Baba wa Mhe. Joseph Selasini Afariki

Ina sikitisha na kuuma sana, pamoja na machungu yote hayo.....
Poleni sana wafiwa.
 
Nakupa pole ya dhati kabisa mh. Joe. Usijali mtangulize mungu. Dah imefanana kiasi fulani na mkasa wa ayubu anayeelezwa kwenye bible agano la kale. God is there for you, just call him. May daddy's soul rest in peace.
 
kwani dr masumbuko lamwai na mh joseph selasini ni ndugu?

Poleni sana Mh. Joseph Roman Selasin na Mpwa wako Dr. Masumbuko Lamwai. Mzee Roman Selasini ni Mjomba wake the disgraced Lawyer Dr. Masumbuko Lamwai.
 
Pole sana Mheshimiwa. Mwenyeezi Mungu atakupa subra. Na amlaze popote atapoona anastahili.
 
unapita kwenye kipindi kigumu sana katika maisha yako lakini kikubwa na kujipa moyo na kumtegemea mungu kwani yeye ndiye muweza wa kila kitu, majaribu hayana budi kuwepo ila kikubwa ni kuyashinda!
R.I.P DAD!!!
 
Pole sana mheshimiwa. Umepita katika bonde la uvuli wa mauti lakini Bwana Yesu yu pamoja nawe.
 
Duh, poleni sana ndungu na jamaa wote, huu ni msiba mzito sana, ikumbukwe kama sikosei wakati Mh Mbunge anapata ajali alitoka kumuangalia Mzee akiwa amelazwa hospital
 
pole sana kamanda.mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu.mungu amlaze mahalipema peponi mzee wetu. Amina
 
TANZIA:

Baba yangu Mzazi Mzee Roman Selasini Amefariki Jioni ya Leo saa 12:15 Katika hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa akiendelea na Matibabu.
R.I.P My Dad.

Joseph Roman Selasini
MB-Rombo
CHADEMA



Source: Mhe. Selasini on Social Networks

R.I.P Hon.Roman Selasini Shao
 
"Nanyi kwa Subira yenu, mtaziponya nafsi zenu"
Mh. Selasini sijui nikuambie nini ili ufarijike, maana kama ni majaribu umeyapata brother. Ila neno hili likutie faraja kwa uvulivu na subira yako utaiponya nafsi yako. Wala usifikiri hata mara moja kwamba Mungu amekuacha au hakupendi tena kwa kuwa imeandikwa "Yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka"

Pole sana Kaka, na Mungu ailaze roho ya Mzee wetu Mahali pema peponi.

Its me your brother Onesphor.


]TANZIA:
 
Pole sana Joseph Roman Selasini
kweli nina makosa nilishindwa kufika hata
hapo mhimbili kuwaona, poleni sana Mungu yupo
pamoja na nyie.
 
Back
Top Bottom