Watu wenye matatizo km yako hata kauli zenu huwa zinafanana utadhani huwa mnaambizana. Pole sana mkuu. Lkn me nataka nikuambie na kukupa ushauri ambao si lazima uuchukue. Pamoja na kwamba sijapata maelezo ya upande wa Baba yako lkn ukweli hicho unachosema kuhusu weakness za Baba yako ni 15%tu.
Hizo sababu zingine unazotoa unatuonyesha tu kwa hisia kuwa Baba yako alikuwa mbaya sana..na kwa bahati mbaya sana mpaka leo unaamini hivyo na unaposema jambo hilo kwa watu na wakakuonea huruma ww ndo unapata nafuu.
Hasira zako zote zinatokana na sumu aliyokulisha mama yako ambaye ndo alikulea na kwa sababu mlikuwa na shida sana wakati huo,ile sumu iliyokuwa inapandwa na mama yako ilikuwa rahisi tu kukuingia na kusema kweli imekuumiza mno!
Me nakuhakikishia mama yako pamoja na kukulea,lkn ndo alikuwa mbaya sana aliyesababisha hadi Baba yako awatelekeze. Me nakushauri ufanye jambo moja kubwa sana,msamehe Baba yako na muoneshe upendo utakuja kusikia vitu ambavyo hukutarajia kuhusu mama yako. Wanaume huwa ni wastaarabu sana huwa wanajizuia mambo mengi sana kuyasema kwa watoto wao.
Usiangalie sana mafanikio uliyoyapata,hayo mafanikio yamepatikana kutokana na hilo tukio. Pengine ungekuwa unapata kila kitu kwa Baba na mama ungebweteka na usingefika hapo ulipo leo. Hayo mapungufu ya wazazi wako ndo yaliyokujenga na kukupa hasira ya kupambana. Natamani kuandika sana,lkn Acha niishie hapa. Lkn unahitaji ushauri mkuu,hicho kitu kitakutesa maisha yako yote. Na kimsingi ww ndo unaumia kuliko hata Baba yako.
Sent using
Jamii Forums mobile app