BABA MCHAWI:Mke wangu anataka nimpeleke Nyumbani

BABA MCHAWI:Mke wangu anataka nimpeleke Nyumbani

Nigendako

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2017
Posts
23,296
Reaction score
122,445
Habari wana JF

Husika na kichwa cha habari hapo juu,, ningependa nieleze japo kwa uchache juu ya historia ya maisha yangu, familia yangu pamoja na hali inayoendelea hv sasa.

Mimi in kijana, umri wangu ni 28,na nina familia yaani na mke pamoja na watoto wawili(mapacha wa kike),,,
Mke wangu ni mwenyeji wa Arusha,ila tulikutana miaka mitano iliyopita, tulikutana Mwanza kwenye harakati za kutafuta maisha basi bhana tukapendana na tukaanzisha uhusiano baadae tukaanza kuishi pamoja yaani mume na mke,, tuliishi maisha hayo ndani ya mwaka mmoja,, Yule binti akasema inabidi twende Arusha nyumbani kwao wanifahamu, kipindi hcho chote naishi na Yule binti sikuwahi kumpeleka nyumbani wala hata kuongea na ndugu zangu hata mmoja tofauti na yy kila alipokuwa anataka kuwafahamu ndugu zangu au hata kuongea nao nilimpa sababu nyingi sana zingine hata nilimuongopea,,, Kwani ukweli nlikuwa naufahamu mimi!

Stori yangu kwann sikutaka binti huyu hapafahamu nyumbani!!

Nimezaliwa miaka 28 iliyopita huko Kahama,, kwenye familia yetu tulizaliwa watoto watatu,, yaani wa kike, nafata mm, halafu wa mwsho ni wa kiumu pia,, Baba yetu ni msukuma ila mama alikuwa mtu wa kutoka morogoro(Mungu alaze roho ya marehemu mama pema peponi)

Baba alikuwa mfanyakazi kwenye bodi ya Pamba miaka hyo,,, kiukweli maisha yalikuwa safi tu,, tuliishi maisha ya wastani,,, hali ilianza kubadirika nilipofika darasa la tano,, kwani nakumbuka hapa ndipo misukosuko ilipoanza ugomvi nyumban haukuisha,, kipindi hcho nyumbani mkubwa nilibaki mm tu pamoja na mdogo wangu,, kwani Dada tayali alikuwa ameshaanza kujitegemea alikuwa mfanyabiashara,,,

Ugomvi mkubwa ulikuwa kwa sababu mama alikuwa anamtuhumu Baba ni mshirikina,,, kwani hata pesa alizokuwa anazipata alikuwa hafanyi maendeleo yoyote zaidi ya kushiriki shiriki tena kikubwa alikuwa anashirikiana na dada,, hawakuwa wanamsikiliza mama tena,,,kuna siku nilikuwa natoka shule nilipokarbia na geti la kuingilia ndani,,, nikasikia kelele kubwa za ugomvi wa baba na mama,,, hapa nilisikia Baba akisema "yote haya umeyataka mwenyewe kama hukutaka kumchota mwanao unyayo wake na Ndio yuko na nyota,,, unataka nn tena?? Mm ni mchawi Ndio, ni mapenzi yako Ndio yalikufanya uolewe na mm, sasa ni hv mm ntarudi hapa nikisikia umekufa vinginevo hutakuja niona nmekanyaga" baadae kidogo baba alitoka na kuondoka kipindi hicho marehemu mama angu alikuwa mgonjwa lkn hata dada yetu hakuwa na msaada kwa mama kwan alikuwa upande wa baba,,,,,

Kuhusu hyo ishu ya kumchota mtt unyayo ni hv,,, mama alikuwa na mtt mwingine kabla ya kuolewa na baba,,, yaani kaka yetu kipindi cha ugomv kaka alikuwa anasoma chuo huko dar so kuna kipindi alikuja likizo baba akawa anamshawishi mama amchote unyayo kaka yetu huyo,,, mama akagoma.

Bhasi baada ya Baba kuwa ametutelekeza na mama akiwa mgonjwa hali ilikuwa mbaya sana,,,, ilibidi niache shule na niingie mtaani kutafuta chochote,,,,baada ya miaka miwili mama alifariki,,, nakumbuka ile siku kwan alifariki juu ya mapaja yangu alinisimulia kila kitu hadi mambo yote ya baba ya ushirikina wake na ndugu zake,,,,

Siku ya msiba Baba alikuja pamoja na ndugu zake alitaka kuuchukua mwili wa marehemu mama yangu na kwenda kuuzika kwao maeneo ya Kagongwa eneo alilozaliwa Baba yangu,,,, lkn niliweka ngumu kila mtu alishangaa kwann namkatalia baba yangu ili hali nikiwa kijana mdogo tu,,,, mwsho wa siku mwili wa mama angu ulizikwa kahama na sio kagongwa tena,,,, baada ya msiba hatukuwahi kuongea na baba tena na hata dada angu,,,, nilibaki mm na mdogo wangu nyumbani,,,, wakti wa usiku tulipokuwa tunalala kwenye chumba cha mama yetu kulitokea kelele za ajabu Mara kwa Mara kuna siku nilipigwa makofi pasipo kumuona mtu,,,,, ili bidi nihame like chumba.

Tukio la pili la haya mauza uza toka mama amefariki ni siku moja nikiwa natoka garage (kwani baada ya kuingia mtaani ilibidi niende garage kujfunza kazi za ufundi),,, Nakumbuka hyo siku narudi nyumbani ilikuwa mwezi July hali ya hewa ilikuwa ya kawaida hakukuwa na dalili yoyote ya mvua,,,, basi kabla sijaingia ndani nikiwa nje ya nyumba nikafikia kwenye kenopu nikakaa pale kama dak 15 hv ghafra hali ya mawingu ikabadirika Mara upepo ukaanza,,,, manyunyu kwa mbali yakaanza ikabd niingie ndani,,,, ile naingia tu radi ilipiga jirani ya ile kenopu kulikuwa na nguzo ya umeme ile nguzo iliangukia pale pale kwenye kenopu nilipokuwa awali,,,,, aisee nilishangaa sanakuna matukio mengi sana yaliyokuwa yanafanyika pale kwa nyumban,,,, mwsho wa siku niliamua kuondoka na kwenda kutafuta maisha,,,,, maisha haya Ndio yakanikutanisha na huyu binti kutoka arusha,,,,,

SASA POINTI YANGU IPO HIVI
Baada ya kwenda arusha na kutambulishwa ukweni tukarudi mwanza na kuendelea na maisha hatimaye mke wangu akabeba mimba,,, kipindi cha mimba ikabidi mama ake aje kumuangalia pindi atakapojifungua,,,, baada ya kujifungua mama mkwe akarudi arusha,,,

Halo ndio picha ilipoanza kwani mke wangu anataka nmpeleke kwetu akapafahamu afahamiane na wazazi wangu pia,,, sasa mm naogopa kwani Baba navyomjua nahisi hawa wanangu anaweza kuwauwa kwani mambo kama haya tayali ameshayafanya kwa dada angu na hadi sasa hawapatani!!!

Mke wangu nmeshamuelezea kuhusu hali ya baba lkn anadai ni uongo tu nafanya hvyo kwa kuwa sina nae future!!!!

Naombeni ushauri wenu ndugu zangu,,,,, samahani sana kama story imekuwa ndefu sana.
 
Polee mkuu ila huyo mke wako anahitaji busara sana katika hilo asilazimishe mambo sana.
 
Pole sana mkuu kwa mtihani huo mzito aisee,cha msingi kuwa na msimamo katika hilo ulilomueleza mkeo na kamwe usiende huko maana mchawi huwa hatosheki na wala huwa hahitaji sababu yoyote ya msingi ili aweze kukudhuru.We mwambie mkeo kuwa mama alishafariki na baba hakuna uwezekano wa kwenda kumuona kama anataka mpeleke kwa kaka yako au mdogo wako aje akutembelee hao ndo ndugu zako waliobakia hakuna cha zaidi.Akikataa sana achague kukubali msimamo wako au akuache maana aweza kukusababishia majanga tena ukajikuta unaingia ktk mitihani mingine kama kupoteza watoto ambao ndio furaha yako.

Kila la kheri mkuu ningendako
 
Mpeleke tu mkeo kwa nduguzo sio lazima umpeleke kwa Baba...Fanya ivyo ili mkeo awe na Amani na wewe
Hayo mambo ya shirki muache tu Mungu
 
organize hata na wajomba/baba mdogo kama wao ni watu wema na ukamtambulidhe huko vinginevye.... majuto yatakiwa mjukuu
 
Mwambie aache mawazo ya ajabu, huna future nae ungeenda kwao?.

But ili kumuonesha kuwa unafuture nae, fanya mpango wa ndoa hata kama ni bila sherehe.
 
Pole Kiongozi una mtihani sana
Je baada ya kugombana na baba yako haujawahi kufikiria kurudi nyuma na kumsamehe? Mtaishi kwa kukwepana mpaka kifo?

Je akifa utakwenda kumzika?
Anyway hayo mambo ni magumu ila kikubwa tengeneza mazingira ya mkeo kujulikana kwenu
Nadhani una ndugu Wengine, mashangazi, wajomba dada na kaka pia.
Usisahau kufunga ndoa,
 
Haya mambo pamoja na kwamba huwa sina imani nayo lakini kama kweli yamtokea kwako just ignore hofu yake endelea na msimamo wako, USIMPELEKE KWA HUYO MZAZI MCHAWI, muoneshe upendo mke wako.
 
Baba yako wala sio mchawi, kupiga radi kwenye nguzo ya umeme ni kawaida. Mpaka sasa sijaona ushahidi wowote wa kwamba baba yako ni mchawi. Labda kama ulishawahi kumkamata na vitu vinavyohusiana na uchawi. Chukua mkeo mpaleke akapate baraka za mzazi wako
 
Tukisema uchawi siyo ishu tueleweke.

Walikua mapatna lakini baba akaamua kumharibia dada....

Mdogo wako wa kiume yuko wapi?

Kaka wa chuo yuko wapi?

Ndugu upande wa mama wako wapi?

Hao ndiyo ndugu zako watafute na mpeleke kwa hao.

NB. Sijataja ndugu wa baba kwakua uchawi huvuka kizazi kimoja kwenda kwa kingine. Kama baba mchawi inawezekana upande wake wapo wanga au wote ni wanga
 
Nadhani bidada ana hofu kwa kuwa hamjafunga ndoa. Anadhani unatafuta visingizio. Japo binafsi siwezi kushurutisha jambo kinalohusiana na ndugu wa mwenza wangu. Ye ndo anawajua vilivyo wazazi/ndugu zake. Yanini kujivika kibwebwe ilhali ugomvi si wangu?? Ili Kumridhisha, mkutanishe na ndugu yeyote.
 
Back
Top Bottom