Baba Mbasha: Flora alichoka kuishi na mwanangu

Baba Mbasha: Flora alichoka kuishi na mwanangu

Halafu yaani ndoa tokea 2002,wana mtoto mmoja tu.Ila mkwe wake inaonekana anataka ndoa iendelee,najiuliza kwa nini Flora hataki ndoa?si aliapa mpaka kifo kiwetenganishe

Si ungemuuliza huyo mzee Maneno mengi na Nkewe.Ukiwa na wazazi wa aina hii chunga sana.kaa mbali nao kabisa.mara nyingine wanavizia miradi ya Flora.Mtu anayefahamu maana ya ndoa ya mume na mke asingeita press kutoa taarifa kivyake vyake.kwa jumla hawafai kabisa kabisa.
 
Flora tapeli tu
kuna mwaka alikwepo singida mjini,pale kanisa la roma,alikuwa akizindua album yake km sikosei
kabla ya kuimba akasimama jukwaani na kuahidi eti atajenga hospitali,aliongea kwa bashasha kweli,yapata miaka karibu mitano sasa hata kiwanja hajapata

flora ni tapeli tu,hata sura yake inajieleza

Sure broo nakumbuka sana wanakwaya walishindanishwa wakaachiwa hewa
 
Hivi Emma Mbasha anafanya kazi ganii!!!???
 
Wokovu ni wa mtu mmoja mmoja
Kila mtu na nafsi yake
Mungu hahukumu Kanisa anahukumu nafsi ya Mtu
Olé wako wewe unaehukumu Wokovu kwa ajili ya kanisa flani
Hukumu nzito ipo juu yako
 
Kwanini amuite Frola kumpokea stand na si mwanae! Huu ni unafiki wa kwanza wa huyu mzee! Na kwanini afike Ubungo ndio ampigie simu akampokee, kwanini asimpe taarifa kabla hajaanza safari! Hii haijakaa sawa, hata mimi mtu akitoka mkoani agike ubungo aniambie nikampokee siwezi kwenda!

Mzee anasema mwanae alikuwa mkoani kumsalimia ndugu ambae ni mgonjwa..hapa flora ana kosa maana alivopigiwa simu na baba mkwe wake akampokee alikua na uwezo wa kusema kuwa hawezi kuja kumpokea na mzee wa watu akatafuta njia nyingine..sasa Flora yeye akamjibu nakuja baba wa watu akakaa stand masaa matano anasubiri...alivoona kimya akajua Flora kaingia mitini which is not good.
Huyu ana mambo mengi yaliojificha tusioyajua...
 
Mzee anasema mwanae alikuwa mkoani kumsalimia ndugu ambae ni mgonjwa..hapa flora ana kosa maana alivopigiwa simu na baba mkwe wake akampokee alikua na uwezo wa kusema kuwa hawezi kuja kumpokea na mzee wa watu akatafuta njia nyingine..sasa Flora yeye akamjibu nakuja baba wa watu akakaa stand masaa matano anasubiri...alivoona kimya akajua Flora kaingia mitini which is not good.
Huyu ana mambo mengi yaliojificha tusioyajua...

Huyu baba ana wake wangapi?Uaminifu wake una mashaka sana.Mwanae hakuwepo.tena anajua ameenda kutizama bibi yake aliyevunjika mguu.sasa alienda kwa Mbasha kuwapatanisha nani?Kwa nini yeye hakwenda kumuona mgonjwa?
 
mwimbaji km mkewe aliyekimbilia kwa mch.gw

Bibie Flora atakua aona yeye na mumewe mbasha wamefulia kwa sasa akatafuta namna ya kumkimbia mumewe ili atoke na mchungaji mwenye pesa...according to madai ya mbasha mwenyewe..dah kweli pesa mwanaharamu
 
Baba mzazi wa Emmanuel Mbasha, Mzee Maneno amefunguka kuwa mwimbaji wa Injili Flora Mbasha alichoka kukaa na mwanaye ndiyo maana mgogoro wao umefika hatua hii.



Hiki ni kipindi cha mzazi kuonyesha hekima yake kwa kuchagua nini cha kuongea, ukiwa mpayukaji unaharibu zaidi badala ya kutengeneza
 
Last edited by a moderator:
Interview ingekuwa nzuri kama kungekuwa na mdahalo kati ya wazazi wa Flora na Emmanuel, kwani wakati wazazi wa Emmanuel wanamtetea mtoto wao, basi wazazi wa Flora nao wangekuwa wanamtetea mtoto wao..

Mimi ningekuwa mzazi ningekataa kuongea na vyombo vya habari..kwani ukweli na siri ya mzozo wanajua Mke, Mume na Mungu tu...

Binadamu wote ni dhaifu na sio watakatifu, kuimba nyimbo za injili, kusali au kuswali sana, au kuongoza ibada hakutaondoa ubinadamu wako..kama kuanguka utaanguka tu..kwani tunajiandaa kwa maisha ya kiroho na sio kimwili...

Msiwahukumu hao wote wawili kwa maneno wanayosema mdomo... kama mnao uwezo basi muwahukumu kwa ukweli uliojificha ndani ya mioyo yao wote wawili...
 
Sina hamu na makanisa ya kilokole, yaani siku hizi nimesimama mimi kama mimi.

Huo ndo uamuzi sahihi. Kama una access nzuri ya internet basi ukitaka nyimbo mwangalie Kim Walker Smith, ukitaka mahubiri muangalie Bro Zac Poonen. Hawa mimi nimeona wananafuu maana nikiwa nyumbani kwangu napata chakula cha roho
 
Dar es Salaam. Kuna kila dalili kwamba
mwimbaji maarufu wa muziki wa Injili nchini,
Flora Mbasha na mumewe Emmanuel Mbasha
wanatamani kurudiana, baada ya kuwapo
mgogoro katika uhusiano wao wa ndoa,
ulioingia katika vyombo vya habari yapata
mwezi mmoja sasa.
Kwa nyakati tofauti jana, kila mmoja wao
alimwambia mwandishi wetu kwamba yupo
tayari kurudiana na mwenzake, hatua ambayo
inaweza kuondoa mgogoro huo ambao
umefifisha taswira yao ya kiutumishi.
Akizungumza nyumbani kwake Tabata
Kimanga, Dar es Salaam, Mbasha alisema
ameshamsamehe mkewe na kwamba
anamsubiri muda wowote arudi nyumbani
kusuluhisha mgogoro wao.
“Nawapenda Watanzania wote wazidi
kutuombea ili mimi na mke wangu turudiane.”
Kauli hiyo ni sawa na ile aliyoitoa Flora wiki
iliyopita pale aliposema: “Ninawaomba
Watanzania waendelee kuniombea ili niweze
kushinda majaribu haya, kilichotokea ni
sehemu tu ya kupimwa imani yangu”.
Jana, Flora alirudia kauli hiyo kupitia kwa
wakili wake, Addo Mwasongwe ambaye
alisema mwimbaji huyo yupo tayari kukutana
na mumewe na ndugu ili waondoe tofauti zao.
Maelezo ya Mbasha
Kwa upande wake Mbasha alisema: “Mi
namwomba Flora ajishushe akubali, aje home
(nyumbani) tuyamalize na maisha yaendelee.
Yeye ni mke wangu namtaka. Kama
ananipenda arudi, tuite wazazi tutatue
mgogoro huu.”
Aliongeza kuwa hakuna binadamu yeyote
asiyesamehewa na kwamba kilichotokea
katika ndoa yao ni sehemu ya maisha ambayo
wengi hupitia.
“Siku zote naamini tunachotakiwa ni kujenga
na siyo kubomoa… Flora asing’ang’anie kwa
watu arudi hapa… apige hodi… ‘mume wangu’
nimerudi …na mimi nitampokea tuendelee
kulea watoto.”
Mbasha anakabiliwa na tuhuma za kumbaka
shemejiye wa miaka 17 na kesi yake
inaendelea katika Mahakama ya Wilaya ya
Ilala na sasa yupo nje kwa dhamana.
Kauli ya Flora

Wakili Mwasongwe alisema: “Flora amesema
ameshayatoa rohoni masuala yote ya
mgogoro na mumewe na leo (jana) aliniambia
anataka kusuluhishwa hata kesho (leo) lakini
nimeshindwa kuwakutanisha kwa sababu nipo
‘busy’.
“Ila nilimwambia Ijumaa hii nitafanya hivyo
kwa kuwakutanisha yeye (Flora), Mbasha na
wazazi wake ili kumaliza tofauti hizo.”
Wakili huyo alisema awali alikutana na wazazi
wa Mbasha lakini hawakufikia mwafaka, lakini
kwa sasa anaamini mambo yatakwenda vizuri.

by: MCL
 
Back
Top Bottom