Baba mkwe, mahari hii imenishinda

Bro angemtia na mimba kabisa wangempa bure kabisa. Waluguru muda mwingine siwaelew watu wenyewe full utegemezi ila bado masharti kibao
 
Chief huyo dem ulimkuta Bikra?yeye mwenyewe ana utajiri sana ama?hyo 280000 uliyotoa waambie ndio mahali..hawataki waambie wakae na lidemu lao
 
Bado kidogo nikushauri uongee na huyo mama watoto kuhusu hio mil 5 ili awashawishi wazazi wakupunguzie..
ila kila nikiikumbuka laki mbili na themanini ya chakula uliyolipishwa naskia uchungu Chief..

tupa kule hio familia takataka.
King ndio kashasema

na mimi nilitaka kushauri hivyo

ila kulipishwa pesa ya maandalizi ya event yao 280k

Asee ki ufupi hiyo sio familia

Niamini nakwambia hata ukisema ufumbe macho ulipe yote 5M

mbele utakutana na mi cost mengine na watakufanya kama DUKA lao

Funga macho TEMANA nao....

Mtoto akizaliwa mtunze kwa gharama zote Tena in a CLASSIC WAY

ili waone sio kwamba huna hela,ila ni HAUNA hela za kuwapa wajinga wajinga

kwa mambo yakijinga jinga.

Subiri mtoto azaliwe,Hudumia mwanao hadi wahisi n mtoto wa JAY Z
 
Haki ya nani washamtengenezea usingo mother mtoto wao! Mkuu Ml 5 nenda nayo Kisemvule Obey Village kiwanja tsh 1,400,000/= au 2,000,000/= ....nunua kiwanja... 1000,000/= nunua tofari za vyumba viwili...inayobaki anza ujenzi hata vyumba viwili hamia kama hutaki kukaa huko pangisha..... papuchi ushaila sana na ikitaka itakuja kwako mwenyewe. Nisije ona unanyanyua kwato zako unaenda Moshi tenaaaaa.
 
Kabisa mkuu..... Halafu ukute driving motive yao ni wivu na tamaa ya fedha (nikisema wivu nina maana pana sana)
 
Ukweli sisi vijana tunateseka sana, wazazi nao wametia ngumu sana, hasa haka kamtindo ka kukomoana kuanzia millioni, niliwahi kujaribu nikiwa na kalaki 8 walidai ni pesa ya kununulia kiatu cha sikukuu, aisee niligive up, mpaka sasa siwezi kuwa na mahusiano tena, naona Dunia inaenda kasi sana
 
Mkuu hawa watakua Wahaya tu
 
Waambie utawalipa kidogo kidogo wakikubali ndo mazima iyoo
 
Umefanya maamuzi ya kiume hongera bro
 
Ndoa za kihivyo nitakuwa nazisindikiza kwa macho tu hadi naingia kaburini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…