Wadau salaam,
Ni kijana wa miaka 28 naishi Masaki D'salaam, nina shahada moja ya udaktari wa binadamu na stashahada ya sheria. Mchumba wangu ana shahada ya Biashara na Utawala.
Sijao ila nina mchumba wangu tangu tukiwa Advance, hadi leo tunaishi vizuri kwa kuheshimiana, kujaliana na kusikilizana, ananipenda nami nampenda sana tena sana.
Lakini kuna jambo linanisumbua sana moyoni na kunikereketa sana akilini, iko hivi wakuu, Baba yangu alikuwa ni wakili wa kujitegemea, kipindi nikiwa O level baba mdogo wake na mchumba wangu ambaye alikuwa ni mfanya biashara, alimpiga mtu barabarani na kumuumiza vibaya sana, wakati huo baba yangu alikuwa akitoka kazini jioni hivyo alishuhudia tukio zima akiwa kwenye gari yake.
Akaondoka zake kuelekea nyumbani, kesho yake baba ake mdogo na mchumba wake alikuja nyumbani kumwomba baba akamsaidie kusimamia kesi yake yakupiga na kujeruhi mtu aliyempiga jana yake baada ya yule mtu kwenda kumshataki polisi.
Baba alikataa na kusema yeye ni Wakili ambaye lengo lake ni kusaidia watu kwa haki, akamwambia yupo tayari kutoa ushahidi mahakamani kwa aliyoyaona kama raia mwema na sio wakili.
Yule mzee aliitwa mahakamani, lakini akawa anakuja kumwomba mzee wangu kila siku ili akubali kwenda kumsaidia kesi yake, Baba alikuja kukubali akaenda mahakamani, kadiri siku zilivyozidi kwenda baba alikuwa akirudi nyumbani akiwa analalamika kuwa mteja wake hamlipi malipo yake, waliendelea hivyo lakini karibia kufikia mwisho wa kesi mzee wetu alirudi nyumbani na kukiri mazingira ya mtuhumiwa kutenda lile kosa hayampi mteja wake ahaueni ya kushinda kesi zaidi ya kushindwa.
Basi mtuhumiwa pia naye alishaanza kunusa harufu ya kushindwa kesi, hivyo alichokifanya, alimwita baba yangu nyumbani kwake, wakala chakula, mzee akarudi nyumbani alivyopewa chakula aliomba asile na badala yake wapewe watoto maana yeye ameshiba kwani alisema alikula kwa huyo mzee mwenye kesi.
Mzee wangu kesho yake alifajiri aliamka akiwa anaumwa sana, hakuweza kuongea, ila alikuwa akigalagala kwa maumivu, na hatimae kufariki.
Nilisikia familia yetu (baadhi) wakihusanisha kifo cha baba yangu na mipango miovu ya mteja wake. Kwani baada tu ya kifo cha baba yangu yule mzee kesho yake alitorokea mjini Arusha, na wala hata baada ya kurudi hakuja nyumbani kutoa pole, licha ya kwamba alikuwa ni jirani yetu wa mtaa moja.
Turudi kwa Mchumba wangu, Mchumba wangu hili jambo hakuwahi kulifahamu kwani hata habari za kifo cha baba yangu nilimjuza mimi majuzi tuu, hajui chochote kuhusu kesi ya babaake mdogo na baba yangu, ingawa mimi nafahamu.
Huyu binti nampenda sana, mara kadhaa tumekuwa tukijadili kuhusu kuvalishana pete ya uchumba lakini moyo wangu unakosa utayari. Mwaka mmoja na nusu niliwahi kumwacha kwa siri baada yakuwa na msongo wa mawazo kuhusiana na mambo ya baba yake mdogo na kifo cha mzee wangu, ila aliendelea kuwa karibu sana na mimi hadi mwaka juzi tukarudiana tena japo sikumwambia sababu za kumwacha, zaidi ya kumwambia "sikukuacha ni ukali wa maisha na ubusy wa masomo" kwani wakati yeye akiwa chuo kikuu cha D'salaam mimi nilikuwa masomoni nchini Finland.
Hivyo wadau naombeni ushauri, je huyu binti niachane naye kimya kimya au nimpe mkanda mzima wa kifo cha mzee wangu na jinsi baba yake mdogo alivyohusika?
Au niendelee naye tu kisha tuoane? Je familia yangu haitajiskia vibaya? (Japo hakuna uhasama wowote wa wazi kati ya hizo familia mbili)
Nifanyaje wadau wangu, naombeni mawazo yenu.