Baba wa mchumba wangu alimuua baba yangu

kifo cha baba yako hakitaleta amani kwenye ndoa yenu labda uamue kusamehe wewe mwenyewe na usamehe kweli.. ila sababu baba yako kifo chake kiliumiza wengi hao wengine watageuka chachu kwenye ndoa yenu kwa namna moja au nyingine .. ushauri wangu mueleze ukweli huyo binti na mwache aendelee na maisha yake sababu hata ndugu zako kufanya utaratibu wa ndoa italeta mushkeli kidogo na kuleta mtafaruku
Nampenda sana, najua nikimweleza ukweli anaweza kushtuka sana, yule ni mtoto wa kike, mbali na majuto ya baba mdogo wake, kwa namna anavyonipenda na malengo tuliyojiwekea naweza kumtafutia matatizo mengine, sipati picha kilio atakacholia, atanizimikia naogopa!

Nishauri namna yakumweleza ukweli bila kusababisha madara zaidi
 
Baba yake mdogo bado yu hai? Kuna uwezekano utakapomweleza huyo binti hayo unayofikiri ndio yaliyomsibu baba yako, basi naye ataamua kuutafuta ukweli, ambao utaleta uhasama, pengine kupelekea kuhatarisha maisha yako. Ikiwezekana achana naye, bila ya kumpa hiyo sababu.
Baba mdogo wake yupo hai, ila hayuko karibu sana na familia yao, ni tajiri mbinafsi!
 
Nampenda sana, najua nikimweleza ukweli anaweza kushtuka sana, yule ni mtoto wa kike, mbali na majuto ya baba mdogo wake, kwa namna anavyonipenda na malengo tuliyojiwekea naweza kumtafutia matatizo mengine, sipati picha kilio atakacholia, atanizimikia naogopa!

Nishauri namna yakumweleza ukweli bila kusababisha madara zaidi
Vella sawa anakupenda ila wewe umempoteza mpendwa wako leo .. kama unaina huwezi kumwambia ukweli kuhusu baba yako ni vyema ukaamua kumtema kimya kimya .. ukweli unauma sana lakini utakuweka huru ... kama unaona utaweza kuface real situation in future okey endelea
 
Umesema umesoma sheria, unamfungulia mashtaka kwa ushahidi gani?
Ushahidi upo wa mazingira, na mawasiliano yao ya mwisho ninayo kwenye simu aliyokuwa anatumia mzee wangu
 
Wadau salaam.
Naitwa Vella ni kijana wa miaka 28 naishi Masaki D'salaam, nina shahada moja ya udaktari wa binadamu na stashahada ya sheria. Mchumba wangu ana shahada ya Biashara na Utawala

Sijao ila nina mchumba wangu tangu tukiwa Advance, hadi leo tunaishi vizuri kwa kuheshimiana, kujaliana na kusikilizana, ananipenda nami nampenda sana tena sana.

Lakini kuna jambo linanisumbua sana moyoni na kunikereketa sana akilini, iko hivi wakuu, Baba yangu alikuwa ni wakili wa kujitegemea, kipindi nikiwa O level baba mdogo wake na mchumba wangu ambaye alikuwa ni mfanya biashara, alimpiga mtu barabarani na kumuumiza vibaya sana, wakati huo baba yangu alikuwa akitoka kazini jioni hivyo alishuhudia tukio zima akiwa kwenye gari yake.
Akaondoka zake kuelekea nyumbani, kesho yake baba ake mdogo na mchumba wake alikuja nyumbani kumwomba baba akamsaidie kusimamia kesi yake yakupiga na kujeruhi mtu aliyempiga jana yake baada ya yule mtu kwenda kumuishataki polisi.

Baba alikataa na kusema yeye ni Wakili ambaye lengo lake ni kusaidia watu kwa haki, akamwambia yupo tayari kutoa ushahidi mahakamani kwa aliyoyaona km raia mwema na sio wakili.

Yule mzee aliitwa mahakamani, lakini akawa anakuja kumwomba mzee wangu kila siku ili akubali kwenda kumsaidia kesi yake, Baba alikuja kukubali akaenda mahakamani, kadiri siku zilivyozidi kwenda baba alikuwa akirudi nyumbani akiwa analalamika kuwa mteja wake hamlipi malipo yake, waliendelea hivyo lakini karibia kufikia mwisho wa kesi mzee wetu alirudi nyumbani na kukiri mazingira ya mtuhumiwa kutenda lile kosa hayampi mteja wake ahaueni yakushinda kesi zaidi ya kushindwa.

Basi mtuhumiwa pia naye alishaanza kunusa harufu ya kushindwa kesi, hivyo alichokifanya, alimwita baba yangu nyumbani kwake, wakala chakula, mzee akarudi nyumbani alivyopewa chakula aliomba asile na badala yake wapewe watoto maana yeye ameshiba kwani alisema alikula kwa huyo mzee mwenye kesi.

Mzee wangu kesho yake alifajiri aliamka akiwa anaumwa sana, hakuweza kuongea, ila alikuwa akigalagala kwa maumivu, na hatimae kufariki.

Niliskia familia yetu (baadhi) wakihusanisha kifo cha baba yangu na mipango miovu ya mteja wake. Kwani baada tu ya kifo cha baba yangu yule mzee kesho yake alitorokea mjini Arusha, na wala hata baada yakurudi hakuja nyumbani kutoa pole, licha ya kwamba alikuwa ni jirani yetu wa mtaa moja.

Turudi kwa Mchumba wangu, Mchumba wangu hili jambo hakuwahi kulifahamu kwani hata habari za kifo cha baba yangu nilimjuza mimi majuzi tuu, hajui chochote kuhusu kesi ya babaake mdogo na baba yangu, ingawa mimi nafahamu.

Huyu binti nampenda sana, mara kadhaa tumekuwa tukijadili kuhusu kuvalishana pete ya uchumban lakini moyo wangu unakosa utayari. Mwaka mmoja na nusu niliwahi kumwacha kwa siri baada yakuwa na msongo wa mawazo kuhusiana na mambo ya baba yake mdogo na kifo cha mzee wangu, ila aliendelea kuwa karibu sana na mimi hadi mwaka juzi tukarudiana tena japo sikumwambia sababu za kumwacha, zaidi ya kumwambia "sikukuacha ni ukali wa maisha na ubusy wa masomo" kwani wakati yeye akiwa chuo kikuu cha D'salaam mimi nilikuwa masomoni nchini Finland.

Hivyo wadau naombeni ushauri, je huyu binti niachane naye kimya kimya au nimpe mkanda mzima wa kifo cha mzee wangu na jinsi babaake mdogo alivyohusika?

Au niendelee naye tu kisha tuoane? Je familia yangu haitajiskia vibaya? (Japo hakuna uhasama wowote wa wazi kati ya hizo familia mbili)

Nifanyaje wadau wangu, Naombeni Mawazo Yenu.
Mwambie baba mdogo au mkubwa amwue baba wa mchumba wako ili wrote msiwe na baba.
 
Kwanza pole sana pili huna ushahidi wa kuthibitisha kama baba yako aliuawa katika mazingira unayoyaamini. Hata kama kuna ukweli lakini huyo binti hajui lolote na wala hakuhusika katika kifo cha Baba yako. Ila kama kumvisha pete huyu na hatimaye kufunga naye pingu za maisha kunakunyima amani moyoni basi ni bora umwambie kweli mapema badala ya kuendelea kumpotezea muda wake.
 
sikubaliani na wanaosema mchumba wako hana kosa. mikono imwagayo damu laana yake hupatiliza.
mie sikushauri wala hata umwambie just tell her siwez kukuoa basi.

jiulize hivii.................hivi siku ya harusi unaambiwa uwashike wakwe mkono utaanzaje kumshika buyo baba bila kutokwa na chozi?

afu pata picha baba yako huko aliko anakuona na anaona umejiunga urafiki na wale waliomuua na pengine anasema 'mwanangu huyu aliniua' utamjibuje?

hao wanalaana ya kuua na usishange hata wewe wakataka jambo la kinyume na taratibu zako ukawagomea wakakuua.
Swali hapa: Kuna mtu aliyethibitisha pasipokuwa na shaka kuwa baba mdogo wa binti ndiye aliyemuua baba wa mleta mada???
 
Wadau salaam.
Naitwa Vella ni kijana wa miaka 28 naishi Masaki D'salaam, nina shahada moja ya udaktari wa binadamu na stashahada ya sheria. Mchumba wangu ana shahada ya Biashara na Utawala

Sijao ila nina mchumba wangu tangu tukiwa Advance, hadi leo tunaishi vizuri kwa kuheshimiana, kujaliana na kusikilizana, ananipenda nami nampenda sana tena sana.

Lakini kuna jambo linanisumbua sana moyoni na kunikereketa sana akilini, iko hivi wakuu, Baba yangu alikuwa ni wakili wa kujitegemea, kipindi nikiwa O level baba mdogo wake na mchumba wangu ambaye alikuwa ni mfanya biashara, alimpiga mtu barabarani na kumuumiza vibaya sana, wakati huo baba yangu alikuwa akitoka kazini jioni hivyo alishuhudia tukio zima akiwa kwenye gari yake.
Akaondoka zake kuelekea nyumbani, kesho yake baba ake mdogo na mchumba wake alikuja nyumbani kumwomba baba akamsaidie kusimamia kesi yake yakupiga na kujeruhi mtu aliyempiga jana yake baada ya yule mtu kwenda kumuishataki polisi.

Baba alikataa na kusema yeye ni Wakili ambaye lengo lake ni kusaidia watu kwa haki, akamwambia yupo tayari kutoa ushahidi mahakamani kwa aliyoyaona km raia mwema na sio wakili.

Yule mzee aliitwa mahakamani, lakini akawa anakuja kumwomba mzee wangu kila siku ili akubali kwenda kumsaidia kesi yake, Baba alikuja kukubali akaenda mahakamani, kadiri siku zilivyozidi kwenda baba alikuwa akirudi nyumbani akiwa analalamika kuwa mteja wake hamlipi malipo yake, waliendelea hivyo lakini karibia kufikia mwisho wa kesi mzee wetu alirudi nyumbani na kukiri mazingira ya mtuhumiwa kutenda lile kosa hayampi mteja wake ahaueni yakushinda kesi zaidi ya kushindwa.

Basi mtuhumiwa pia naye alishaanza kunusa harufu ya kushindwa kesi, hivyo alichokifanya, alimwita baba yangu nyumbani kwake, wakala chakula, mzee akarudi nyumbani alivyopewa chakula aliomba asile na badala yake wapewe watoto maana yeye ameshiba kwani alisema alikula kwa huyo mzee mwenye kesi.

Mzee wangu kesho yake alifajiri aliamka akiwa anaumwa sana, hakuweza kuongea, ila alikuwa akigalagala kwa maumivu, na hatimae kufariki.

Niliskia familia yetu (baadhi) wakihusanisha kifo cha baba yangu na mipango miovu ya mteja wake. Kwani baada tu ya kifo cha baba yangu yule mzee kesho yake alitorokea mjini Arusha, na wala hata baada yakurudi hakuja nyumbani kutoa pole, licha ya kwamba alikuwa ni jirani yetu wa mtaa moja.

Turudi kwa Mchumba wangu, Mchumba wangu hili jambo hakuwahi kulifahamu kwani hata habari za kifo cha baba yangu nilimjuza mimi majuzi tuu, hajui chochote kuhusu kesi ya babaake mdogo na baba yangu, ingawa mimi nafahamu.

Huyu binti nampenda sana, mara kadhaa tumekuwa tukijadili kuhusu kuvalishana pete ya uchumban lakini moyo wangu unakosa utayari. Mwaka mmoja na nusu niliwahi kumwacha kwa siri baada yakuwa na msongo wa mawazo kuhusiana na mambo ya baba yake mdogo na kifo cha mzee wangu, ila aliendelea kuwa karibu sana na mimi hadi mwaka juzi tukarudiana tena japo sikumwambia sababu za kumwacha, zaidi ya kumwambia "sikukuacha ni ukali wa maisha na ubusy wa masomo" kwani wakati yeye akiwa chuo kikuu cha D'salaam mimi nilikuwa masomoni nchini Finland.

Hivyo wadau naombeni ushauri, je huyu binti niachane naye kimya kimya au nimpe mkanda mzima wa kifo cha mzee wangu na jinsi babaake mdogo alivyohusika?

Au niendelee naye tu kisha tuoane? Je familia yangu haitajiskia vibaya? (Japo hakuna uhasama wowote wa wazi kati ya hizo familia mbili)

Nifanyaje wadau wangu, Naombeni Mawazo Yenu.
Kabla sijasema lolote, kuna mtu yeyote aliyethibitisha pasipokuacha shaka kuwa baba mdogo wa mchumba wako ndiye aliyemuua baba yako???
 
Samehe ila kama huwez bhas muue mtoto wake ambae ndio mchumba wako ili kulipa kisas.
Duuh!huu ushauri wako mmkuu unatia ukakasi kama vile nimekosea kusoma au miwani yangu haiko sawa
 
Vella sawa anakupenda ila wewe umempoteza mpendwa wako leo .. kama unaina huwezi kumwambia ukweli kuhusu baba yako ni vyema ukaamua kumtema kimya kimya .. ukweli unauma sana lakini utakuweka huru ... kama unaona utaweza kuface real situation in future okey endelea
Sitoweza kuja kuhimili changamoto zinazohusiana na kifo cha babaangu, kwani aliipenda sana familia yetu, alitusapoti sana masomoni hadi kukubali kukata kiasi fulani cha kipato chake na kutuwekea kwenye akaunti ambayo ndiyo iliyonisaidia kwenda finland kusoma, alitu inspire sana hivyo ni lazima nimkumbuke tuu!
 
Mwambie baba mdogo au mkubwa amwue baba wa mchumba wako ili wrote msiwe na baba.
Ha ha ha unataka nyumba yetu nayo inuke damu? Na niko na dada mrembo si atakosa mume ndugu??
 
Binafsi sikushauri umueleze juu ya hilo jambo maana moja kwa moja mkiachana atajua ndo sababu na inaweza ibua matatizo mengine.

Pia kweli binti hana kosa na mwenye unakiri anakupenda sana na unawish awe mkeo ishu ni kuwa ndoa itakuwa na changamoto maana kila ukimuona unamkumbuka mzee wako utakuwa mwenye hasira na huzuni mara kwa mara wakati yeye hajui kinachoendelea so itakuwa changamoto sidhani kama ndoa inawork out

Nkuulize je ushawah ongea na nduguyo wa karibu yoyote akakushauri???
 
Kwanza pole sana pili huna ushahidi wa kuthibitisha kama baba yako aliuawa katika mazingira unayoyaamini. Hata kama kuna ukweli lakini huyo binti hajui lolote na wala hakuhusika katika kifo cha Baba yako. Ila kama kumvisha pete huyu na hatimaye kufunga naye pingu za maisha kunakunyima amani moyoni basi ni bora umwambie kweli mapema badala ya kuendelea kumpotezea muda wake.
Naanzaje sasa eeh Mungu maana ataniona msaliti mm na mm sitaki kuyaona machozi yake?
 
Sitoweza kuja kuhimili changamoto zinazohusiana na kifo cha babaangu, kwani aliipenda sana familia yetu, alitusapoti sana masomoni hadi kukubali kukata kiasi fulani cha kipato chake na kutuwekea kwenye akaunti ambayo ndiyo iliyonisaidia kwenda finland kusoma, alitu inspire sana hivyo ni lazima nimkumbuke tuu!
basi let her go soon usiendelee kumpotezea muda
 
Binafsi sikushauri umueleze juu ya hilo jambo maana moja kwa moja mkiachana atajua ndo sababu na inaweza ibua matatizo mengine.

Pia kweli binti hana kosa na mwenye unakiri anakupenda sana na unawish awe mkeo ishu ni kuwa ndoa itakuwa na changamoto maana kila ukimuona unamkumbuka mzee wako utakuwa mwenye hasira na huzuni mara kwa mara wakati yeye hajui kinachoendelea so itakuwa changamoto sidhani kama ndoa inawork out

Nkuulize je ushawah ongea na nduguyo wa karibu yoyote akakushauri???
Bado sijaongea na ndugu yangu yoyote kuhusu hilo jambo
 
Jaribu kumwambia unaemuamini

Kwa upande wangu changamoto nyingine hii ishu si yako pekee ni ya familia sasa hapo ukimuoa na hao ndugu ni mtihani for sure

Tafuta tu njia muachane tena mapema usibuy time bila kumueleza hiyo ishu kabisa
 
Ushauri wangu utakuwa mbaya kdg,,, nahisi kama ibilisi anataka kukupeleka kusiko.......kwanza kabisa ilikuwaje ukampenda then leo uje hapa kuomba ushauri??mshafanya uasherati mpaka shetani anawashangaa.....pili unakubali mwenyewe kuwa na msukumo wa kuachana nae, coz of those bad memories ulizo nazo....ukamuacha then umemrudia....shetani anazidi kukuzogeza karibu na mauaji usiyotegemea.....tatu familia yako inajua nini kilichopo kati ya familia zenu, na mafarakano yataibuka upya utakapomtambulisha kwenu......nne najilazimisha kuamini kuwa unaweza kujikuta ktkt hali ya kulipiza kisasi bila kutegemea....damu ya baba yako inakulilia na itakulilia wewe........jichunge hata usimjaze mimba......na achana nae.....shetani atakuheshimu kwani umemshinda mbinu zake......
 
ushauri wangu achana naye tu hilo jambo litakutesa mno,kwa sbb maisha ni safari ndefu mtakuja gombana kidogo tu tiayari mawazo yako utayaelekeza huko
 
Back
Top Bottom