Baba mdogo anakula kitimoto hadharani

Baba mdogo anakula kitimoto hadharani

Mawardat

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2021
Posts
25,858
Reaction score
136,485
Wassalaam.

Ni hivi upande wa baba wapo mseto lkn %95 ni wakristo, %5 ndiyo siye,

Baba mdogo kaja nyumbani kutusalimia na ana wiki sasa,

Shida ba mdogo anapenda kula kitimoto balaa,

Yaani chai yake ni kitimoto na pepsi,

Shida anakuja nacho ndani, kama leo kamtuma boda amletee na muda boda kaja ba mdogo anaoga na akaniambia nikampokelee

Na kumuambia asilete ndani nitaanzaje??

Hawezi kuona tunamnyanyapaa??

Au hatumtaki??

Je anafanya kusudi?? maana anaelewa kuwa hatutumii,

Naombeni ushauri nitumie njia gani kumfikishia kuwa hatupendezewi na hii tabia?

NB. Mama hajui maana si mtu wa nyumbani.

MREJESHO..............................
______________________________

mchana huu,nimemwambia ba mdogo

Si unajua imani tumetofautiana,akasema ndiyo,

Nikamwambia hivyo hiyo nyama unayokujaga nayo siye hatutumi,uwage unakula huko mabandanii

Akasema sorry kwanini usingenishtua? maana nilijisahau mwanangu,NISAMEHE,

Nimemwambia haina shida baba kuwa na amani,
 
Was salaam.

Ni hivi upande wa baba wapo mseto lkn %95 ni wakristo, %5 ndiyo siye,

Baba mdogo kaja nyumbani kutusalimia na ana wiki sasa,

Shida ba mdogo anapenda kula kitimoto balaa,

Yaani chai yake ni kitimoto na pepsi,

Shida anakuja nacho ndani, kama leo kamtuma boda amletee na muda boda kaja ba mdogo anaoga na akaniambia nikampokelee

Na kumuambia asilete ndani nitaanzaje??

Hawezi kuona tunamnyanyapaa??

Au hatumtaki??

Je anafanya kusudi?? maana anaelewa kuwa hatutumii,

Naombeni ushauri nitumie njia gani kumfikishia kuwa hatupendezewi na hii tabia?

NB.mama hajui maana si mtu wa nyumbani.
kwani wewe ni Muislam au haupendi tu Kitimoto?
Namaanisha kama wewe ni Muislam, muite Pembeni umueleze kuwa familia yako haitumii na kwa imani yako haifai kuleta hapo nyumbani hivyo unamuomba asifanye hivyo.
Akileta tena, itakuwa ni dharau ya hali ya juu nyumbani kwa mtu hivyo mtengenezee mazingira ya kuondoka chap!
 
Me muislam,

nashukuru kwa ushauri.
 
Back
Top Bottom