Baba wa mchumba wangu alimuua baba yangu

Kama nikweli unavyosema Hata ulikua huitaji ushauri mkuu ungemalizana nae long time ago,hata ukimwambia hujui utaleta vita BARIDI huyo msichana wako ataanza kulia nakusema kua ni sababu ya Baba mdogo amemua Baba wa mchumba wangu ndio mana amenikata sasa unataka na huyo Baba mdogo akufukuzie na wewe sababau ukweli umeshaujua kua amemua mzee wako? Mkuu sioni sababu ya kutafuta shari kama salama ipo,jiepushe mtu akiwa muuwaji kila anapokaa anawaza huuwa,am sure unataka kuacha jinala mzee wako liendelee kuwepo na kutimiza ndoto zake achana na huyo mdada wala usiwe sababu ya kumpa wewe hutokua wa kwanza kumuwacha mwanamke wala hutokua wa mwisho..
 
Uzuri unafahamu aliyekatisha uhai Wa Mzee wako na inawezekana yuko mtaani anakula maisha, ushauri wangu kama unauchungu na Mzee kweli hakikisha unalipiza kisasi kwanza hata yy aliko atatambua kuwa nilizaa jembe, maana roho ya Mzee inasononeka huko aliko kwa nn wanangu hawalipi kisasi, kama ni dhambi zipo tu ila MTU asicheze na maisha ya familia,aliwarudisha nyuma, muliishi kwa kusononeka , visasi vingine tuvimalize tukiwa hapa duniani, mizigo mingine tusimwachie muumba ikiwa tunauwezo Wa kuimaliza, pambana naye aondoke ndo uwaze masuala ya ndoa.
Hapana kisasi ni cha Mwenyezi Mungu, mimi siwezi kuua, na unaona watu wengi huku wanashauri niachane na huyo binti kwasababu tu mmoja wa mwanafamilia ameua?

Sasa unataka na mimi uzao wangu uje utengwe na kubaguliwa?
 
Sikushauri kabisa watu wana sema et mchumba hana kosa lakin familia yake ndio iliyotenda hilo kosa na unapooa unaunganishwa na uko mzima wa hiyo familia, sasa kaa saiz tu ukimuona unapata huzuni na pia umefanya majaribio kadhaa kutaka kumuacha hiyo ni ishara tosha kuwa hata wewe unaona uzito juu ya hilo dhambi ya kuua hufuatilia usijekuta na ww unauawa, achana naye ndugu yangu
Allah Akbar! We shall overcome!
 
Huyo baba mdogo wako atakuua na wewe, hiyo familia wazee wa binti wanajua lililotokea.

Kaa kimya usimwambie tafuta msichana mwingine, huwezi kuwa na amani naye.

Imagine siku ya harusi na sherehe zingine uncle wake na wazazi wake wana dance kwa furaha na wewe unamkumbuka baba yako hapo ulipo.

Kaa kimya nenda zake, omba kwa Mungu kifo cha baba yako aliyemuua apatwe na majuto ukiea bado upo hai kuona haki inatendeka.

Pole sana, achana na hiyo familia kama unajipenda na unaoenda familia yenu.
 
Kama nikweli unavyosema Hata ulikua huitaji ushauri mkuu ungemalizana nae long time ago,hata ukimwambia hujui utaleta vita BARIDI huyo msichana wako ataanza kulia nakusema kua ni sababu ya Baba mdogo amemua Baba wa mchumba wangu ndio mana amenikata sasa unataka na huyo Baba mdogo akufukuzie na wewe sababau ukweli umeshaujua kua amemua mzee wako? Mkuu sioni sababu ya kutafuta shari kama salama ipo,jiepushe mtu akiwa muuwaji kila anapokaa anawaza huuwa,am sure unataka kuacha jinala mzee wako liendelee kuwepo na kutimiza ndoto zake achana na huyo mdada wala usiwe sababu ya kumpa wewe hutokua wa kwanza kumuwacha mwanamke wala hutokua wa mwisho..
Au nimfungulie mashataka? Maana haki ndio iliyonisukuma kusomea Sheria?
 
Utakuwa na changamoto nyingi kwenye maisha yako ukiamua kumwuoa huyu msichana. Hutakubalika kwao, nafsi yako itateseka sana kwani utakuwa unaona umemdhulumu mzazi wako ambaye ni marehemu. Umweleze msichana kwa nini unafikiri ndoa yenu haitawezekana.
Umsamehe baba mdogo songa mbele.
 
Au nimfungulie mashataka? Maana haki ndio iliyonisukuma kusomea Sheria?
Mwenyezi Mungu anatosha Kushtakia Mkuu yeye ndio anaijua kweli kwa yote yate yalio tokea na mfanyaji,najua sio rahisi kumuona Adui yako yuko uhuru lakini still huna kithibitisho chakutosha lakini utakapo mpa mwenyezi mungu kilio chako
niamini hatokuangusha,huko kwengine nikujitafutia uwadui kwani hujui nani ni mwema wako na dunia ya leo baadhi ya watu wengi imani imewatoka wanauza utu wao kwa kitu kidogo tuu,ningekua wewe Ningelia kwa mungu usiku na mchana
anilipie na humtaji mtu kua ni fulani la hashaa,kwanza ujue kua ikiwa mwenyezi mungu hajataka lolote likufike basi halikufiki
omba kwa mwenyezi mungu ikiwa ni kwa utukufu wako mwenyezi mungu basi nipe subra niweze kuhimili na umpe makazi mema peponi mja wako,ikiwa ni jengine lolote basi mwenyezi mungu wewe ndio hakimu wa haki usie lala wala usie sinzia na unaposema kua basi hua ...
 
kifo cha baba yako hakitaleta amani kwenye ndoa yenu labda uamue kusamehe wewe mwenyewe na usamehe kweli.. ila sababu baba yako kifo chake kiliumiza wengi hao wengine watageuka chachu kwenye ndoa yenu kwa namna moja au nyingine .. ushauri wangu mueleze ukweli huyo binti na mwache aendelee na maisha yake sababu hata ndugu zako kufanya utaratibu wa ndoa italeta mushkeli kidogo na kuleta mtafaruku
 
Achana nae laana hiyo inazunguka kwenye ukoo wao.Hujui baba yako alitamka maneno gani kabla mauti hayajamfika.
 
kifo cha baba yako hakitaleta amani kwenye ndoa yenu labda uamue kusamehe wewe mwenyewe na usamehe kweli.. ila sababu baba yako kifo chake kiliumiza wengi hao wengine watageuka chachu kwenye ndoa yenu kwa namna moja au nyingine .. ushauri wangu mueleze ukweli huyo binti na mwache aendelee na maisha yake sababu hata ndugu zako kufanya utaratibu wa ndoa italeta mushkeli kidogo na kuleta mtafaruku
Kwa upeo wangu, sioni kama jamaa yupo tayari kusamehe na kusahau. Naogopa na huwa nikiogopa basi jambo la kuogofya huenda likawakumba. Kwanza, ndugu wote watampinga na akilazimisha kuoa basi atatengwa kitu ambacho si kizuri kwake. Pili, mwenyewe anakiri kuwa anakumbuka mara kwa mara namna baba yake alivyokufa na sidhani kama kumbukumbu hizo zitafutika kichwani mwake kamwe.
Aepuke tu kujihusisha na binti huyo. Kama mapenzi au ndoa ni furaha, basi hayo au ndoa yake hiyo haiwezi na haitakuja kuwa na furaha daima.
 
kabisa ana abadilishe mtizamo sasa
 
Baba yake mdogo bado yu hai? Kuna uwezekano utakapomweleza huyo binti hayo unayofikiri ndio yaliyomsibu baba yako, basi naye ataamua kuutafuta ukweli, ambao utaleta uhasama, pengine kupelekea kuhatarisha maisha yako. Ikiwezekana achana naye, bila ya kumpa hiyo sababu.
 
Mwenyezi Mungu anatosha Kushtakia Mkuu yeye ndio anaijua kweli kwa yote yate yalio tokea na mfanyaji,najua sio rahisi kumuona Adui yako yuko uhuru lakini still huna kithibitisho chakutosha lakini utakapo mpa mwenyezi mungu kilio chako
niamini hatokuangusha,huko kwengine nikujitafutia uwadui kwani hujui nani ni mwema wako na dunia ya leo baadhi ya watu wengi imani imewatoka wanauza utu wao kwa kitu kidogo tuu,ningekua wewe Ningelia kwa mungu usiku na mchana
anilipie na humtaji mtu kua ni fulani la hashaa,kwanza ujue kua ikiwa mwenyezi mungu hajataka lolote likufike basi halikufiki
omba kwa mwenyezi mungu ikiwa ni kwa utukufu wako mwenyezi mungu basi nipe subra niweze kuhimili na umpe makazi mema peponi mja wako,ikiwa ni jengine lolote basi mwenyezi mungu wewe ndio hakimu wa haki usie lala wala usie sinzia na unaposema kua basi hua ...
Mkuu nashukuru kwa busara zako
 
Back
Top Bottom