BABA MCHAWI:Mke wangu anataka nimpeleke Nyumbani

BABA MCHAWI:Mke wangu anataka nimpeleke Nyumbani

Naona unaelekea kumpoteza mtu ambaye unampenda kwa dhati. Ushauri; nenda tu kamtambulishe mwenzio kwa baba, ndugu na jamaa, hayo mambo mengine ya ushirikina muachie Mungu atakulinda wewe na familia yako.
Na muda mrefu sana sina maelewano mazuri na mzee,,, toka kwenye msiba wa mama,, toka 2011 hatujawahi hata kupigiana simu
 
Hizi imani hizi. Anyways mke wako anahaki ya kuwa na wasiwasi. But kama huwezi kumpeleka kwa baba, basi atleast mu-introduce kwa ndugu yako hata mmoja, ulisema unamdogo wako. Je anamfahamu? Kama sio, basi mpeleke hata wakafahamiane.
Mdogo wangu wanafahamiana,,, ila yeye anadai kumjua mdogo wangu tu haitoshi,, anataka na baba amfahamu pia kama yy kwao wanavyonifahamu
 
Pole kwa mitihani
Ila naomba niulize mahusiano kati yako na hao nduguzako(kaka yako,mdogo wako pamoja na dada yako baada ya kukosana na mzee)yakoje hadi sasa.

Kingine,upande wa mama yako mna mawasiliano yoyote tangu kufariki kwa mama yako?

Na baba zako wadogo ama wakubwa mna mawasiliano?

Kama kuna mawasiliano mazuri upande wa mama yako mpeleke mama watoto wako kamtambulishe huko.

Lakini pia ukumbuke huyo bado akabaki kuwa baba yako mbali na mapungufu yake,ifike kipindi msameheane tu.

Mungu akuongoze na awalinde wewe na mama watoto wako
 
Pole sana mkuu kwa mtihani huo mzito aisee,cha msingi kuwa na msimamo katika hilo ulilomueleza mkeo na kamwe usiende huko maana mchawi huwa hatosheki na wala huwa hahitaji sababu yoyote ya msingi ili aweze kukudhuru.We mwambie mkeo kuwa mama alishafariki na baba hakuna uwezekano wa kwenda kumuona kama anataka mpeleke kwa kaka yako au mdogo wako aje akutembelee hao ndo ndugu zako waliobakia hakuna cha zaidi.Akikataa sana achague kukubali msimamo wako au akuache maana aweza kukusababishia majanga tena ukajikuta unaingia ktk mitihani mingine kama kupoteza watoto ambao ndio furaha yako.

Kila la kheri mkuu ningendako
Ni kweli kabsa mkuu,,, na mm hiki ndio nachokiogopa kupoteza furaha yangu,,, kwan baba ni mzazi wangu na atabaki kuwa hvyo lkn mambo aliyokwisha yafanya Yule mzee ni mnyama na sitaki hata aione familia yangu
Shukran sana kwa ushauri wako mkuu
 
Mpeleke tu mkeo kwa nduguzo sio lazima umpeleke kwa Baba...Fanya ivyo ili mkeo awe na Amani na wewe
Hayo mambo ya shirki muache tu Mungu
Kuna mdogo wangu anamfahamu tayali,,, nia yake ni kupafahamu nyumbani hasa mzazi pekee aliyebakii
 
Ni kweli kabsa mkuu,,, na mm hiki ndio nachokiogopa kupoteza furaha yangu,,, kwan baba ni mzazi wangu na atabaki kuwa hvyo lkn mambo aliyokwisha yafanya Yule mzee ni mnyama na sitaki hata aione familia yangu
Shukran sana kwa ushauri wako mkuu
Poa mkuu
 
organize hata na wajomba/baba mdogo kama wao ni watu wema na ukamtambulidhe huko vinginevye.... majuto yatakiwa mjukuu
Ndio nipo kwenye michakato hyo ya kumpeleka angalau upande wa mama angu
 
Pole Kiongozi una mtihani sana
Je baada ya kugombana na baba yako haujawahi kufikiria kurudi nyuma na kumsamehe? Mtaishi kwa kukwepana mpaka kifo?

Je akifa utakwenda kumzika?
Anyway hayo mambo ni magumu ila kikubwa tengeneza mazingira ya mkeo kujulikana kwenu
Nadhani una ndugu Wengine, mashangazi, wajomba dada na kaka pia.
Usisahau kufunga ndoa,
Hapana mkuu,, sijawahi kufikilia kumsamehe,,yule mzee ni mnyama ndugu yangu huwezi acha mkeo yupo kitandani na familia yake wanataseka kwa muda miaka miwili anakuja siku ya msiba,,sidhani kama ntakuja msamehe ila atabaki kuwa biological father tu

Ntafanya hvyo pia,,,mambo ya harusi yapo kwenye michakato tatzo ni hili kwanza
 
Sawa kiongozi Kila la kheri.
 
Mtafute yule kaka yako mkubwa kwa mama yako ikiwezekana uwende nae kwa wakwe Arusha kama kaka na mzazi wako
Dada kwenda ukweni haina shida,, kwani tayali nilishaenda peke yangu,, baadae mama mkwe akaja pia kumsimamia mwanae kujfungua,,, tatzo lipo kwangu kumpeleka kwetu sisi,, Kwa Baba mchota nyayo za miguu
 
Haya mambo pamoja na kwamba huwa sina imani nayo lakini kama kweli yamtokea kwako just ignore hofu yake endelea na msimamo wako, USIMPELEKE KWA HUYO MZAZI MCHAWI, muoneshe upendo mke wako.
Upendo upon mkuu,,, familia inaishi poa tu kwan ndio furaha yangu hii,,, tatzo ni hili, pia ukiangalia mwanamke yupo sawa kudai kupelekwa ukweni kwake
 
Baba yako wala sio mchawi, kupiga radi kwenye nguzo ya umeme ni kawaida. Mpaka sasa sijaona ushahidi wowote wa kwamba baba yako ni mchawi. Labda kama ulishawahi kumkamata na vitu vinavyohusiana na uchawi. Chukua mkeo mpaleke akapate baraka za mzazi wako
Yule ni mzee wangu ndugu yangu,,, kwan haya malalamiko sio ya kwangu peke yangu hata Watt wengine wamemtenga
 
Tukisema uchawi siyo ishu tueleweke.

Walikua mapatna lakini baba akaamua kumharibia dada....

Mdogo wako wa kiume yuko wapi?

Kaka wa chuo yuko wapi?

Ndugu upande wa mama wako wapi?

Hao ndiyo ndugu zako watafute na mpeleke kwa hao.

NB. Sijataja ndugu wa baba kwakua uchawi huvuka kizazi kimoja kwenda kwa kingine. Kama baba mchawi inawezekana upande wake wapo wanga au wote ni wanga
Kaka wa chuo yupo Dar anafanya maisha yake huko,,, huyu tumechangia nae mama ila baba ni tofauti kwa hyo hata ukarbu sana haupo japo tunapatana na yy ndio alikuwa mhanga wa kwanza juu ya tabia ya mzee

Khs mdogo wangu,, yy yupo Moshi anafanya maisha yake pia
Ndugu wa upande wa mama wengi wao wapo morogoro,, huko ndio nakofikilia kumpeleka mke wangu huyu
 
Kuwa mkali ehee mtu ushamueleza kila kitu lakini anakazania.

Mpeleke kwa mama wadogo, wajomba na mashangazi.

Ila kwa baba yako usikanyage.
Haina jinsi aisee inabd nimpeleke kwa upande wa mama

Lkn khs kwenda kwa baba,, Kule siwezi fanya kitu kama hcho kwan ukweli mm ndio naufahamu khs mzee
 
Pole kwa mitihani
Ila naomba niulize mahusiano kati yako na hao nduguzako(kaka yako,mdogo wako pamoja na dada yako baada ya kukosana na mzee)yakoje hadi sasa.

Kingine,upande wa mama yako mna mawasiliano yoyote tangu kufariki kwa mama yako?

Na baba zako wadogo ama wakubwa mna mawasiliano?

Kama kuna mawasiliano mazuri upande wa mama yako mpeleke mama watoto wako kamtambulishe huko.

Lakini pia ukumbuke huyo bado akabaki kuwa baba yako mbali na mapungufu yake,ifike kipindi msameheane tu.

Mungu akuongoze na awalinde wewe na mama watoto wako
Mahusiano kati yangu na hao ndugu zangu wengine yapo vzr tu,,, Dada yetu pekee ndio alikuwa hayupo nasi ila baada yy kukorofishana na mzee,,, akarudi upande wetu

Kuhusu upande wa mama,kule kuna mawasiliano vzr tu carba

Ila kwa upande wa baba,, hakuna mawasiliano mazuri kwan wanadai kitendo cha kukatalia kuuchukua mwl wa marehemu mama yetu ni dharahu kwa hyo hawakupenda toka kpnd hcho hakuna maelewano poa

Ni kweli atabaki kuwa baba angu tu,, hata mm sijakataa kwa hlo ila juu ya vtendo vyake sidhani kama nitasamehe

Shukrani carb!!
 
Back
Top Bottom