Baba mzazi wa Askari Polisi anayedaiwa kujinyonga Mtwara adai kutoridhishwa na taarifa ya mwanae kujiua

Yaani haya majibu ya polisi yananifanya nielewe polisi wanahisi raia akili hatuna.Babake marehemu kasema kawaida tukio la kujinyonga ilibidi apigwe picha au ndugu aitwe kushuhudia .lkn yote hayo hayakufanyika.Na bado tuwaamini marehemu alijinyonga tena mbaya zaidi na tambara la deki?Tena akiwa mahabusu. GetHilo tambara la deki lenye urefu wa kutosha kujinyonga na uimara wa kubeba mtu mzima let say kg 70 ni la aina gani?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Sio wanahisi raia hawana akili bali wao ndio hawana akili
 
Penye haki utalindwa still bado sio final zipo mamlaka zinazoshughulika na uonevu wa viongozi.Kama imesimama kwenye haki unasikilizwa na haki yako hazipotei.
Nadhani wengi sababu ya kutokujua sheria za Kazi na haki zao kazini.
Unayo haki ya kugomea amri binafsi ya kiongozi wako kama Ina kiuka maadili.
Na unategemea atakuacha salama wakatiushajua siri?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
"Ndugu yetu aliitwa wakati marehemu alishapelekwa hospitali ya Ligula na akaoneshwa michubuko akielezwa ni ya kamba, kisha akaambiwa ni ya tambara la deki, hivi mahabusu ya jeshi kuna tambara la deki?" Gaitan Mahembe, baba mzazi wa Greyson Mahembe, askari anayedaiwa kujinyonga https://t.co/1ezV2Sk4KQ
Hilo halikuwa tambara la deki bali tambara la kamba maana michubuko ilikuwa ya kamba na nijuavyo kamba haiwezi kuwa tambara la deki

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Akiongea na Azam News, Baba mzazi wa askari aliyejinyonga anasema hajaridhishwa na taarifa za kifo cha mwanae!

Anasema alipigiwa simu na kuambiwa mwanao tumpeleke akazikwe wapi? Akawaambia mleteni nyumbani kwangu Tabata, Dar Ea Salaam...
Jeshi la polisi lifumuliwe upya, kuna uozo mwingi sana wa mauaji, utekaji na utesaji wa raia, weledi wao ni finyu na mbinu zao ni za kitoto sana

Sifa chafu nyingi, hakuna mwenye imani na jeshi letu la polisi, hii ni aibu na hatari kwa Taifa
 
ASKARI ALIYESHTAKIWA KWA MAUAJI AJINYONGA MAHABUSU KWA TAMBALA LA KUDEKIA...
Ukiua kwa upanga utauawa kwa upanga, inashangaza kwamba askari anashindwa kusimamia ethics za kazi yake anakubali kutumwa kuua raia wasio na hatia....halafu leo tunaambiwa amejiua kwa tambara deki

Kila mtu abebe msalaba wake, na malipo ni hapa hapa duniani
 
Na unategemea atakuacha salama wakatiushajua siri?

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Hata wasipokuacha salama Siri haifichi.
Watu wa ulimwengu usioonekana wao uona KILA kitu na ndio uwapa Siri watu wa ulimwengu unaonekana.
Ukishaua mtu umewasha taa nyekundu utamulikwa maisha yote,hata familia uliyoua haitokubali lzm ilipe kisasi.
 
Akiongea na Azam News, Baba mzazi wa askari aliyejinyonga anasema hajaridhishwa na taarifa za kifo cha mwanae!

Anasema alipigiwa simu na kuambiwa mwanao tumpeleke akazikwe wapi? Akawaambia mleteni nyumbani kwangu Tabata, Dar Ea Salaam...
Kwani mazingira ya kifo chake kinaonyesha alijitundika au pio lupango hawewezi tolea maelezo juu ya hilo ndiyo maana wameshikilia hilo la kujiua
 
Ukifanya kosa,unategemea ufanye kosa ili ukwepe makosa?Haipo hivyo,labda utokee utendaji wa makosa kukwepesha wahalifu kukutwa na makosa.
Criminal law principle: kwenye kesi za accessories/accomplices: mtenda kosa mkuu yaani mshitakiwa mkuu asipopatikana na hatia kwa sababu iwayo yeyote, wale watuhumiwa wengine wanakuwa hawana hatia kwa sababu ikiwa mashtaka ni kula njama na kuua, halafu mtendaji mkuu hajapatikana na hatia ya kuua, basi haiwezekani uwakute washiriki na hatia ya kosa ambalo halijathibiyishwa.

Rejea kesi ya akina Zombe. Saadi ambaye alifyatua risasi alifariki kabla ya hukumu. Na zombe akaponea hapo maana mshirika wake hakupatikana na hatia
 
Unaelezaje watuhumiwa kuachiwa,halafu kudakwa upya nje ya mahakama ili mbilinge ianze upya?
 
Back
Top Bottom