema hiyo ni Masia Bwana Yesu tu.

Ila baada ya kufufuka na kuhudhuria kanisa leo na kusomewa/Kusikiliza mkataba kati ya Tanzania & DP world hakika angeweza kufa tena au yeye mwenyewe angeomba kufa tena ili arudi mbinguni.

Tumesali na Kutafakari.

Haya ni moja ya kati ya maneno mazito sana yaliyoambatana na Waraka wa Kichungaji wa Mababa zetu wa kiroho uliosomwa leo karibia makanisa yote ya Kikatoliki Tanzania.

Baba zetu wa kiroho wametwambia wamesali kwanza na kutafakari kabla ya kuja na waraka huu mimi na wewe hatujui wamesali sala gani ila kwa maongozo ya Roho Mtakatifu naimani ndio kawaongoza kuandika kilichoandikwa kwenye waraka wa leo kama wakristo wengi tunavyoamini Mungu Roho Mtakatifu ametupa karama tofauti za kutambua mema na mabaya.

Kumbe basi kwa maongozo ya Roho Mtakatifu na tafakari zao wametambua mkataba husika hauna tija kwa taifa leo bali unafaidisha upande mmoja ambao ni Dubai Emirates swali la kujiuliza kwanini watawala wengi wanaupigia chapuo je ni Rushwa, kiburi cha mamlaka, kutoheshimu wananchi waliowapa hizo nafasi, kukosa busara za Kimungu ? mimi na wewe hatujui tuelewe kiburi ndio silaha kubwa ya Shetani watawala wakiendelea na hiki kiburi pasipo na shaka anguko lao limefika.

Mababa wetu wa kiroho wamewakilisha sauti ya watu wengi kama maandiko yanavyosema sauti ya watu ni sauti ya Mungu basi baada ya waraka wa leo yataibuka makundi ya kila aina wakija na hoja zao za kupinga ni sawa ila watambue hawapambani na kanisa wala maaskofu bali wanapambana na Mungu mwenyewe ambaye kupitia viongozi wake wa kiroho kwa uchache wao watumike kuwasilisha sauti za watu wengi wanaolia kwa mkataba wa kilaghai na pia Wamasai wa Loliondo waliokosa watetezi na utu wao kubezwa na watawala wenye nguvu & mamlaka.

Huo sio waraka wa kwanza nawa mwisho kutoka kwa mababa wetu wa kiroho nakumbuka walishatoa Nyaraka nyingi tu kipindi cha nyuma kuna waraka mmoja walitoa nchi ikiwa kwenye kipindi kigumu sana cha utawala mtawala aliyekuwepo aliishia kuwabeza na kuwacheka kwenye majukwaa ya siasa badala ya kumwomba Mungu roho mtakatifu ampe hekima zaidi aliishia kusema "Nawaangalia na kuwacheka tu" bado viburi vinatutawala tukipata mamlaka kidogo kwenye huu ulimwengu.

Kumbe basi ni muda muafaka wa watawala wetu kujitafakari na kufanya maamuzi magumu tena kama walivyofanya maamuzi magumu awali ya kuuza nchi yetu kwa vipande 30 vya fedha na wasishupaze shingo zao.

Jumapili njema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom