Baba mtarajiwa, nini natakiwa kufanya?

Baba mtarajiwa, nini natakiwa kufanya?

Bima tumia yako ndio heshima ya kiumeni mtoto anatumia ubini wako kwa nini akatiwe bima ya mama? Pia hata kama mama yake ana uwezo wa kununua ndege gharama zote za kutunza mtoto anatoa baba. Utagongewa mchana kweupe kama una akili utakuwa umenielewa
Sawa mkuu.

Ila nakukumbusha, sio mke wangu na wala hatuna mpango wa kuoana, ni rafiki tu tumeamua kuzaa
 
cha kufanya tafuta dem mwingine mpige mimba
 
Mleta mada hauko serious kimaisha na unachokifanya ni kucheza bahati nasibu.

Kwa mfano, unawezaje kuzaa na girlfriend na kuona ufahari?
Unawezaje kumlea vyema mtoto ambaye haishi naye?
Unajisikiaje mtoto wako kulelewa na single mother?

Kuweza kukusaidia tu hapa, malezi bora ya mtoto yanategemea mambo makuu matatu;
1. Uhusiano kindoa wa wazazi.
2. Misingi ya kiimani na kijamii ya wazazi
3. Ukaribu wa wazazi kwa mtoto
Mkuu umeongea jambo la msingi sana.
 
Wakuu habari za wakati huu.

Girl Friend wangu anatarajia kujifungua ndani ya mwezi mmoja hivi ama zaidi kidogo.

Sasa kama baba mtarajiwa ni kitu gani ama maandalizi gani natakiwa kufanya kabla na baada ya kujifungua.

Girl friend wangu anaishi kwake na mimi naishi kwangu, yuko financially stable ila I want to support her kwa vitu vyote vinavyohitajika.

Naomba kujua nahitaji kuandaa nini na nini ili niweze kupanga Budget yake mapema.

Ahsante.
Kajitambulishe kwao, wakufahamu na utoe kishika uchumba uanze maandalizi ya ndoa, hatutaki single mamas wameshajaa jaribu kupunguza matatizo
 
Sawa mkuu.

Ila nakukumbusha, sio mke wangu na wala hatuna mpango wa kuoana, ni rafiki tu tumeamua kuzaa
Hata kama hapo kuna baba na mama, mahitaji yanatolewa na baba. Mtoto haujui urafiki wenu atajua mama na baba na katika kumkuza lazima ajue kuwa baba ndiye provider otherwise mtatuletea kina Aggrey wapya au Marioo
 
Mzee lea mtoto wako...

Hudumia familia yako kwa uwezo wako wote...
 
Girl friend wangu anaishi kwake na mimi naishi kwangu, yuko financially stable ila I want to support her kwa vitu vyote vinavyohitajika.
Tatzo limeanzia hapa ndio maana had anakaribia kujifungua ujui nn unatakiwa kufanya.

Andaa gharama zote na vifaa vinavyo itajika kwenda navyo hospital wakat wa kujifungua, tengeneza mazingira atakayofikia baada ya kutoka hospital na mtoto, andaa nguo za mtoto, vifaa vya usafi vya mtoto(sehemu ya kumuoshea, mafuta ya kupaka, poda, nk), chakula cha mzazi, nk
Ila kubwa zaidi ni pamoja na mda wako kuwa karibu na mzazi mwenzio wakati wote wa malezi
 
Back
Top Bottom