Baba wa mwanakwaya aliyeuawa ajutia posa ya mwanaye

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Baba wa Mariam mwimbaji wa kwaya ya vijana ya kanisa la AICT Chang'ombe (CVC) jijini Dar es Salaam, Charles Lutonja amesema hakujua kama 'posa' ingeondoa uhai wa mwanae na sasa amemwachia Mungu.

Mariam anadaiwa kuuawa kwa kunyongwa na mchumba wake katika nyumba ya kulala wageni iliyopo Buza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo, Lutonja alisema taarifa juu ya posa ya mwanae ilifikishwa kwa misingi ya maadili hivyo hawakuwa na wasiwasi juu ya muoaji.

"Posa ilipokelewa vizuri, walikuja na washenga tena hata kanisa lilisaidia kusimamia jambo hili," alisema na kuongeza:

"Tena barua ya posa ilipokuja nilimuachia mjomba wake apokee nilikuwa safarini, sikutarajia kama posa ya mwanangu ingesababisha mauti ayke."

Rafiki wa karibu wa Mariam, Jesca Julius alisema alimuona mchumba wa Mariam siku moja kabla ya mauaji.

"Alichati na mimi, alinitafuta baada ya kumkosa Mariam kwenye simu lakini baadae akaja akanikuta na Mariam. Nilimuuliza mbona umekuja ghafla? akasema eeh basi nikamkaribisha, hakukaa," alisema.

Mwenyekiti wa vijana katika mtaa wa Keko, Paul Peter alisema isingekuwa rahisi kwa wazazi kujua tabia za ndani za kijana huyo kwa sababu alijificha kwenye mwavuli wa kwaya.

"Ni tukio la kusikitisha kwa sababu namfahamu Mariam tangu mdogo, alikuwa binti mstaarabu. Hata kijana mwenyewe alikuja kipole na kiungwana isingekuwa rahisi kumjua," alisema.
 
Mapenzi hayana tabia, huyo mzee mkewe abunguliwe na ajue na sisi tuone tabia yake

RIP Posa
 
haya mambo huwezi jua upande wa pili, yawezekana mariam amechangia kifo chake mwenyewe, yawezekana ametumia gharama nyingi na kuanza danadana km madenge unategemea jamaa atafanyaje?
ww mchumba wa mtu hupatikani hewan halafu unakutwa kwa shoga kweli.
haya mambo yamenikuta
 
Mapenzi hayana tabia, huyo mzee mkewe abunguliwe na ajue na sisi tuone tabia yake

RIP Posa
Aisee " hahaa " kwani wadhani hajawahi kubanguliwa"""? anatumia hekima tu " Yakuchapiwa ni siri ya ndani
 
Aisee " hahaa " kwani wadhani hajawahi kubanguliwa"""? anatumia hekima tu " Yakuchapiwa ni siri ya ndani
Hayo hayana fundi yanahitaji hekima, ila hekima zipo kwa mmoja mmoja na si kila mtu

Kikubwa wasijaji tabia ya jamaa huko nyuma, kilichotokea ndani ni siri yake na marehemu
 
Hayo hayana fundi yanahitaji hekima, ila hekima zipo kwa mmoja mmoja na si kila mtu

Kikubwa wasijaji tabia ya jamaa huko nyuma, kilichotokea ndani ni siri yake na marehemu
Aisee mtihani sana "... sawa chief
 
haya mambo huwezi jua upande wa pili, yawezekana mariam amechangia kifo chake mwenyewe, yawezekana ametumia gharama nyingi na kuanza danadana km madenge unategemea jamaa atafanyaje?
ww mchumba wa mtu hupatikani hewan halafu unakutwa kwa shoga kweli.
haya mambo yamenikuta
Usemalo huenda kweli huyo alitaka kuitosa posa na alianza zile zao za kikekike, mtu huwezi kumuua mpenzi wako kabla ya posa lazima issue nzima ipo around hicho kitu...'POSA'.
 
Back
Top Bottom