Kiukweli nakubaliana na mtu anayesema mama zetu wanapenda sana kuvutia kamba upande wao
Inreality hakuna mtu atakae farakana na mtu mwingine alafu aje akusimulie kwa namna ambayo itaonyesha yeye ana kosa...lazima aelezee kwa namna ambayo mwenzie ndio mwenye kosa
Kwa sasa nina wazazi wote ila kwa situation inayoendelea nazidi kumshkuru mungu sipo karibu nao maana kwa jinsi mother anavyonielezea anayoyafanya mzee nahisi ningeshaingilia kati kitu ambacho sio kizuri kuingilia ugomvi wa wazazi...
Kwa sasa bado nasoma ila kila nikipata likizo nikaenda home cha kwanza ninachokutana nacho kwa maza ni mabaya yote anayoyafanya mzee na anachotaka ni mimi nichukue hatua kumwambia mzee anachokifanya sio kizuri kitu ambacho ni kigumu mimi kukifanya kama mtoto kwa sababu pia sina uhakika na anayosema maza kama kweli ni ya kweli
Unakuta maza analalamika sana kuusu mzee kuwa amjali kwa kua anaumwa au atoi matumizi ...kwa swala la matumizi napingana na maza kwa kuwa mara nyingi mzee anakua hana ela ila yeye maza anashindwa kulitambua ilo....
Kwa hali ii nimejikuta nabaki dillema nifanye nini...mother anataka nimface mzee nimchane live anayoyafanya sio mazuri wakati mimi sijaprove kama kweli mzee anayafanya na ata kama kweli anayafanya siwezi kumface mimi kama maza anavyotaka maana ni kama nitakua nawaachanisha kabisa
Kwa ili limenifanya nisiwaamini sana mama zetu kwa kile wanachotwambia kuusu baba zetu
Kwa wanaowachukia baba zao nadhani ni swala la kutokuchambua yap ya kuchukua na yap ya kuyapotezea kutoka kwa mather
Kwa ufupi tu ninachotaka kushauri kabla ujamchukia mzazi mmoja jaribu kufatilua kwanza pande zote kama kweli yanayosemwa ni kweli
Sent using
Jamii Forums mobile app