Baba wa mchumba wangu alimuua baba yangu

Baba wa mchumba wangu alimuua baba yangu

Sikushauri uachane naye lakini hebu usikilize moyo wako. Ingelikuwa ni mimi, basi nisingejiuliza hata mara moja kuhusu kuachana naye, ningemwacha haraka sana kwani hata nikilazimisha kumuoa basi sitakuwa na mafanikio yoyote zaidi ya nyumba kutawaliwa na simanzi. Japokuwa unasema hakuna uhasama wa wazi baina ya familia zenu, lakini upo tena ni mkubwa.
ukitaka kuuona na kuuthibitisha kuwa upo, jaribu kumtambulisha huyo mpenzio kwa familia ndiposa utaona na kuamini. Kwa ninavyojua na kadri ya uelewa wangu, familia yenu itatawaliwa na simanzi na mikosi itokanayo na chozi la babayo. Epuka majonzi kama hayo na chozi hilo kwa kuachana naye na kuitafuta furaha kwingineko.
Cha msingi hata kama unampenda sana tena sana, huna budi kuchukulia kama ametoweka duniani kama alivyotoweka baba yako.

Huu ushauri ni wa msingi sana, kama jamaa anaweza auchukue bila hata ku-edit.
 
Rafiki ni kweli mchumba wako hana kosa ila kumbuka yule ni baba yake hivyo mtakapooana tayari ukaribu utaongozeka na huyo ba'mdogo wake..je utaweza kuvumilia kuwa naye na kufanya siri hasa pale unapojikuta mnakula naye chakula sahani moja. Utaweza kumuangalia usoni na kumfutahia.. Kwa binti hana shida na Huyo ni upendo wa uchumba ni tofauti kabisa na maisha ya ndoa..maana maisha ya ndoa ni harisi... JIPIME
Huu ni mwaka Wa 6 Niko naye kwenye mahusiano
 
  • Thanks
Reactions: lup
Sikushauri uachane naye lakini hebu usikilize moyo wako. Ingelikuwa ni mimi, basi nisingejiuliza hata mara moja kuhusu kuachana naye, ningemwacha haraka sana kwani hata nikilazimisha kumuoa basi sitakuwa na mafanikio yoyote zaidi ya nyumba kutawaliwa na simanzi. Japokuwa unasema hakuna uhasama wa wazi baina ya familia zenu, lakini upo tena ni mkubwa.
ukitaka kuuona na kuuthibitisha kuwa upo, jaribu kumtambulisha huyo mpenzio kwa familia ndiposa utaona na kuamini. Kwa ninavyojua na kadri ya uelewa wangu, familia yenu itatawaliwa na simanzi na mikosi itokanayo na chozi la babayo. Epuka majonzi kama hayo na chozi hilo kwa kuachana naye na kuitafuta furaha kwingineko.
Cha msingi hata kama unampenda sana tena sana, huna budi kuchukulia kama ametoweka duniani kama alivyotoweka baba yako.[/QUOT
Fata huu ushauri, huyo ndo mtu utakaeishi nae milele mpaka kifo kiwatenganishe, halaf una kitu moyoni, dunia haina siri hasa sisi wanawake, ukimueleza huyo mchumba hyo story ataeleza kwao mpaka itafika kwa baba yake mdogo, je unahisi maisha yako yatakuwa salama? baba mdogo atajua kumbe lile jambo halijasahaulika.

Kuhusu uhasama utakuja jitokeza baada ya kuingia ndani ya ndoa, au utakapotangaza ndoa yataibuka mengi, na Je? utakuwa na furaha na Amani ndani ya familia iliyomuua baba yako??

KIUFUPI TAFUTA MWENGINE WA KUMUOA, Kumbuka kizazi chake kitachangia au kuhusika na familia iliyomuua baba yako, watoto wako watamuita Babu mtu aliemuua baba yao...ACHANA NAE.
 
Daaah Ushauri mzuri ni kama nauelewa vile, maana baada yakumaliza tu shahada yangu ya udaktari, nilianza kusomea Sheria lengo likiwa ni kuwasaidia watu wanyonge wanaonyimwa haki, nahofia kiu hii hii nisijekuielekeza kwa wakwe zangu!

Ila nampenda sana huyu bibie sijui tutaachanaje yaani daah!
Huu ushauri ni wa msingi sana, kama jamaa anaweza auchukue bila hata ku-edit.
 
Mikono imwagayo damu imekwisha laaniwa toka enzi za biblia.
ndio maana leo hii kuna watu mambo hayaendi kisa laana walizobeba toka kwenye koo zao. wapo wengine wanaofikia adi hatua ya kukataa majina ya ukoo kwasabb tu wamejitenga na koo zao kwa namna ya kiroho ili kukwepa laana za koo zao.

unless uwe umetuandikia hadith za alfu lela lea ila kama ni kweli huyo binti atakunajisi tuu. hivi hebu jiulize wanao utawapaje historia yako? utathubutu kuwaambia babu yenu aliuwawa na baba wa mama yao?
 
Dah ningekua mimi mtu kamua baba angu tayari huyo ni adui yangu mkubwa uwezi kua na amani ndani ya ndoa yako kama uliweza kumuacha mwaka kwanini? Ushindwe kumuacha saivi?
 
Daaah Ushauri mzuri ni kama nauelewa vile, maana baada yakumaliza tu shahada yangu ya udaktari, nilianza kusomea Sheria lengo likiwa ni kuwasaidia watu wanyonge wanaonyimwa haki, nahofia kiu hii hii nisijekuielekeza kwa wakwe zangu!

Ila nampenda sana huyu bibie sijui tutaachanaje yaani daah!

Mwisho wa siku akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Girlfriend wako hana tatizo lolote..adhabu ya baba ake mdogo usimpe mpenz wako. Kiufupi hana kosa lolote. Shes very innocent
 
Kosa ni la mzaz wake na sio yy,...
Ukimwacha utakuwa unamwonea bure ndg yangu
[HASHTAG]#jifunze[/HASHTAG] kusamehe na kusahau mambo yaliyopita ili usonge mbele kwa amani#
 
Mama yako anajua kuwa huyo binti anatoka ule upande uliosababishA kifo cha mume wake?
 
Uzuri unafahamu aliyekatisha uhai Wa Mzee wako na inawezekana yuko mtaani anakula maisha, ushauri wangu kama unauchungu na Mzee kweli hakikisha unalipiza kisasi kwanza hata yy aliko atatambua kuwa nilizaa jembe, maana roho ya Mzee inasononeka huko aliko kwa nn wanangu hawalipi kisasi, kama ni dhambi zipo tu ila MTU asicheze na maisha ya familia,aliwarudisha nyuma, muliishi kwa kusononeka , visasi vingine tuvimalize tukiwa hapa duniani, mizigo mingine tusimwachie muumba ikiwa tunauwezo Wa kuimaliza, pambana naye aondoke ndo uwaze masuala ya ndoa.

Wadau salaam.
Naitwa Vella ni kijana wa miaka 28 naishi Masaki D'salaam, nina shahada moja ya udaktari wa binadamu na stashahada ya sheria. Mchumba wangu ana shahada ya Biashara na Utawala

Sijao ila nina mchumba wangu tangu tukiwa Advance, hadi leo tunaishi vizuri kwa kuheshimiana, kujaliana na kusikilizana, ananipenda nami nampenda sana tena sana.

Lakini kuna jambo linanisumbua sana moyoni na kunikereketa sana akilini, iko hivi wakuu, Baba yangu alikuwa ni wakili wa kujitegemea, kipindi nikiwa O level baba mdogo wake na mchumba wangu ambaye alikuwa ni mfanya biashara, alimpiga mtu barabarani na kumuumiza vibaya sana, wakati huo baba yangu alikuwa akitoka kazini jioni hivyo alishuhudia tukio zima akiwa kwenye gari yake.
Akaondoka zake kuelekea nyumbani, kesho yake baba ake mdogo na mchumba wake alikuja nyumbani kumwomba baba akamsaidie kusimamia kesi yake yakupiga na kujeruhi mtu aliyempiga jana yake baada ya yule mtu kwenda kumuishataki polisi.

Baba alikataa na kusema yeye ni Wakili ambaye lengo lake ni kusaidia watu kwa haki, akamwambia yupo tayari kutoa ushahidi mahakamani kwa aliyoyaona km raia mwema na sio wakili.

Yule mzee aliitwa mahakamani, lakini akawa anakuja kumwomba mzee wangu kila siku ili akubali kwenda kumsaidia kesi yake, Baba alikuja kukubali akaenda mahakamani, kadiri siku zilivyozidi kwenda baba alikuwa akirudi nyumbani akiwa analalamika kuwa mteja wake hamlipi malipo yake, waliendelea hivyo lakini karibia kufikia mwisho wa kesi mzee wetu alirudi nyumbani na kukiri mazingira ya mtuhumiwa kutenda lile kosa hayampi mteja wake ahaueni yakushinda kesi zaidi ya kushindwa.

Basi mtuhumiwa pia naye alishaanza kunusa harufu ya kushindwa kesi, hivyo alichokifanya, alimwita baba yangu nyumbani kwake, wakala chakula, mzee akarudi nyumbani alivyopewa chakula aliomba asile na badala yake wapewe watoto maana yeye ameshiba kwani alisema alikula kwa huyo mzee mwenye kesi.

Mzee wangu kesho yake alifajiri aliamka akiwa anaumwa sana, hakuweza kuongea, ila alikuwa akigalagala kwa maumivu, na hatimae kufariki.

Niliskia familia yetu (baadhi) wakihusanisha kifo cha baba yangu na mipango miovu ya mteja wake. Kwani baada tu ya kifo cha baba yangu yule mzee kesho yake alitorokea mjini Arusha, na wala hata baada yakurudi hakuja nyumbani kutoa pole, licha ya kwamba alikuwa ni jirani yetu wa mtaa moja.

Turudi kwa Mchumba wangu, Mchumba wangu hili jambo hakuwahi kulifahamu kwani hata habari za kifo cha baba yangu nilimjuza mimi majuzi tuu, hajui chochote kuhusu kesi ya babaake mdogo na baba yangu, ingawa mimi nafahamu.

Huyu binti nampenda sana, mara kadhaa tumekuwa tukijadili kuhusu kuvalishana pete ya uchumban lakini moyo wangu unakosa utayari. Mwaka mmoja na nusu niliwahi kumwacha kwa siri baada yakuwa na msongo wa mawazo kuhusiana na mambo ya baba yake mdogo na kifo cha mzee wangu, ila aliendelea kuwa karibu sana na mimi hadi mwaka juzi tukarudiana tena japo sikumwambia sababu za kumwacha, zaidi ya kumwambia "sikukuacha ni ukali wa maisha na ubusy wa masomo" kwani wakati yeye akiwa chuo kikuu cha D'salaam mimi nilikuwa masomoni nchini Finland.

Hivyo wadau naombeni ushauri, je huyu binti niachane naye kimya kimya au nimpe mkanda mzima wa kifo cha mzee wangu na jinsi babaake mdogo alivyohusika?

Au niendelee naye tu kisha tuoane? Je familia yangu haitajiskia vibaya? (Japo hakuna uhasama wowote wa wazi kati ya hizo familia mbili)

Nifanyaje wadau wangu, Naombeni Mawazo Yenu.
 
Sikushauri kabisa watu wana sema et mchumba hana kosa lakin familia yake ndio iliyotenda hilo kosa na unapooa unaunganishwa na uko mzima wa hiyo familia, sasa kaa saiz tu ukimuona unapata huzuni na pia umefanya majaribio kadhaa kutaka kumuacha hiyo ni ishara tosha kuwa hata wewe unaona uzito juu ya hilo dhambi ya kuua hufuatilia usijekuta na ww unauawa, achana naye ndugu yangu
 
Hii sio La Revancha hii ?? Msela kachakachua.....

Ila ajiangalie tu asije akaitwa central kutoa maelezo. We mwache anogewe na Chit Chat sijui MMU. Kuna Jela !!!
Sijawahi kuangalia TBC zaidi yakuona kwenye list ya king'amuzi changu, nina zaidi ya miaka 5 sijathubutu kuangalia TBC, na hiyo movie mie siijui, km imefanana am sorry but that's how it is
 
Girlfriend wako hana tatizo lolote..adhabu ya baba ake mdogo usimpe mpenz wako. Kiufupi hana kosa lolote. Shes very innocent
Haya mawazo napenda kuyaskia sana maana yananifariji, ingawa pia napenda ukweli mchungu utakao niokoa
 
Kosa ni la mzaz wake na sio yy,...
Ukimwacha utakuwa unamwonea bure ndg yangu
[HASHTAG]#jifunze[/HASHTAG] kusamehe na kusahau mambo yaliyopita ili usonge mbele kwa amani#
Mimi sina kinyongo na huyu baba, na familia ya binti wananifahamu na tunaheshimiana ila mambo mawili yananiumiza, nikifikiria mapenzi ya babaangu kwa familia yetu na namna alivyokufa naumia mno, pili mpenzi wangu huyo nampenda sana nae vivyo hivyo nashindwa na nakosa sababu ya kumwacha!
 
Mama yako anajua kuwa huyo binti anatoka ule upande uliosababishA kifo cha mume wake?
Huyu binti aliwahi kunitembelea nyumbani kwetu kipindi nikiwa likizo na alikuja na gari ya mama ake, mama aliifahamu ile gari, akaniuliza huyu rafiki yako ni wawapi mbona simfahamu lakini gari imefanana na ya mama nanilia? Nikapotezea sikumjibu, nilihofia asijue mapema kabla hatujajipanga na huyo binti kuhusu maswala ya uchumba, km mama angu anafahamu sio kupitia mimi bali udadisi wake binafsi, ingawa kwa upande wa binti wazazi na ndugu zake wanafahamu kuhusu mahusiano yetu!
 
Back
Top Bottom